Ndani ya Katiba: Tai nyekundu kuwa vazi la Mwenye Mamlaka imeandikwa kwenye ibara gani?

Ndani ya Katiba: Tai nyekundu kuwa vazi la Mwenye Mamlaka imeandikwa kwenye ibara gani?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Tumeonywa mara nyingi sana na wanasheria kwamba kutokujua sheria , iwe kwa sababu ya elimu yako duni , uzembe wako au labda ujinga wako wa kutokufuatialia sheria na makatazo mbalimbali ya nchi yako hakukufanyi usichukuliwe hatua za kisheria pale unapokosea , ukikutwa na hatia utahukumiwa bila huruma yeyote ile.

Naomba nikiri hadharani kwamba mimi ni mvaa Tai wa siku nyingi na ninazo zaidi ya Tai 50 zenye rangi nyekundu , ambazo nazivaa ninapotaka na tena nazivaa hata kwenye hafla za kitaifa , kiukweli sikuelewa kama natenda kosa , hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza nene !

Naomba sana Wanasheria mliomo humu mkiongozwa na Petro E. Mselewa mnionyeshe andiko lililomo ndani ya Katiba yetu linalokataza kapuku kuvaa Tai nyekundu ili iwe fundisho kwangu na kwa mbumbumbu wenzangu wengine wasiojua chochote ili tuepuke jela ya kizembe.

Natanguliza Shukrani.
 
Wala haipo kwenye katiba ila ni fikra za watu walioamua kuzipa maana rangi mbalimbali zilizopo na hivyo nyekundu kupewa tafsiri ya mamlaka kwa kuwa kwa leo kwenye bunge mkuu wa nchi ni Mh Samia basi wengine itabidi wasivae tai za namna hiyo isipokuwa mama ambaye huenda akatupia ushungi mwekundu kuonyesha yeye ndiye mkuu.
 
Kwani wewe umesikia wapi? Au umeona wapi kuwa tai nyekundu ni vazi la mwenye mamlaka? Walifafanua ni mamlaka gani? Hizo tai zako 50 uishawahi kuzuiwa popote usizivae? na nani?
 
Labda Huu mwongozo unapatikana kwenye lile file alilonalo Suwboofer Kule hospitali ya Dodoma ila kwenye katiba ya nchi hatuna kifungu kama hicho.
 
Si hivyo tu hata kusign president anasain na kalam nyekundu.

Ukiuliza reference, sijui
 
Back
Top Bottom