Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Fokker Wulf walitengeneza ndege za Luftwaffe, jeshi la anga la Nazi Germany. Ilikuwa kampuni kubwa ila ikapotea na sasa iko kwenye consortium ya Airbus
 
Nawaza huyp dogo amejuaje kama engine moja imezima? While haoni dashboard? Nitoeni ushamba hapo
 
Elimu tu mtu wangu, ndege nyingi tu kama sio zote zinatengenezwa na uwezo wa kukamilisha kazi hata ikibaki na injini moja tu.

Ningekuwa kwenye hiyo ndege abiria wenzangu wangeniona chizi kwa kutoonesha hata lepe la paniki, na kuwashangaa wanaopaniki hata baada ya rubani kutoa maelezo kamili kabisa!

Hint: sijawahi kupanda ndege🤣😂😂😂
 
yeah kwa sababu midege hii ina power backup nyingi. kama ni engine moja tu imekufa yeah anaweza kwenda kwa muda huo. haya yana migenerator ya kuzalisha umeme kusaida kuendesha ndege, lakini pia ya batteries kama generator pia zitazingua
 
Tungesema tuwahi Kuwakagua 'Kibaiolojia' hao Abiria Wote waliokuwa na Hofu kutokana na Hitilafu hiyo ni kwamba 99.9999% yao lazima tu walikuwa wameshajisaidia Small and Big Haja kwa pamoja.
 
Napata shida kuelewa juu ya kuzima kwa engine moja na ndege na kuendelea na safari. Ndege za Precision Air hazina engine tatu; zote zina engine mbili, kila bawa imefungwa engine moja. Kuruka na kupaa kwa ndege hizi za engine mbili, ni lazima engine zote mbili zifanye kazi. Ikitokea engine moja ikazima, ndege hiyo haiwezi kuendelea na mwendo katika uelekeo wake, kwani engine moja inayofanya kazi itavuta upande mmoja na kupoteza direction. Nadhani kulikuwa na hitilafu tu ya engine, lakini sio engine kuzima. Kama ingekuwa na engine tatu; engine hii ya tatu ambayo haitegemeani na nyingine (unpaired), hata ikizima, ndege inaweza kwenda in the same direction, labda speed ndio itapungua, kwakuwa the turning torque is balanced.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…