Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Nchi inaendeshwa na katiba. Lipa Kodi. Fanya Kazi. Hutapata Shida wala hutataka hata sababu ya kujua Rais kaamkaje. Mengine Ni ushabiki maandazi na kukosa Kazi.

Umepatia tu pale maneno matamu hayajengi nchi. Watanzania walishasikia maneno Bora na matamu toka lwa nyerere. Sasa Ni Kazi tu. Watanzania wengi wenye maneno kila siku mko mtandaoni, Sijui bundle mnatoa wapi. Amkeni fanyeni kazi. Ukiona barabara mbovu nk. Afya ndo unaweza kukumbuka na kuuliza Hivi Nani mkurugenzi. Nani mkuu wa Wilaya nk. Otherwise nobody cares so long as tuna Amani binafsi na majambazi hawana pa kukimbilia. Ndo mana i will always be proud of having a president by the name of JPM. Police wanafanya Kazi Lakini huwa wanaangalia kama Kiongozi wa juu Yuko serious ama legelege.

Unajua Kwanini mnasifia sana Sasa, Ni kwa kuwa bado mnataka JPM azungumziwe. All the best my Madam President Lead us.
Huwezi kamwe kufanya kazi katika nchi ambayo ina sheria mbovu ndiyo maana hata wafanyabiashara wakubwa wamekimbia nchi kama Mama alivyokuwa anadai jana.Yote haya yamesababishwa na sheria mbovu alizotunga Magufuli.Huwezi kufanya kazi ukawa productive kama huna amani na furaha.Huwezi kufanya kazi kama muda wote unawaza kwenda kufungwa kwa makosa ambayo hujatenda.Kwenye hii nchi kuna watu wengi sana wamebambikiziwa kesi za kuhujumu uchumi wakati hawajawahi kutenda kosa hilo kisa tu Serekali ikusanye mapato ambayo ni haramu na ambayo ni unsustainable.Kwenye nchi yenye mambo kama hayo huwezi kufanya kazi ukawa productive.Dikteta anaehimiza watu kufanya kazi wakati sheria ni mbovu ni dikteta aliechanganyikiwa!
 
1.Sheria ya Mitandao ya mwaka 2015.

2.Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na ya Posta (Maudhui ya Mtandaoni) zilizopitishwa mwaka 2018 zinamtaka kila anaemiliki blogu au tovuti kulipa ada ya leseni hadi shilingi za kitanzania milioni 2.1 (zaidi ya Dola za Marekani 900). Sheria hii pia inadhibiti maudhui ya mtandaoni na kuruhusu uchunguzi wa mitandao bila usimamizi wa mahakama.

3.Serikali ya Tanzania pia inadhibiti utafiti binafsi na upatikanaji wa taarifa za takwimu kwa umma kupitia sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, ambayo inawanyima wananchi vyanzo mbadala vya taarifa huru zilizothibitishwa. Wakati marekebisho ya sheria hii yaliyoletwa mwaka 2019 yameondoa dhima ya jinai kwa kuchapisha takwimu zisizo rasmi, mamlaka bado inadhibiti nani anayeweza kukusanya na kusambaza taarifa za takwimu na kuamua kipi ni sahihi au sio sahihi.

4.Januari 2019, Bunge lilifanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na kuweka vikwazo vingi zaidi vya haki ya uhuru wa kushiriki na kukusanyika kwa amani. Marekebisho haya yalimpa Msajili wa Vyama vya Siasa nguvu ya kufuta vyama vya siasa, kuitisha taarifa kutoka vyama vya siasa na kusimamisha wanachama. Pia ilianzisha hitaji la mashirika na watu binafsi kupata kibali kabla ya kutoa elimu ya uraia, jambo ambalo linazuia haki ya mwananchi kupata taarifa.
That's very good...

Sasa kumbuka Mama Samia kasisitiza juu ya kurejesha mahusiano mazuri ya kimataifa na kisha ku - encourage foreign investments..

Hii nia na kisha kuzaa maelekezo na maagizo haya ya Rais kwa wasaidizi ni ishu mtambuka.

Huwezi kuvutia wawekezaji bila kutazama mambo ya kisheria, kisera na ikibidi katiba..

Tukumbuke kuwa sheria hizi zote ulizoziorodhesha hapa zimelalamikiwa hata na nchi washirika wetu wa maendeleo ambako ndiko kunakotoka hawa investors tunaotaka waje kuwekeza hapa nchini...

For sure, kama nia ya Rais ni thabiti ktk haya anayoagiza na ili yatekelezeke kwa kasi, basi ni sharti kufanyike marekebisho makubwa ya kisheria, kisera na kimfumo wa usimamizi na uendeshaji wa mambo yetu kama nchi...

