Sasa unataka kunipinga Mimi au unapinga maandiko? Wala usichanganyikiwe mtaalam. Mtoto wa Mungu Ni Mungu iko hivyo na ukitaka kujua zaidi Ni kwamba; unajua kwanini tunakufa? Au kwanini tulikatazwa kula tunda? Sababu Ni hiyohiyo ya umungu ndani yetu. Tumeumbwa kwa sifa zote za kimungu.
Biblia inasema kwamba:
1. Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu. (Kutoka 4:22).
2. Daudi ni mwana wa Mungu, yeye pia ni mwana wa kwanza. (Zaburi 89: 26-27).
3. ....maana mimi ni baba wa Israeli na Efraim (Ibrahim) ni mzaliwa wa kwanza wangu. (Yeremia 31:9).
Hawa wana wa Mungu wote, kila mmoja wao ni mzaliwa wa kwanza kwa Mungu.
Kwanza inakuwaje watoto wote watatu wawe wazaliwa wa kwanza kwa Mungu. ???
Pili kwa nini hawa wazaliwa wa kwanza wasiitwe miungu?
Na kama hawa watatu wakubwa hawawezi kuwa miungu wala hawaabudiwi, basi mtoto mdogo Yesu pia hana haki yoyote ya kuitwa Mungu wala hana haki ya kuabudiwa.
4. Suleimani ni Mwana wa Mungu. (Mambo ya Nyakati 22:9-10).
5. Wapatanishao wameitwa Wana wa Mungu. (Mathayo 5:9).
Oo! siyo tu bali katika Biblia baadhi ya watu wameitwa miungu.
Tena hakuna Mkristo ambaye anawaita miungu wala hawaabudiwi.
Kama Biblia inavyosema kwamba:
A. Yesu akawajibu, Je! haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, mimi nimesema, ndinyi miungu? (Yohana 10:34).
B. Bwana akamwambia Musa angalia, nimekufanya wewe kuwa kama mungu kwa Farao na huyo ndugu yako Harun atakuwa Nabii wako. (Kutoka 7:1).