Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Sheria za magufuli zimekufa na magufuli brother,niambie Samia kavunja sheria ipi ya Nchi hadi sasa? Itakapofikia akakengeuka tutamsema tu,Mungu atupe uhai,ila hadi hapa angalau anatupa matumaini!!
Sheria za Magufuli zimefutwa lini?Unaelewa kuwa sheria gandamizi za Magufuli zilitungwa na bunge na haziwi kufutika ni mpaka zifutwe na bunge?
 
Ndani ya siku 18 za Urais wa Samia Suluhu, nchi imejawa na FURAHA, siyo kwamba amepandisha mishahara HAPANA, siyo kwamba ameajiri HAPANA, siyo kwamba anagawa pesa huko mitaani HAPANA
bali ni MATAMSHI yake tu kama Kiongozi Mkuu wa nchi yanaendelea kuliponya taifa bila sindano wala vidonge.

Kwenye utawala uliopita taifa liligawanyika vipande vipande, taifa liliumizwa na hata yeye alijua ndiyo maana ameanza kwa kuliponya taifa kwa maneno yake kabla ya vitendo.

Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.

Mafisadi pia mkae mbali na mama, Wanasiasa vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Viongozi wa dini vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Watendaji wa serikali vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Wajinga wajinga mkae mbali na mama huyu, Waandishi wa habari vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Matapeli wala rushwa mkae mbali na mama huyu

Hatufurahi kupitiliza ila angalau ukikutana watanzia watano, watatu kama sio wanne wanalotabasamu utasikia mama ....oohh mama ni mtu na nusu .

Mungu Mbariki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan
Mungu atubariki Watanzania
Mungu Ibariki Tanzania.
Faraja itoke wapi? Vifurushi vimepanda wakati wake, mafuta ya kula lita 5 ni elfu 35 leo, mvua imegoma kunyesha tangu awe Rais. Niendelee?
 
Maana yake ni kwamba heri uwe na sheria nzuri ambazo haziheshimiki kuliko kuwa na sheria mbaya ambazo zinafuatwa sana.

Wewe umekula maharage ya wapi??!!

"Ni bora uwe na chakula kizuri usichoweza kula kuliko kuwa na chakula kibaya unachoweza kukila."

Maneno hayo yanaingia akilini???🤣
 
Unamaanisha kuwa nchi iongozwe kwa utashi bila sheria?Are you kidding?Suala la sheria nzuri kutokufuatwa halihalalishi kuwa sheria nzuri hazina maana.
Utayari huo wa kutunga sheria nzuri unaanza na utashi.

Vinginevyo sheria za kulazimishana bila utayati zitakuwa mbovu tu au kukwama kabisa kama ilivyokwama katiba ya Warioba.
 
Wewe umekula maharage ya wapi??!!

"Ni bora uwe na chakula kizuri usichoweza kula kuliko kuwa na chakula kibaya unachoweza kukila."

Maneno hayo yanaingia akilini???🤣
Umeandika kinyume na nilichoandika hapa juu.Nimeandika kuwa ni heri uwe na chakula kizuri ambacho huwezi kula kuliko kuwa na chakula kibaya/chenye sumu ambacho unakila sana.
 
Kweli kabisa.. ccm oyee [emoji16]

I guess mama ni CCM right?
Nyie ndiyo wale wanafiki wachumia tumbo tunaowataka mkae mbali kabisa na MAMA!! Si ndiyo nyie mlitaka fedhuli arefushiwe muda wa kutunyanyasa zaidi? Mungu amewakatalia,kaeni mbali na samia,msijempaka kinyesi chenu bata nyie,ni mwana ccm sawa,hata hivyi ccm si binaadamu flani,hata hiyo ilani ya ccm nyie makapurwa hamjui iliandikwa na nani na kwa malengo gani,mlishangilia watu kuuliwa,watu kufilisiwa,kubambikiwa kesi za ajabu ajabu,kuporwa,nk,Samia amesema wazi kuwa hayo mambo hataki!! Hilo tu linamtofautisha yeye na nyie mbwakoko,kwendeni huko!!!
 
Umeandika kinyume na nilichoandika hapa juu.Nimeandika kuwa ni heri uwe na chakula kizuri ambacho huwezi kula kuliko kuwa na chakula kibaya/chenye sumu ambacho unakila sana.

Huo ni mfano wa ulichoandika .
 
JPM aka Chuma au Jiwe aliwahi sema katika hotuba zake yeye hana maneno matamu au maneno ya kuwabembeleza watanzania subirini baada utawala wangu atakuja wa kuwabembeleza RIP JPM I miss your words and actions
Ni kweli,yule sio tu alikuwa na maneno ya kikatili,bali matendo yake yalidhihirisha hilo, kama kweli atafanikiwa kuwa kiongozi wa malaika basi nawaonea huruma malaika,watapata tabu sana.
 