Hebu tumpe mama Samia Suluhu a benefit of doubt katika huko anakotaka kutupeleka na Mungu amsaidie kusimamia kusudi lake...
 
Ndani ya siku 18 za Urais wa Samia Suluhu, nchi imejawa na FURAHA, siyo kwamba amepandisha mishahara HAPANA, siyo kwamba ameajiri HAPANA, siyo kwamba anagawa pesa huko mitaani HAPANA
bali ni MATAMSHI yake tu kama Kiongozi Mkuu wa nchi yanaendelea kuliponya taifa bila sindano wala vidonge.

Kwenye utawala uliopita taifa liligawanyika vipande vipande, taifa liliumizwa na hata yeye alijua ndiyo maana ameanza kwa kuliponya taifa kwa maneno yake kabla ya vitendo.

Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.

Mafisadi pia mkae mbali na mama, Wanasiasa vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Viongozi wa dini vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Watendaji wa serikali vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Wajinga wajinga mkae mbali na mama huyu, Waandishi wa habari vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Matapeli wala rushwa mkae mbali na mama huyu

Hatufurahi kupitiliza ila angalau ukikutana watanzia watano, watatu kama sio wanne wanalotabasamu utasikia mama ....oohh mama ni mtu na nusu .

Mungu Mbariki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan
Mungu atubariki Watanzania
Mungu Ibariki Tanzania.
Ni akili tu wala si nguvu kama alivyofanya bwana yule.
 
That's very good...

Sasa kumbuka Mama Samia kasisitiza juu ya kurejesha mahusiano mazuri ya kimataifa na kisha ku - encourage foreign investments..

Hii nia na kisha kuzaa maelekezo na maagizo haya ya Rais kwa wasaidizi ni ishu mtambuka.

Huwezi kuvutia wawekezaji bila kutazama mambo ya kisheria, kisera na ikibidi katiba..

Tukumbuke kuwa sheria hizi zote ulizoziorodhesha hapa zimelalamikiwa hata na nchi washirika wetu wa maendeleo ambako ndiko kunakotoka hawa investors tunaotaka waje kuwekeza hapa nchini...

For sure, kama nia ya Rais ni thabiti ktk haya anayoagiza na ili yatekelezeke kwa kasi, basi ni sharti kufanyike marekebisho makubwa ya kisheria, kisera na kimfumo wa usimamizi na uendeshaji wa mambo yetu kama nchi...

Hebu tumpe mama Samia Suluhu a benefit of doubt katika huko anakotaka kutupeleka na Mungu amsaidie kusimamia kusudi lake...
Sasa utajua kuwa Afrika ni kichwa cha wendawazimu pale ambapo Mama atataka kuvutia wawekezaji bila kutazama mambo ya sheria kandamizi,sera na katiba!
 
Taifa limejawa na furaha kwa sababu ni taifa la majuha.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kumsifia Mama au kufikiri kuwa Mama ana nia njema na Tanzania kwa sababu bado anaongoza nchi kwa kutumia zile zile sheria kandamizi za Magufuli.

Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu na ahadi za matumaini.Kuongoza nchi kwa maneno matamu na ahadi za matumaini wakati sheria ni mbovu na kandamizi hilo huwa ni changa la macho.Mama atakuwa na nia njema na Tanzania if and only if atafuta zile sheria kandamizi za Magufuli na kutunga sheria zinazoleta haki,usawa na ukuaji sahihi wa uchumi.
Neno linaweza kuwa lilelile lkn likawa tusi kwako na kwangu likanipa faraja itategemea mwongeaji alikuwa katka hali gani.
 
Neno linaweza kuwa lilelile lkn likawa tusi kwako na kwangu likanipa faraja itategemea mwongeaji alikuwa katka hali gani.
Suala la viongozi wetu kutoa uongozi bora na kuongoza kwa mujibu wa sheria ni haki yetu sisi wananchi kikatiba.Kwa kuwa ni haki yetu hawapaswi kutoa ahadi tamu za kutupa haki hiyo kwa sababu ni wajibu wao kikatiba kutupa haki hiyo.Wewe ulishawahi kumuahidi mtoto wako mdogo kwa maneno matamu kuwa akiugua utampeleka hospitali?Jibu ni hapana!Hujawahi kufanya hivyo kwa sababu unajua ni jukumu lako kisheria kufanya hivyo na pia mtoto wako hajawahi kutarajia ahadi kama hizo kutoka kwako kwa kuwa anajua ni haki yake akiugua apelekwe hospitali na mzazi wake.
 
Back
Top Bottom