Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Kweli kila nchi na tamaduni zake, msosi pia ni sehemu ya tamaduni. Wakati bongo tunajivunia chipsi yai, au supu chapati usichukulie poa, Mrisho Ngasa na Kapombe walishindwa kucheza Ulaya kisa chipsi yai.

Turudi kwenye mada, nikiwa Cape town, nilishuhudia watu wakila soda na mikate kama mlo, Zimbabwe, Zambia, USA wataita hotdog Ila ndio huohuo, Ulaya ukipandisha bei ya mkate utapata shida Sana.

Kwa wakristo sala ya Bwana kuna ile phrase ya our daily bread imekuwa termed kama chakula, hata Yesu Alisha watu elfu tano samaki na mkate. Mkate ni chakula sio kitafunwa Kwa wenzetu.
Kiswahili sahihi ni vitafunio. Tatizo letu siku hizi tunajua sana Kiswahili
Logic behind ya mkate au kitumbua kuitwa vitafunio ni kwamba mtu akinywa chai bila mkate au kitumbua, hawezi kutafuna kwa sababu atakuwa anameza tu chai kama maji. Sasa ili mtu aweze kutafuna wakati anakunywa chai, anahitaji kitu kama mkate au chochote cha kumfanya aweze kutafuna, na ndiyo maana vitu hivi vikaitwa vitafunio.
Kama mkate na vitumbua n.k. vitaitwa vitafunwa, kwa nini ugali au wali hatuviiti hivyo? Kwa sababu hata ugali au wali navyo pia huwa vinatafunwa.
 
Kweli kila nchi na tamaduni zake, msosi pia ni sehemu ya tamaduni. Wakati bongo tunajivunia chipsi yai, au supu chapati usichukulie poa, Mrisho Ngasa na Kapombe walishindwa kucheza Ulaya kisa chipsi yai.

Turudi kwenye mada, nikiwa Cape town, nilishuhudia watu wakila soda na mikate kama mlo, Zimbabwe, Zambia, USA wataita hotdog Ila ndio huohuo, Ulaya ukipandisha bei ya mkate utapata shida Sana.

Kwa wakristo sala ya Bwana kuna ile phrase ya our daily bread imekuwa termed kama chakula, hata Yesu Alilisha watu elfu tano samaki na mkate. Mkate ni chakula sio kitafunwa Kwa wenzetu.

Mkuu umesema kweli

Ila ukizamia kidogo Tu utaona hao jamaa hawana vyakula mbadala kama kwetu TZ.

kwa mfano hapa kwetu Mwanza, mikate ni chaguo la kumi na moja huko maana kuna viazi, mihogo, magimbi, chapati (n Aina zake), maamdazi, vitumbua, kacholi, kababu, ...mikate haifikii uhondo wa hivi vyakula.

Jambo la pili kwa wenzetu mikate ndio cheapest, vyakula vingine ni ghali sana.

Ndio kusema kuhusu misosi TZ tupo vizuri mno
 
Mimi slice 4 za mkate mayai ya kukaanga 3 glass ya juice na tunda kama parachichi tikiti etc usiku natosheka kabisa
Nchi za Wala Mikate wale wa Maisha ya kawaida, wanakula Mkate na Soda, kuna Vitu vichache tu wanalia na Mkate, kwa South Africa wanakula Chips na Mkate!
 
Tatizo hata mikate yetu imechakachuliwa,haina ladha,mikavu Sana na kipimo ni kidogo. Ili mtu ashibe labda ale miwili,so familia ya kisukuma kwa siku labda wale kirikuu nzima.
Bado kitakuwa chakula ghali Sana kwa mtanzania.
ule mkate wa yesu ulikua ni mgumu sana, mkate walikuwa wanatumia nguvu kuukata na ulikuwa unatoa mlio
 
Unalosema ni kweli kabisa na ninashangaa inakuaje hapa bongo kunakuwa na tatizo la nguvu za kiume wakati tuna vyakula vyenye nguvu na virutubisho.

Sasa mfano SA nilifika nikakuta machakula hayaeleweki nikajiuliza hawa wanaishije. Nadhani kibongo bongo tuna tatizo la kukinai ngono lakini kwa nguvu siamini hata kidogo kwamba kwa kula chipsi yai ndio kufanye mtu asiwe na nguvu za kiume wakati zipo nchi hawajui wali na wakipika wali wao utakimbia.
Mambo ya nguvu ni mfumo wa maisha wenyew,mtu unawatoto 5,unaishi nyumba la kupanga,watoto wanataka wasome,mke asuke,kodi,umeme,maji kipato hakieleweki unafikiri utaishi vipi.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Punguza ujuaji kenge wewe sio lazima kila post uchangie
Mahindi tumeletewa na mabeberu ndio maana tumekuwa mazezeta na watu wengi wanaamini Mahindi ni ya Mwafrika na ndio utamaduni wake tumeacha kula ugali wa mtama na mihogo tumekimbilia kwa mabeberu na kuona ndio utamaduni wetu kumbe sio...

Mahindi yanalika na wazungu sana tu, ni kwamba hujielewi na hauna exposure, ugali ni utamaduni, lakini ulaji wa mahindi unalika sana Europe ans UA
 
Tatizo hata mikate yetu imechakachuliwa,haina ladha,mikavu Sana na kipimo ni kidogo. Ili mtu ashibe labda ale miwili,so familia ya kisukuma kwa siku labda wale kirikuu nzima.
Bado kitakuwa chakula ghali Sana kwa mtanzania.
🤣🤣🤣🤣🤣 Aiseee!

Tatizo la waTz hatuli mboga mboga, tuna utamaduni fulani hivi katika ulaji ambao haupo popote. Mtu anapika jungu kubwa la ugali, vinyama kidunchu na vimboga vya majani kidunchu. Jungu la ugali linatakiwa kuwa sawasawa na jungu la mboga za majani, (kwani majani bei gani?) watu wale majani kama wanavyokula ugali.

Mtu anapika mboga anaweka karoti nusu, hoho robo! 🤷🏻‍♀️ kuna upishi tumefundishwa toka wadogo ambao si mzuri/si wa afya. Ndio maana ni mwendo wa ma** magumuuuuu!

Tule mboga mboga, tule chakula cha maji maji, tunywe maji kwa wingi.
 
Dah! Wakati nasoma Udsm miaka ile! Nilikuwa nakomunika kwa mkate na chai asubuhi na jioni. Naikumbuka sana ile mikate yangu pendwa ya super loaf! Sijui bado ipo huko mjini Darisalama!!
 
Mahindi yanalika na wazungu sana tu, ni kwamba hujielewi na hauna exposure, ugali ni utamaduni, lakini ulaji wa mahindi unalika sana Europe ans UA
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya ulaji wa ugali na matumiz ya maindi ,sisi waafrika tunatumia mahindi kwa matumizi ya ugali lkn wenzetu ugali hawali (sio utamaduni wao) ila wanatumia mahindi kwenye vitu vingine.

Wazungu kutokula ugali baadhi ya watu wamechukulia kama ni chakula kisicho faa kutumia.

Huu ni utamaduni tu wa watu ambao watu wanakuwa wameuzoea kwa mfano inchi kama china , Korea na Japan wanapendelea sana tambi hivyo ngano hawapendelei sana iwe mikate bali wanafanya kuwa tambi pia mchele wanakula wali lkn pia wanatengeza tambi za mchele hata hivi viazi (potato) wanatengeza kwenye mfumo wa tambi

Hio ni kwasbabu ni utamaduni wao ndio uko hivyo lkn wote tunatumia hivyo vitu kwa tofauti na wao.
 
Back
Top Bottom