Anakuwa Mungu aliyeumbwa si ndivyo?Jina alilorithi yesu ndilo linalobeba mamlaka yote juu ya mwanadamu. Pamoja na kupewa mamlaka juu ya wote wenye mwili bado haimaanishi kwamba yeye ndiye Mungu baba hapana, Bali anabaki kuwa mwana wa Mungu lkn mwenye mamlaka juu ya wanadamu wote.
Sijui Nini ambacho huelewi mbona nimeeleza vizuri Sana?Anakuwa Mungu aliyeumbwa si ndivyo?
Ukweli mchungu: Tutate tusitake hao jamaa wamefanikiwa sababu ya uelewa na akili nyingi na sio nchi za Kikristo tu tuseme nchi za Wazungu. Waislam wamekuwa wepesi wa kurubuniwa sababu ya kuamini sana 'extremism' na kuacha kufikiri matokeo ya baadae najaribu kuliweka sawa hili ili nisijitukane maana mi mwenyewe Muislam.
Watawala wa dunia wametumia mbinu ya kugombanisha watu husika ili kufanikisha mambo yao na hata Wazungu kabla ya kujitambua walishapigana sana miaka hiyo kuanzia vita za ndani (wenyewe kwa wenyewe), za kidini na za nchi na nchi. Sasa wao walishastaarabika wamejua adui nani nani rafiki. Hatakama vikundi vya mlengo wa kulia vipo lakini huwezi kusikia wameanzisha mauaji dhidi ya wale wasioamnini itikadi zao.
Kwa dunia ya sasa wajinga wamebaki Africa na Asia (sana nchi za kiarabu) tunauwana kwaajili ya mali na dini wenyewe kwa wenyewe au na majirani zetu wakati huo mtawala wa dunia anafaidika na mali zetu
Imani Yao imejengwa kwenye mizizi ya Kuua Kwa wale wasioamini miungu au mungu wao. Ni uendawazimu kulazimisha watu kua kama wewe na unawaua wale usiokubaliana nao.
Upendo pekee ndio unaleta furaha na amani katika jamii, si vitisho na Yesu alituonyesha haya katika maisha yke hapa Duniani.
Yesu na Mungu Ni baba na mtotoMimi binaadamu nikizaa mtoto atakuwa mwanangu, mimi na mwangu ni binaadamu wawili na si mmoja. Kwahiyo kama Yesu ni Mungu na Baba yake ni Mungu hivyo hapo tunazungumzia Miungu wawili.
Waarabu sio ndugu zako mkuu. Au wewe umeona mmatumbi huko mbagala analipua watu? Hao ndio ndogo zako sasa. Sasa wewe sijui unaongelea ndugu gani hao.Wanaishi kwa kilichoandikwa kwenye maandiko.Ndg zetu waislam wao wameambiwa wakifa wakimpigania mola wao mlezi kuna mademu bikira 72 na mikenyenge itakuwa na nguvu haswa.Wee huogopi?
Sasa unataka kunipinga Mimi au unapinga maandiko? Wala usichanganyikiwe mtaalam. Mtoto wa Mungu Ni Mungu iko hivyo na ukitaka kujua zaidi Ni kwamba; unajua kwanini tunakufa? Au kwanini tulikatazwa kula tunda? Sababu Ni hiyohiyo ya umungu ndani yetu. Tumeumbwa kwa sifa zote za kimungu.
Waarabu sio ndugu zako mkuu. Au wewe umeona mmatumbi huko mbagala analipua watu? Hao ndio ndogo zako sasa. Sasa wewe sijui unaongelea ndugu gani hao.
Hi picha ilizua utata Sana.
View attachment 3180171
Ukiisoma biblia vizuri huwezi niuliza swali Hilo,Biblia inasema kwamba:
1. Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu. (Kutoka 4:22).
2. Daudi ni mwana wa Mungu, yeye pia ni mwana wa kwanza. (Zaburi 89: 26-27).
3. ....maana mimi ni baba wa Israeli na Efraim (Ibrahim) ni mzaliwa wa kwanza wangu. (Yeremia 31:9).
Hawa wana wa Mungu wote, kila mmoja wao ni mzaliwa wa kwanza kwa Mungu.
Kwanza inakuwaje watoto wote watatu wawe wazaliwa wa kwanza kwa Mungu. ???
Pili kwa nini hawa wazaliwa wa kwanza wasiitwe miungu?
Na kama hawa watatu wakubwa hawawezi kuwa miungu wala hawaabudiwi, basi mtoto mdogo Yesu pia hana haki yoyote ya kuitwa Mungu wala hana haki ya kuabudiwa.
4. Suleimani ni Mwana wa Mungu. (Mambo ya Nyakati 22:9-10).
5. Wapatanishao wameitwa Wana wa Mungu. (Mathayo 5:9).
Oo! siyo tu bali katika Biblia baadhi ya watu wameitwa miungu.
Tena hakuna Mkristo ambaye anawaita miungu wala hawaabudiwi.
Kama Biblia inavyosema kwamba:
A. Yesu akawajibu, Je! haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, mimi nimesema, ndinyi miungu? (Yohana 10:34).
B. Bwana akamwambia Musa angalia, nimekufanya wewe kuwa kama mungu kwa Farao na huyo ndugu yako Harun atakuwa Nabii wako. (Kutoka 7:1).
