Nchi za Afrika za Francophonie na Common wealth zinalipa Trillion 3000 kila mwaka kwa Ufaransa na Uingereza kama fidia ya faida za ukoloni

Nchi za Afrika za Francophonie na Common wealth zinalipa Trillion 3000 kila mwaka kwa Ufaransa na Uingereza kama fidia ya faida za ukoloni

H
Watu bilioni 1.5 wanafanyakazi usiku na mchana, kwa miaka zaidi ya 60 ya uhuri, na bado hatuna hata ambulance tu za kueleweka ni shida.., pesa zote zinaenda wapi? Commomwealth sisi mtego wetu upo IMF na World bank.., kataa kukopa pesa uone kitakachokupata,uliza Djibouti walifanywa nini baada ya kugoma kukopa. Yaani. Unakopa Trillion 2 kwenye makaratasi, mkopo wenyewe hauji, ila unatakiwa ulipe Trillion5 na riba, mnamuonea mama wa watu bure kumuuliza pesa alizokopa zimeenda wapi, mnamuonea bure! Hakuna anaependa kufa jamani, huo ushujaa alikuwa nao jiwe tu! Tuombe sana aje mwingine atakaekuwa tayari kufa, kama Burkinafaso walivyompata yuke dogo..
Mkuu FRANCIS DA DON ni nchi zipi hizo walizong'oa miundombinu,kuchoma maghala na kutia sumu visima? Unaweza kujitajia?
 
Sasa kumbe tunabishana nini? , maana unachosema ndicho ninachosema.., kwamba Africa inanyonywa..
Tofauti yangu na wewe ni kwamba wewe unalaumu Wafaransa wana mikataba ya siri mibaya ambayo Waafrkka hawawezi kujiondoa wakijiondoa wanauawa.

Mimi nasema mikataba hiyo ya CAF/Ufaransa iko wazi inajulikana na tatizo ni viongozi wa Afrika wanaoangalia interests zao zaidi ya za Wafaransa.

Achana na hao Wafaransa, Thabo Mbeki rais msomi wa Afrika ya kusini, aliyeanzisha idea ya "African Renaissance", idea ya kuirudisha Africa katika kujitambua na maendeleo, alitia saini mkataba wa doka bili9ni 10 za kampuni ya BAE ya Uingerwza kuhusu manunuzi ya sioaha (dellal kama la radar enzi za Mkapa, na kampuni ile ile).

Thabo Mbeki alijua kuwa BAE imezidisha bei ya silaha kwa mara mbili na nusu, na Afrika ya Kusini haikuhitaji hizo silaha. Na kwamba hizo hela ni nyingi sana na zingeweza kutumika kwenyw shughuli nyingi sana za kijamii, including kusaidia kupigana na HIV/AIDS South Africa.

Lakini Thabo Mbeki aliamua kununua sulaha kwa sababu tu wazee wa ANC walikuwa wanapewa rushwa ya dola za Marekani milioni 300 ambazo walitaka kuzitumia kwenye uchaguzi.

Tanzania tulipigwa deal kama hilo kwenye ununuzi wa radar mpaka Claire Shirt akaibana BAE tukarudishiwa sehemu ya hela.

Na hapo itaona Tanzania na South Africa hazijatawaliwa na Ufaransa.

Sasa hapo utasema tatizo ni Wafaransa au viongozi wa Africa?

Tafuta documentary inaitwa "Shadow World : Inside The Global Arms Trade" uangalie jinsi biashara ya silaha ilivyogubikwa na rushwa na jinsi viongozi wa Afrika wanavyojiingiza kwenye hii rushwa kwa hiyari yao wenyewe.
 
Ukoloni hauja wahi ondoka katika bara la Afrika,bali ulibadilika kuendana na hali ya mageuzi ya kipindi hicho.

Mwafrika kajikuta yu katika Ukoloni wa mwafrika mwenzie na huyo mkoloni mweusi yuko katika Ukoloni wa Beberu.
Inawezekana kabisa ,maana hata hawa puppets wanaongoza hizi nchi ukiangalia impunity Yao unaona kabisa hawa ni nyapara na kuna master nyuma yao
 
Fake news, hizo nchi kwanza hazina uwezo wa kugenerate hizo dollar billioni 500 kwa mwaka za kulipa kadeni na bado zijiendeshe

Hakuna Siri sa ivi duniani kwenye ulimwengu wa kidijitali, labda uniambie hua wanalipana hizo pesa kwenye magunia, ila kama ni transactions za kibenk ingekua ishajulikana kitambo tu,

Btw, nchi Gani hizo mbili ambapo wafaransa walifanya ivo?
We hujui sabotage ya France kwa Guinea mwaka 1960 baada ya kuamua kuwa na Currency yake?
We hujui CFA kule West Africa ina majukumu gani?
We hufahamu ni kampuni za nchi gani zinashikilia uchimbaji wa madini na mali asili kwenye hizo nchi za Africa Magharibi?
 
Usiende Mbali Tanzania hii kuna Mgodi umejazwa maji na kutiwa SUMU. Wakoloni walikasirika kufurushwa. Wamekuja Waturuki na Wachina wameushindwa wametoa ripoti kwamba maji na Sumu yaliyojazwa kwenye huo Mgodi ukiyavuta kuja Nchi kavu yataathiri vyanzo vyote vya Nchi kavu na watu watapoteza Maisha.

Mgodi Upo Mpanda Mjini Mkoa wa Katavi eneo la Kampuni. Reli ya kutoka Tabora Mpanda inaishia ndani ya Mlima/Handaki la Mgodi huo wa Dhahabu. Afrika tumeonewa sana na makaburu.
Napajua pale,aysee kumbe story behind ndio iko hivi? Hii ngozi nyeupe hatari sana
 
Mrusi kaanza kazi ya kunyoosha huyu mshenzi ,Mali , Bukinafasso na Niger sasa hivi mfaransa kafurushwa huko .
Mali, Burkinafaso na Niger wamefanikiwa kumtimua Mfaransa sababu wamehakikishiwa ulinzi na Putin, hata hivyo kuna pesa kidogo wanailipa Russia kwa ajili ya ulinzi, maana ulinzi ni gharama, ila bora kumlipa kidogo Putin kuliko kunyonywa kiasi kile na Ufaransa
 
Back
Top Bottom