Nchimbi: Kiongozi wa kweli habagui anaowangoza. Huwezi kuwa na vikosi vya upelelezi muda wote unatafuta wenzako wanasema nini

Nchimbi: Kiongozi wa kweli habagui anaowangoza. Huwezi kuwa na vikosi vya upelelezi muda wote unatafuta wenzako wanasema nini

Niwaombe wana CCM wanaoshinda uchaguzi katika ngazi zote, kiongozi wa kweli ni mnyenyekevu na habagui anaowaongoza, waunganishe watu wote waliokuwa chini yako.

Huwezi kuwa wewe una vikosi vya upelelezi muda wote unatafuta wenzako wanasema nini. Binadamu ana haki ya kufikiri, anaweza akayona ya kwako mazuri 100 akayongelea na akayona mabaya ya kwako mawili akayaongelea. Sasa wewe utasikia yale mawili yale 100 hutasikia. Hivi huyu kakkukosea nini kama kakusifia mara moja kakusema vibaya mara mbili? Kuna shida hapo? Hamna shida yoyote n ani haki yake kufikiri siyo? Hajatumi aubongo wako wewe kufikiri katumia ubongo wake, hajatumia nguvu yako yoyote kufikiri.

Kwahiyo niseme, viongozi wa kuchaguliwa katika chama chetu tunaomba wawe wanyenyekevu, na wasiwagawanye watu. Tutawapima viongozi wetu kwa jinsi wanavyounganisha watu na siyo wanavyowagawanya. Maeneo ambayo yamejaa mipasuko ni matokeo ya kuwa na uongozi unaotamani kugawanya watu

Dkt. Nchimbi amezungumza hayo wakati alipokutana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM mkoani Katavi jana, Jumamosi Aprili 13. 2024.

Jambo TV
Hakika Katibu wangu...Kwanza kiongozi anayegawanya watu Hana kujiamini na ana wasiwasi kwakua anajua anapwaya...Kiongozi anayejiamini na anayefanya Kwa weledi hawezi kuwa Kila mara anawaza watu wanasema Nini kwanini na kuweka wambea wakumpelekea maneno maneno yakuokoteza
 
Chongoro alikua vizuri kuliko huyu Nchimbi...

Huyu jamaa hata kuongea hajui...

Nina wasiwasi kama ataweza kumsaidia raisi...

Watu aina ya Nchimbi hua vizuri kwenye mikakati.
Mbona Bashite hajui kuongea na amekuwa kiongozi mkubwa tu??
 
wote hawa wanamwogopa bashite, wanashindwa hata kumtaja au kumwambia mama amwondoe. hii ndio huzuni kubwa kwa taifa hili.
 
Back
Top Bottom