Unamaanisha kuwa nchi iongozwe kwa utashi bila sheria?Are you kidding?Suala la sheria nzuri kutokufuatwa halihalalishi kuwa sheria nzuri hazina maana.
Je, sheria iliyotungwa inaweza kujisimamia yenyewe ??

Haya wabunge 19 wa chadema wa CHADEMA wako bungeni kinyume na sheria na katiba. Je, suluhisho tutunge sheria mpya tena ???
 
Majirani wanatupenda kwa sababu hawawez kuamisha mipaka (ardhi)
Magufuli hatukuwahi kukubaliana nae kwa lolote alilofanya .
Si kweli,magu kafanya mazuri mengi tu,ila mizani inaangukia kwenye mabaya yake,give credit when its due,we stand with Samia period.
 
Je, sheria iliyotungwa inaweza kujisimamia yenyewe ??

Haya wabunge 19 wa chadema wa CHADEMA wako bungeni kinyume na sheria na katiba. Je, tutunge sheria tena ???
Msimamo wangu ni kwamba kitendo cha sheria nzuri kushindwa kusimamiwa au kushindwa kufuatwa haihalalishi wala haimaanishi kuwa sheria nzuri hazifai.Unaelewa kwanza maana ya hii logic?
 
Taifa limejawa na furaha kwa sababu ni taifa la majuha.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kumsifia Mama au kufikiri kuwa Mama ana nia njema na Tanzania kwa sababu bado anaongoza nchi kwa kutumia zile zile sheria kandamizi za Magufuli.

Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu na ahadi za matumaini.Kuongoza nchi kwa maneno matamu na ahadi za matumaini wakati sheria ni mbovu na kandamizi hilo huwa ni changa la macho.Mama atakuwa na nia njema na Tanzania if and only if atafuta zile sheria kandamizi za Magufuli na kutunga sheria zinazoleta haki,usawa na ukuaji sahihi wa uchumi.
Ndugu ni vema ukapunguza chuki na mihemko binafsi ambayo wala haina maana. Cha kwanza kabisa hua inaanza dhamira na kisha ndo hatua au utekelezaji. Mama tayari amekwisha tuonesha dhamira sasa twasubiri utekelezaji. Kitendo cha kuonesha dhamira pekee haijalishi alikua katika mfumo ama lah! Yeye ndie mwenye mamlaka hivyo atakua chachu ya utekelezaji wa Yale yote ambayo wananchi wake wanayatarajia.

Ni kweli zipo sheria kandamizi ambazo bado hazijafanyiwa mabadiliko na pia wapo watendaji ambao pia kwa namna moja au nyingine ndo walichangia kuvuruga sheria pamoja na mambo mengi lakini ukumbuke hivi vyote haviwezi kubadilika kwa pamoja. Vitabadilika lakini ni kwa awamu.

Awamu ya kwanza mama ameanza kwa kuwapa matumaini wale wote ambao waliathiriwa na utawala wa mzee yule, hatua ya pili ni kubadilisha baadhi ya wizala na mambo mengine kama hayo. Hatua zitakazofuata ni kuwaondoa baadhi ambao hawataonekana kubadilika.

Kwahiyo tumuunge mkono maadam ameonesha nia na pale atakapobadili ile nia ambayo alituahidi awali hapo ndipo tunaweza kuleta mashinikizo mbalimbali ila ukianza tu kusema ooh! Yule hatobadilisha kitu Mara yule ndo walewale CCM utakua haupo sahihi.
 
Ndani ya siku 18 za Urais wa Samia Suluhu, nchi imejawa na FURAHA, siyo kwamba amepandisha mishahara HAPANA, siyo kwamba ameajiri HAPANA, siyo kwamba anagawa pesa huko mitaani HAPANA
bali ni MATAMSHI yake tu kama Kiongozi Mkuu wa nchi yanaendelea kuliponya taifa bila sindano wala vidonge.

Kwenye utawala uliopita taifa liligawanyika vipande vipande, taifa liliumizwa na hata yeye alijua ndiyo maana ameanza kwa kuliponya taifa kwa maneno yake kabla ya vitendo.

Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.

Mafisadi pia mkae mbali na mama, Wanasiasa vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Viongozi wa dini vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Watendaji wa serikali vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Wajinga wajinga mkae mbali na mama huyu, Waandishi wa habari vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Matapeli wala rushwa mkae mbali na mama huyu

Hatufurahi kupitiliza ila angalau ukikutana watanzia watano, watatu kama sio wanne wanalotabasamu utasikia mama ....oohh mama ni mtu na nusu .

Mungu Mbariki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan
Mungu atubariki Watanzania
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu aibariki Tanzania [emoji1241], ampe nguvu rais wetu
 
Back
Top Bottom