Huyo mtoto ni binaadamu kama sisi au kiumbe gani?Yesu na Mungu Ni baba na mtoto
Msingi wa mjadala huu ni kwamba watu humuita Yesu kuwa ni Mungu, sasa hapo ndipo ambapo wewe unajizungusha zungusha yani unataka ibakie kuwa Mungu ni mmoja(Baba) ila mwanae(Yesu) ana uungu kwa sababu ya uwezo wa kuumba ila hautaki kukubali kusema kuwa kuna Miungu wawili.Sijui Nini ambacho huelewi mbona nimeeleza vizuri Sana?
Iko hivi, yesu Ni mwana wa Mungu Kama wewe ulivyo isipokuwa tofauti Ni kwamba yeye aliumbwa kabla yakuzaliwa duniani na kabla ya viumbe vyote mbinguni. Aliumbwa kwa namna ya uwezo wakuumba pia ndio sababu alishiriki pamoja na Mungu kumuumba mwanadamu.
Baada ya anguko la mwanadamu dhambini, Mungu akauliza nimtume Nani? Hakuonekana wakutumwa hivyo yesu ilimuuma Sana kutokana na ushiriki wake ktk uumbaji ndipo alimjibu Mungu nitume mimi.
Mungu akafurahi nakumpa maagizo kwamba lazima utazaliwa Kama binadamu na utaifia dhambi.
Baada ya hapo zawadi zako Ni pamoja na Hawa wanadamu kuwa wako na utawahukumu, pia utakuja kukaa mkono wa kuume kwangu.
Hapo mwanzo kulikuwako neno. Yaani mwanzo wetu sisi Ni neno ambaye Ni yesu.
Naye neno alikuwa kwa Mungu. Yaani huyu neno wakati anatuumba alikuwa kwa Mungu.
Naye neno alikuwa Mungu. Yaani yesu pia alikuwa na uwezo wa kuumba/uwezo wa kimungu.
Vyoote vilifanyika kwa huyo. Yaani huyo yesu alifanya kila kitu Wala pasipo yeye hakikufanyika chochote.
Mimisijizungushi Bali wewe ndio huelewi. Yesu mwenyewe alisemaje kwani?Msingi wa mjadala huu ni kwamba watu humuita Yesu kuwa ni Mungu, sasa hapo ndipo ambapo wewe unajizungusha zungusha yani unataka ibakie kuwa Mungu ni mmoja(Baba) ila mwanae(Yesu) ana uungu kwa sababu ya uwezo wa kuumba ila hautaki kukubali kusema kuwa kuna Miungu wawili.
Sijakuelewa! Unamaanisha Ukraine na Nato + Amerika ni wajinga au........Kwahiyo izo nchi zinawatu wajinga kiasihicho,kwamba wanaweza kugombanishwa kirahisi kama wajinga? nahawajifuzi kilasiku?.
Jiulize mwenyewe, silaha za kupigana ktk nchi hizo zinatoka wapi? Ukipata jibu, nitarudi nikupe za ndani. Maana umasikini wa Afrika unatokana na waafrika kutoelewa michezo ya dunia. Nikikwambia Isis iliundwa na Obama utabisha.Hizi ni baadhi ya nchi zinazo endeshwa kwa misingi ya kikristo na huwezi kuwa kiongozi wa dola ikiwa wewe si mkristo Malta, Armenia, Vatican, England, Denmark, Norway, Iceland nk.
Swali langu ni kwanini huwezi sikia vikundi vya waasi wa kilokole au waasi wa kikatoliki wakiwa msituni wakimpambania mola wao?
Kwanini nchi nyingine kama Syria utasikia sijui wa sunni wameingia msituni kupambana na wasia? Je wanafeli wapi?
Je, nchi zinazo jinasibu zinaongozwa kwa dini ya amani zinawezaje kukosa utulivu miaka nenda rudi?
Kwahiyo wafuasi wa Alkah hawana akili? Wakiona silaha tu wanaanza kupigana? Basi allah atakuwa mpumbavu sana.Jiulize mwenyewe, silaha za kupigana ktk nchi hizo zinatoka wapi? Ukipata jibu, nitarudi nikupe za ndani. Maana umasikini wa Afrika unatokana na waafrika kutoelewa michezo ya dunia. Nikikwambia Isis iliundwa na Obama utabisha.
Ukiisoma biblia vizuri huwezi niuliza swali Hilo,
Labda uwe type ile ya wale waushindani.
Mungu anamwambia farao, mwache Israel mzaliwa wangu wakwanza. Israel Ni yakobo na wakati Mungu anawatoa misri Ni dhahiri yakobo alikuwa marehemu tayari. Je? Ni israel gani anayeongelewa hapo? Israel anayeongelewa hapo ni ile safari ya ukombozi (ukoo) Hadi kufikia kuzaliwa yesu ambaye baada ya kufufuka atakuwa mzaliwa wa kwanza wa waliokufa. Hivyo Basi Mungu anamwambia farao mwache yesu huyo Ni mzaliwa wangu wakwanza usimzuie.
Hivyo hivyo kwa daudi na yeremia maandiko uliotoa hapo juu. Usikariri maandiko, unaposoma jaribu kujua dhima ya ujumbe husika.