Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Kweli kila nchi na tamaduni zake, msosi pia ni sehemu ya tamaduni. Wakati bongo tunajivunia chipsi yai, au supu chapati usichukulie poa, Mrisho Ngasa na Kapombe walishindwa kucheza Ulaya kisa chipsi yai.

Turudi kwenye mada, nikiwa Cape town, nilishuhudia watu wakila soda na mikate kama mlo, Zimbabwe, Zambia, USA wataita hotdog Ila ndio huohuo, Ulaya ukipandisha bei ya mkate utapata shida Sana.

Kwa wakristo sala ya Bwana kuna ile phrase ya our daily bread imekuwa termed kama chakula, hata Yesu Alisha watu elfu tano samaki na mkate. Mkate ni chakula sio kitafunwa Kwa wenzetu.
Nyie wasukuma bila kula ugali sufuria nzima hamuoni kama mmekula kitu.
 
Nawakumbuka vizuri sana hao wa kijijini ila hakuna kazi ngumu sikuhizi
Zamani watu walilima kwa mkono au wanyama.
Siku hizi kuongeza ufanisi Trektor hutumika maana kwa siku hata Hekta 10

Kwenye migodi siku hizi crusher zipo, watu hawatumii nyundo kusaga mawe

Maji vijijini yapo siku hizi
 
Mikate ya Ulaya usifananishe na hii yenu kama Godolo, Nenda Supermarket kubwa huw wanaileta, mkate unazuwa sh 7000/ kuna mikate Whole grain acha kabisa ile wanakula matajiri, shida tusha kalili
Shoppers wana hiyo mikate inauzwa hadi 12000

Huwa najiuliza wanailetaje
 
Back
Top Bottom