Nawasalimia wanabodi.
Inatia hasira,
Inakera,
Yaani hakuna watu nawachukia kama Wanaharakati uchwara wa hii nchi,hakuna watu nawachukia kama hawa.
Mwanzo nilikuwa nawaona ni watu wa maana,lakini kwasasa nimewapuuza mpaka basi ni wajinga na ni hatari Kwa usalama wa nchi.
Wengi wapo abroad halafu wananufaika na machafuko huku watoto wa kitanzania watoto wa masikini wakiozea kwenye kuta za magereza huku wengine wakipoteza maisha.
Ukweli ni kwamba ,
Augustine Mrema alikuwa na lengo la kuleta Mabadiliko,
Hali kadhalika Wilbroad Silaa,
Ukiondoa Ibrahim lipumba na CUF yake,waliobaki wote ni madalali na matapeli wa kisiasa ambao wapo kwaajili ya familia zao ,wanamiliki biashara na miradi mikubwa huku wakijifanya wazalendo wapigania haki na wanademokrasia,kumbe wanawatumia vijana kama mitaji ya kupata pesa chafu na haramu kutoka ng'ambo.
Huwa nazurula mitaa ya Twitter nakutana na watu ambao Wana midomo michafu na hawana hoja za msingi ,Hadi unajiuliza yaani hawa watoto wa Kiswahili, ndiyo wapewe nchi?
Kataa vurugu,
Kataa ujinga,
Linda Amani ya nchi.