Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Huwezi kamwe kufanya kazi katika nchi ambayo ina sheria mbovu ndiyo maana hata wafanyabiashara wakubwa wamekimbia nchi kama Mama alivyokuwa anadai jana.Yote haya yamesababishwa na sheria mbovu alizotunga Magufuli.Huwezi kufanya kazi ukawa productive kama huna amani na furaha.Huwezi kufanya kazi kama muda wote unawaza kwenda kufungwa kwa makosa ambayo hujatenda.Kwenye hii nchi kuna watu wengi sana wamebambikiziwa kesi za kuhujumu uchumi wakati hawajawahi kutenda kosa hilo kisa tu Serekali ikusanye mapato ambayo ni haramu na ambayo ni unsustainable.Kwenye nchi yenye mambo kama hayo huwezi kufanya kazi ukawa productive.Dikteta anaehimiza watu kufanya kazi wakati sheria ni mbovu ni dikteta aliechanganyikiwa!
 
That's very good...

Sasa kumbuka Mama Samia kasisitiza juu ya kurejesha mahusiano mazuri ya kimataifa na kisha ku - encourage foreign investments..

Hii nia na kisha kuzaa maelekezo na maagizo haya ya Rais kwa wasaidizi ni ishu mtambuka.

Huwezi kuvutia wawekezaji bila kutazama mambo ya kisheria, kisera na ikibidi katiba..

Tukumbuke kuwa sheria hizi zote ulizoziorodhesha hapa zimelalamikiwa hata na nchi washirika wetu wa maendeleo ambako ndiko kunakotoka hawa investors tunaotaka waje kuwekeza hapa nchini...

For sure, kama nia ya Rais ni thabiti ktk haya anayoagiza na ili yatekelezeke kwa kasi, basi ni sharti kufanyike marekebisho makubwa ya kisheria, kisera na kimfumo wa usimamizi na uendeshaji wa mambo yetu kama nchi...

Hebu tumpe mama Samia Suluhu a benefit of doubt katika huko anakotaka kutupeleka na Mungu amsaidie kusimamia kusudi lake...
 
Ni akili tu wala si nguvu kama alivyofanya bwana yule.
 
Sasa utajua kuwa Afrika ni kichwa cha wendawazimu pale ambapo Mama atataka kuvutia wawekezaji bila kutazama mambo ya sheria kandamizi,sera na katiba!
 
Neno linaweza kuwa lilelile lkn likawa tusi kwako na kwangu likanipa faraja itategemea mwongeaji alikuwa katka hali gani.
 
Neno linaweza kuwa lilelile lkn likawa tusi kwako na kwangu likanipa faraja itategemea mwongeaji alikuwa katka hali gani.
Suala la viongozi wetu kutoa uongozi bora na kuongoza kwa mujibu wa sheria ni haki yetu sisi wananchi kikatiba.Kwa kuwa ni haki yetu hawapaswi kutoa ahadi tamu za kutupa haki hiyo kwa sababu ni wajibu wao kikatiba kutupa haki hiyo.Wewe ulishawahi kumuahidi mtoto wako mdogo kwa maneno matamu kuwa akiugua utampeleka hospitali?Jibu ni hapana!Hujawahi kufanya hivyo kwa sababu unajua ni jukumu lako kisheria kufanya hivyo na pia mtoto wako hajawahi kutarajia ahadi kama hizo kutoka kwako kwa kuwa anajua ni haki yake akiugua apelekwe hospitali na mzazi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…