Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 242 yaanguka huko Ahmedabad, India muda mfupi baada ya kupaa. 241 wathibitika kufariki dunia

Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 242 yaanguka huko Ahmedabad, India muda mfupi baada ya kupaa. 241 wathibitika kufariki dunia

Kwa kishindo hicho kutegemea angetoka mtu hai ni uwongo.

Hapo ndipo maskini tunapojifariji kumbe kupanda kwetu buses ni afadhali maana yenyewe yakipiga buyu angalao mbabaki wawili watatu mnapumua ndege habaki mtu chap mnaingia ng’ambo ya pili kwa aliyewaumba tena mkiwa idadi sawa na mlivyopanda.
Kifo ni kifo tu
 
Habari kuhusu abiria si nzuri, abiria wote wamefariki.

RIP
إنا لله وإنا إليه راجعون kiukweli ajali ya ndege kutoboa huwa ngumu sana, unakufa kwa presha kabla ya ajali yenyewe, kuna siku kushuka pale JNIA hali ya hewa ilikuwa mbaya sana, rubani alipambana sana mpaka kutua moyo unataka kutokea sikioni.
 
Sio kwamba mwamba aliyekuwa kakaa seat 11A kapona?
Abria Vishwash Kumar Ramesh (40) raia wa Uingereza, aliyekuwa ameketi kwenye siti namba 11A, amenusurika katika ajali ya ndege ya Air India iliyokuwa ikielekea London na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 200.

Shirika la ndege la Air India limesema kwenye ndege hiyo kulikuwa na abiria 169 raia wa India, 53 raia wa Uingereza, raia 7 wa Ureno, na mmoja kutoka Canada.
1749746766116.jpg
 
Hakuna kitu naogopa kama ndege ikiwa inapaa na kushuka huwa natubu kabisa na kutoa shahada sijawahi uzoea huo usafiri.Wapumzike kwa Amani.
Kupaa kabla haijakaa level inatisha kwa kweli. Angalau zile alert za kufungua mikanda zikilia kidogo unapumua.

Incident nyingine ya kuogofya kuna wakati ghafla mnakuwa kama mnadondoka (weightless) halafu inakaa sawa! Dah!
 
Nyakati mbili za hatari sana kwenye ndege ni wakati wa kupaa na wakati wa kutua
 
Kupaa kabla haijakaa level inatisha kwa kweli. Angalau zile alert za kufungua mikanda zikilia kidogo unapumua.

Incident nyingine ya kuogofya kuna wakati ghafla mnakuwa kama mnadondoka (weightless) halafu inakaa sawa! Dah!
Hapana kwa kweli huu usafiri ni wa ajabu kweli kwanza masikio yanavuta mara ujihisi miguu juu kichwa kipo chini kwa kweli haiwezi kudondoka mkapona.
 
Back
Top Bottom