Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Mana anatuteka na maneno mazuri ya kutia faraja na matumaini. Mwendazake Mara atuambie tukae na mavi yetu aisee[emoji23][emoji23]
Hatuna pesa lakini moyo una amani na furaha na ndo kitu kikubwa hicho kwa binadamu...but yule jamaa ilikuwa ukilala unawaza hivi kesho ataamka na lipi jipya nijipange mweeh[emoji848] si kwa mipresha ile ya kizee ingetunyemelea
 
Haya ndiyo mambo makubwa ambayo alifanya Magufuli:

1.Kuondoka duniani wakati hahitajiki.

2.Kuteka wapinzani wake kama akina Azory Gwanda.

3.Kutesa wapinzani wake kwa kuwaweka ndani kila siku.

4.Kuua wapinzani wake na wakosoaji wake kama akina Ben saanane na kuwapiga wapinzani wake risasi kama ilivyokuwa kwa Tindu Lissu.

5.Kuua uhuru wa vyombo vya habari.

6.Kuua uhuru wa kujieleza kwa wananchi kama vile kufungia mitandao ya kijamii kama twitter na kukamata wanaotumia mitandao mingine kumkosoa.

7.Kuiba kura kwa kutumia Polisi,jeshi,TISS pamoja na tume ya uchaguzi.

8.Kuua biashara za watu kupitia sera mbovu za uchumi.

9.Kudanganya katika takwimu za ukuaji wa uchumi wa nchi.

10.Kuweka mihimili yote mitatu mfukoni mwake,yaani mhimili wa urais,bunge na mahakama.

11.Kuua uchumi wa nchi kupitia sheria mbovu za uwekezaji.

12.Kuua watu kwa Corona kupitia leadership negligence.

13.Kuhakikisha kuwa akina Ben Saanane na Azory Gwanda walikipata cha mtema kuni.

14.Ukabila kwa kuhamishia rasilimali nyingi za nchi katika wilaya ya Chato na kujaza wasukuma serikalini.

15 Ukanda kwa kupeleka SGR mwanza wakati siyo economic viable zone.

16.Ubaguzi wa rangi kwa kuwakandia wanawake weusi.Imagine mtu anafanya ubaguzi wa rangi karne ya 21!Is this not insane?

17.Kugandamiza demokrasia kwa kukataza vyama vya upinzani kufanya siasa wakati CCM kufanya siasa ni ruksa.

18.Kunyanyasa malaika-watoto wa kike wasirudi shule wakipata mimba.

19.Ufisadi wa kutisha kwa kufanya miradi mikubwa bila budget kupita bungeni.

20.Wizi wa kutisha wa mali ya uma kupitia kampuni yake ya Mayanga constructions LTD.Mfano uwanja wa Chato umetengenezwa na kampuni hii bila tenda kuitwa.

21.Kubambikizia kesi za kuhujumu uchumi wapinzani wake nchi nzima na kuwatupa korokoroni.

22.Kugushi report ya CAG ya hasara za mabilion za ndege za TTCL na kuilazimisha TTCL watoe gawio fake kwa serekali.

23.Kupora utajiri halali na wa jasho wa matajiri wa Tanzania kwa kuwabambikizia kesi fake za kuhujumu uchumi na kuwalazimisha wakiri makosa ya uwongo kisha kuwafilisi mali zao.
Kuondoka duniani huku haitajiki??[emoji849][emoji849][emoji848][emoji848]
 
Si kweli,magu kafanya mazuri mengi tu,ila mizani inaangukia kwenye mabaya yake,give credit when its due,we stand with Samia period.
Jamaaa kazi alikuwa anapiga hilo halihitaji tochi kujua hili[emoji122][emoji122][emoji122]

Ila...narudia ila...[emoji848][emoji848]
 
Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.
 
Ndani ya siku 18 za Urais wa Samia Suluhu, nchi imejawa na FURAHA, siyo kwamba amepandisha mishahara HAPANA, siyo kwamba ameajiri HAPANA, siyo kwamba anagawa pesa huko mitaani HAPANA
bali ni MATAMSHI yake tu kama Kiongozi Mkuu wa nchi yanaendelea kuliponya taifa bila sindano wala vidonge.

Kwenye utawala uliopita taifa liligawanyika vipande vipande, taifa liliumizwa na hata yeye alijua ndiyo maana ameanza kwa kuliponya taifa kwa maneno yake kabla ya vitendo.

Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.

Mafisadi pia mkae mbali na mama, Wanasiasa vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Viongozi wa dini vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Watendaji wa serikali vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Wajinga wajinga mkae mbali na mama huyu, Waandishi wa habari vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Matapeli wala rushwa mkae mbali na mama huyu

Hatufurahi kupitiliza ila angalau ukikutana watanzia watano, watatu kama sio wanne wanalotabasamu utasikia mama ....oohh mama ni mtu na nusu .

Mungu Mbariki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan
Mungu atubariki Watanzania
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu aliwaonea huruma watu wake akaona huyu jiwe akiendelea hali itakuwa mbaya zaidi ndo maana akaona bora amchukue ili Watanzania wapumue.
Watu walimlilia sana MUNGU nikiwemo na mimi hatimaye yametimia.
Jina la Bwana lihimidiwe.
 
Bainisha sheria kandimizi unazozijua mkuu?
Wamekariri hivyo kila siku katiba mpya katiba mpya sa najiuliza katiba mpya itatoa ajira? Itapandisha mishahara? Kama jibu ni ndio bas tuidai lakini mimi nanavyozijua nchi za kiafrica katiba haimat what matters ni maono ya kiongozi aliyepo madarakani.
 
Mkiamka ndotoni siku moja ndio mtajua hii furaha ya leo ni upepo tu utakaopita, watu wana mihemko sana.

Inashangaza sana kuona watu wanachanganywa akili na maneno tu, nasoma mpaka comment za viongozi wa upinzani naona wanaandika mambo ya kushangaza kabisa, never thought kama tuna wapinzani vichwa vyepesi namna hii.

Hawa wanachotaka ni kuendelea na mambo yao tu, wafanye biashara zao kwa amani baada ya kujichumia kupitia migongo ya "wapiga kura", yaani nasoma comments zote sijaona hata mmoja aliekumbuka Katiba Mpya leo, wote wanashangilia maneno ya mwenyekiti wa CCM, kumbe wanaishi kwa kudra za mwenyekiti wa CCM! ajabu sana.

Niwakumbushe tu, hata Kikwete nae alikuwa na maneno matamu kama haya ya leo. Watanzania tusipoamka badala yake tuendelee kuvitegemea hivi "vyama vya upinzani" tumeliwa.
Kijana fuatilia vzr katiba mbona watu walidhamuuliza alichojibu duh !! Eti tusubir kidogo
 
Alafu hii corona ni kama gonjwa la ki freemason fulani kwa nini wanaokufa ni viongozi tuu wa serikali nawa dini fulani tuu kuwa siri gani hapo.
 
Back
Top Bottom