Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Kenya kwa msosi ni hovyo kabisa...japo naikubali Nairobi kuliko jiji lolote EA.
MK254

Kila mtu ana kile alichokiezoea kulingana na makuzi yake na asili ya watu wake, hii mipaka ya mzungu sijui kwanini huwavuruga Watanzania, unapaswa ufahamu hamna chakula cha nchi ila kila jamii au kabila lina aina yake ya misosi.
Kwa mfano Wasukuma wa Tanzania wanapenda ugali, na ndivyo ilivyo kwa Waluhya wa Kenya, ukienda kwa Wapare wanapenda makande, na ndivyo ilivyo kwa Wakikukuyu wa Kenya.

Ukishuka kwenda Pwani za nchi zote mbili unakuta huko ni mwendo wa biriani, hivyo ni vigumu kusema chakla fulani ni cha Wakenya au Watanzania maana hii ni mipaka ya mzungu iliyokuta jamii za watu wanaishi kwa tamaduni zao.
 
Mkuu unaweza kuwa uko sahihi, lakn niliwahi kusikia kuwa Chips yai (zege) Iko Tanzania tu. Ni kweli?
 
Mkuu unaweza kuwa uko sahihi, lakn niliwahi kusikia kuwa Chips yai (zege) Iko Tanzania tu. Ni kweli?

Ipo Pwani ya Kenya pia, kule unakuta na Pweza na aina ya misosi ambayo mumezoea huko Dar, maana kumbuka Dar, Tanga hadi Mombasa wote huo ni ukanda mmoja wenye watu wanaoendana kidesturi.
Sisi wa mikoani tuna misosi yetu pia....
 
Slices 12!! Rey bhana hapo umetuuza,
Mimi nakula sana mkate na hata usiku huu nimetoka kula huo huo na Mayai mwanzo nilikula wali ukawa haushuki kabisa nikaachana nao nikapiga mkate wangu niko fresh kabisa,

Slices 2 tu hua sizidishi hapo.
Unaishi kizungu sana
 
Kimsingi Nyumbani kwako hutakiwi kukosa mkate na trei ya mayai.

Hiki ni chakula cha haraka ambacho hakihitaji ujuzi wowote kuandaa.
 
Baby wangu anapenda mwenyewe ananiita English Figure "rahisi kubebeka na kukunjika" [emoji3060][emoji3060][emoji3060]
English figure siyo kuwa skeleton kama Mange, bahati nzuri nimeishi Uingereza mademu wazuri na wana tako kama kawaida.

Hata ukipanda British airways air ostes wao siyo skeleton ingawa hakuna tunyetunye.
 
English figure siyo kuwa skeleton kama Mange, bahati nzuri nimeishi Uingereza mademu wazuri na wana tako kama kawaida.

Hata ukipanda British airways air ostes wao siyo skeleton ingawa hakuna tunyetunye.

Sasa Dr mimi sio Skeletoni kama Mange maana sitafuti vibabu vya kizungu, nina kishepu changu cha uchokozi na kifua kilichojaa vizuri siwezi kua tukunyema pia[emoji23][emoji23][emoji23]
 
As mahindi yalivyo junk ndivyo mkate ulivyo junk, ni ujinga tu ushamba vinakusumbua. KUNA kitu kinaitwa utamaduni, kiheshimu tu, na kina maana sana
Mahindi tumeletewa na mabeberu ndio maana tumekuwa mazezeta na watu wengi wanaamini Mahindi ni ya Mwafrika na ndio utamaduni wake tumeacha kula ugali wa mtama na mihogo tumekimbilia kwa mabeberu na kuona ndio utamaduni wetu kumbe sio...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…