Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Tumeonywa mara nyingi sana na wanasheria kwamba kutokujua sheria , iwe kwa sababu ya elimu yako duni , uzembe wako au labda ujinga wako wa kutokufuatialia sheria na makatazo mbalimbali ya nchi yako hakukufanyi usichukuliwe hatua za kisheria pale unapokosea , ukikutwa na hatia utahukumiwa bila huruma yeyote ile.
Naomba nikiri hadharani kwamba mimi ni mvaa Tai wa siku nyingi na ninazo zaidi ya Tai 50 zenye rangi nyekundu , ambazo nazivaa ninapotaka na tena nazivaa hata kwenye hafla za kitaifa , kiukweli sikuelewa kama natenda kosa , hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza nene !
Naomba sana Wanasheria mliomo humu mkiongozwa na Petro E. Mselewa mnionyeshe andiko lililomo ndani ya Katiba yetu linalokataza kapuku kuvaa Tai nyekundu ili iwe fundisho kwangu na kwa mbumbumbu wenzangu wengine wasiojua chochote ili tuepuke jela ya kizembe.
Natanguliza Shukrani.