Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Taifa limejawa na furaha kwa sababu ni taifa la majuha.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kumsifia Mama au kufikiri kuwa Mama ana nia njema na Tanzania kwa sababu bado anaongoza nchi kwa kutumia zile zile sheria kandamizi za Magufuli.

Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu na ahadi za matumaini.Kuongoza nchi kwa maneno matamu na ahadi za matumaini wakati sheria ni mbovu na kandamizi hilo huwa ni changa la macho.Mama atakuwa na nia njema na Tanzania if and only if atafuta zile sheria kandamizi za Magufuli na kutunga sheria zinazoleta haki,usawa na ukuaji sahihi wa uchumi.
Hebu orodhesha hapa sheria za kipindi cha Magufuli ambazo unadai Kuwa ni kandamizi.
 
Huo ni mwanzo tu, huwezi futa sheria hizo ndani ya siku 18 !!!
Sijasema sheria zifutwe ndani ya siku 18!Mimi namlaumu sana mama na sikubaliani nae kwa maneno yake matamu kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Hilo ndilo ambalo lingetupa matumaini.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu.Hata Hitler aliwapa maneno matamu wananchi wa Ujerumani hadi wakamuamini na kumpa uwaziri mkuu ila alikuja kuwaua kama Kuku!
 
Mkiamka ndotoni siku moja ndio mtajua hii furaha ya leo ni upepo tu utakaopita, watu wana mihemko sana.

Inashangaza sana kuona watu wanachanganywa akili na maneno tu, nasoma mpaka comment za viongozi wa upinzani naona wanaandika mambo ya kushangaza kabisa, never thought kama tuna wapinzani vichwa vyepesi namna hii.

Hawa wanachotaka ni kuendelea na mambo yao tu, wafanye biashara zao kwa amani baada ya kujichumia kupitia migongo ya "wapiga kura", yaani nasoma comments zote sijaona hata mmoja aliekumbuka Katiba Mpya leo, wote wanashangilia maneno ya mwenyekiti wa CCM, yaani kumbe wanaishi kwa kudra za mwenyekiti wa CCM! ajabu sana.

Niwakumbushe tu, hata Kikwete nae alikuwa na maneno matamu kama haya ya leo. Watanzania tusipoamka badala yake tuendelee kuvitegemea hivi "vyama vya upinzani" tumeliwa.
Mkuu mbona umeumia sana? Au ulitaka atoe vitisho kama magu?
 
Hayati alikuwa na maadui wengi,toka amefariki zile story za baadhi ya watu kwamba watu wengi wanakufa kwa corona TZ hakuna tena...hii inaonesha wazi kwamba tatizo halikuwa corona bali hayati.
Corona ipo na inaua. Imemuua mpaka Magu mwenyewe na uongozi wa juu, bado mmekaza kichwa tu.

Akili za mizoga hizi.
 
Utakuja kufa kwa presha wewe ambae unaamini na kufurahia maneno matamu ya Samia wakati mambo yatakuja kuwa ndivyo sivyo kwa sababu yeye anaongoza nchi kwa mujibu wa sheria ambazo ni gandamizi na onevu!Maneno matamu na yanayotia matumaini huwa hayaongozi nchi,kinachoongoza nchi ni sheria.
My friend kwani wewe hupendi maneno matamu. Tena yakitoka kwa jinsia Ke[emoji6][emoji6]
 
Kwahiyo tukasirike from Day Zero kuonesha kuwa huko mbele atapuyanga ??
Tuwe neutral mpaka pale atakapofuta sheria zote gandamizi ambazo alizitunga yeye pamoja na Magufuli kwa sababu nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu na yanayotia matumaini.Maneno matamu na yanayotia matumaini huwa ni mitaji ya wanasiasa katika kuhadhaa watu ili watimize malengo yao.
 
Mkiamka ndotoni siku moja ndio mtajua hii furaha ya leo ni upepo tu utakaopita, watu wana mihemko sana.

Inashangaza sana kuona watu wanachanganywa akili na maneno tu, nasoma mpaka comment za viongozi wa upinzani naona wanaandika mambo ya kushangaza kabisa, never thought kama tuna wapinzani vichwa vyepesi namna hii.

Hawa wanachotaka ni kuendelea na mambo yao tu, wafanye biashara zao kwa amani baada ya kujichumia kupitia migongo ya "wapiga kura", yaani nasoma comments zote sijaona hata mmoja aliekumbuka Katiba Mpya leo, wote wanashangilia maneno ya mwenyekiti wa CCM, yaani kumbe wanaishi kwa kudra za mwenyekiti wa CCM! ajabu sana.

Niwakumbushe tu, hata Kikwete nae alikuwa na maneno matamu kama haya ya leo. Watanzania tusipoamka badala yake tuendelee kuvitegemea hivi "vyama vya upinzani" tumeliwa.
Mkuu, tukasajiri Chama chetu tuingie mzigoni
 
Sijasema sheria zifutwe ndani ya siku 18!Mimi namlaumu sana mama na sikubaliani nae kwa maneno yake matamu kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Hilo ndilo ambalo lingetupa matumaini.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu.Hata Hitler aliwapa maneno matamu wananchi wa Ujerumani hadi wakamuamini na kumpa uwaziri mkuu ila alikuja kuwaua kama Kuku!

Je, hakuna tofauti ya kiuongozi kati ya Mwendazake na Mama??
 
Kwa hyo ulitaka hayo yote ayafanye ndani ya siku 18?
Sijamaanisha kuwa hayo yote afanye ndani ya siku 18.Mimi namlaumu sana Mama na sikubaliani nae kwa maneno yake matamu kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Hilo ndilo ambalo lingetupa matumaini.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu ili watimize malengo yao ovu.Hata Hitler aliwapa maneno matamu wananchi wa Ujerumani hadi wakamuamini na kumpa uwaziri mkuu kisha akaanza kuwaua kama Kuku.
 
Tuwe neutral mpaka pale atakapofuta sheria zote gandamizi ambazo alizitunga yeye pamoja na Magufuli kwa sababu nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu na yanayotia matumaini.Maneno matamu na yanayotia matumaini huwa ni mitaji ya wanasiasa katika kuhadhaa watu ili watimize malengo yao.
Anyway:

1- Wananchi tuna mahitaji yetu na

2- Wanasiasa pia wana mahitaji yao.

Ultimate goal ya mwanasiasa ni siku akipewa madaraka, halafu na yeye atatumia sheria hizo hizo kuumiza watu

Na sisi wananchi tunahitaji tu, ubora wa maisha yetu. Maana hakuna mwanasiasa anahangaika kupata kula.
 
We nawe unachosha bwana
Huna jema.
Mama Samia ndiye hana jema kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye mwenyewe pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu ili watimize malengo yao ovu.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kushobokea maneno matamu ya wanasiasa.
 
Anyway:

1- Wananchi tuna mahitaji yetu na

2- Wanasiasa pia wana mahitaji yao.

Ultimate goal ya mwanasiasa ni siku akipewa madaraka, halafu na yeye atatumia sheria hizo hizo kuumiza watu

Na sisi wananchi tunahitaji tu, ubora wa maisha yetu. Maana hakuna mwanasiasa anahangaika kupata kula.
Wewe mwananchi huwezi kuwa na maisha bora kama unaongozwa kwa sheria ambazo hazina nia ya kukupatia muongozo sahihi katika kujitafutia maisha bora.
 
Je, hakuna tofauti ya kiuongozi kati ya Mwendazake na Mama??
Kumpima Mama ndani ya wiki hizi mbili siyo sahihi kwa sababu hata Magufuli,Hitler,Mussolin na kadhalika ndani ya wiki mbili za mwanzo walianza vizuri sana.Magufuli ndani ya wiki mbili za uongozi wake alikuwa ni role model leader huko Ulaya,Marekani,South Afrika na kadhalika ila baadae alikuja kuwa kituko kinachovutia hadi utalii!
 
Hebu orodhesha hapa sheria za kipindi cha Magufuli ambazo unadai Kuwa ni kandamizi.
1.Sheria ya Mitandao ya mwaka 2015.

2.Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na ya Posta (Maudhui ya Mtandaoni) zilizopitishwa mwaka 2018 zinamtaka kila anaemiliki blogu au tovuti kulipa ada ya leseni hadi shilingi za kitanzania milioni 2.1 (zaidi ya Dola za Marekani 900). Sheria hii pia inadhibiti maudhui ya mtandaoni na kuruhusu uchunguzi wa mitandao bila usimamizi wa mahakama.

3.Serikali ya Tanzania pia inadhibiti utafiti binafsi na upatikanaji wa taarifa za takwimu kwa umma kupitia sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, ambayo inawanyima wananchi vyanzo mbadala vya taarifa huru zilizothibitishwa. Wakati marekebisho ya sheria hii yaliyoletwa mwaka 2019 yameondoa dhima ya jinai kwa kuchapisha takwimu zisizo rasmi, mamlaka bado inadhibiti nani anayeweza kukusanya na kusambaza taarifa za takwimu na kuamua kipi ni sahihi au sio sahihi.

4.Januari 2019, Bunge lilifanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na kuweka vikwazo vingi zaidi vya haki ya uhuru wa kushiriki na kukusanyika kwa amani. Marekebisho haya yalimpa Msajili wa Vyama vya Siasa nguvu ya kufuta vyama vya siasa, kuitisha taarifa kutoka vyama vya siasa na kusimamisha wanachama. Pia ilianzisha hitaji la mashirika na watu binafsi kupata kibali kabla ya kutoa elimu ya uraia, jambo ambalo linazuia haki ya mwananchi kupata taarifa.
 
Ndani ya siku 18 za Urais wa Samia Suluhu, nchi imejawa na FURAHA, siyo kwamba amepandisha mishahara HAPANA.
siyo kwamba ameajiri HAPANA
siyo kwamba anagawa pesa huko mitaani HAPANA
bali ni MATAMSHI yake tu kama Kiongozi Mkuu wa nchi yanaendelea kuliponya taifa bila sindano wala vidonge, kwenye utawala uliopita taifa liligawanyika vipande vipande, taifa liliumizwa na hata yeye alijua ndiyo maana ameanza kwa kuliponya taifa kwa maneno yake kabla ya vitendo.

Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.

Mafisadi pia mkae mbali na mama
Wanasiasa vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Viongozi wa dini vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Watendaji wa serikali vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Wajinga wajinga mkae mbali na mama huyu.
Waandishi wa habari vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Matapeli wala rushwa mkae mbali na mama huyu

Hatufurahi kupitiliza ila angalau ukikutana watanzia watano, watatu kama sio wanne wanalotabasamu utasikia mama ....oohh mama ni mtu na nusu .

Mungu Mbariki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan
Mungu atubariki Watanzania
Mungu Ibariki Tanzania.
Utu vs vitu.
 
Back
Top Bottom