Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Inawezekana huyu dogo wa kutoka ubeberuni asingewaambia abiria wa kibongo kuwa injini moja imezima rubani angeforce kulifikisha dude Dar
You nailed it , air crash investigation kuna scenario nyingi sana zinasikitisha , na kuna mchango mkubwa kwa abiria kwa pilots just incase .
Kuna moja jamaa walipata engine fire kwenye engine , namba mbili , kwa kuwa bado ilikuwa inafanya kazi , pilot aamkua kuzima engine ili moto usiendelee , badala ya kuzima ile yenye kukolea moto akazima hii nzima namba moja , dude likashuka mazima .
 
yeah kwa sababu midege hii ina power backup nyingi. kama ni engine moja tu imekufa yeah anaweza kwenda kwa muda huo. haya yana migenerator ya kuzalisha umeme kusaida kuendesha ndege, lakini pia ya batteries kama generator pia zitazingua
Aisee!
 
Napata shida kuelewa juu ya kuzima kwa engine moja na ndege na kuendelea na safari. Ndege za Precision Air hazina engine tatu; zote zina engine mbili, kila bawa imefungwa engine moja. Kuruka na kupaa kwa ndege hizi za engine mbili, ni lazima engine zote mbili zifanye kazi. Ikitokea engine moja ikazima, ndege hiyo haiwezi kuendelea na mwendo katika uelekeo wake, kwani engine moja inayofanya kazi itavuta upande mmoja na kupoteza direction. Nadhani kulikuwa na hitilafu tu ya engine, lakini sio engine kuzima. Kama ingekuwa na engine tatu; engine hii ya tatu ambayo haitegemeani na nyingine (unpaired), hata ikizima, ndege inaweza kwenda in the same direction, labda speed ndio itapungua, kwakuwa the turning torque is balanced.
Usikariri.
 
Ningekuwepo humo ndegeni ningevaa zangu earphone sauti hadi mwisho kabsa. Ningeweka nyimbo ya rose muhando _Nakaza mwenendo nifike mbinguni.
Ningefanya hivyo kwa sababu hata ningepiga makelele ingebadikisha chochote??
Njoo uone reaction ya nduguyo Extrovert
 
Hizi ndege ndogo nakumbuka niliwahi kukaa pale mbele na pilot, tulikua tunatokea Pemba, ndege ilikua imekwisha kabisa mafuta na ilikua inapiga alarm tukaruka mpaka unguja, hakujaza mafuta, tukaenda nayo mpaka uwanja wa Dar.

Siku hiyo ilikua tete maana jamaa alikua mbishi mno yeye alikua analazimisha kufika dar ndio ajaze mafuta.

Jinga sana yule jamaa.
Kifupi alikuwa anatembelea choki 😁😁😁
 
Hizi ndege ndogo nakumbuka niliwahi kukaa pale mbele na pilot, tulikua tunatokea Pemba, ndege ilikua imekwisha kabisa mafuta na ilikua inapiga alarm tukaruka mpaka unguja, hakujaza mafuta, tukaenda nayo mpaka uwanja wa Dar.

Siku hiyo ilikua tete maana jamaa alikua mbishi mno yeye alikua analazimisha kufika dar ndio ajaze mafuta.

Jinga sana yule jamaa.
Hivi mkondo wa Nungwi unavyoyumbishaga ndege mlipoufikia si karibu ujiharishie kwa hofu?🤣
 
Ndege ya engine mbili ikizima engine moja huwa haina shida kabisa, huwa zinatua uwanja ulio karibu ili kuepuka endapo engine iliyobakia inaweza kuzima pia. Ila ndege inaweza kuruka na engine moja na ikatua salama kabisa
Hakuna rubani anaweza kubali ruka na engine 1
Hiyo ikukute tu angani ndo waweza angalia karibu wapi, na ikitokea ikafail ndo yale ya Captain Sully, tafuta maji au mlipuke
 
yeah kwa sababu midege hii ina power backup nyingi. kama ni engine moja tu imekufa yeah anaweza kwenda kwa muda huo. haya yana migenerator ya kuzalisha umeme kusaida kuendesha ndege, lakini pia ya batteries kama generator pia zitazingua
Ila pia huwa haishauriwi kufanya hivyo, maana engine failure moja inaweza sababisha zote zikazima, kwani moja yaweza zidiwa
 
View attachment 2306678
Abiria ndani ya ndege ya Kampuni ya Precision, jana waliingiwa na hofu ya usalama wao baada ya injini moja kuzima ikiwa angani.

Ndege hiyo yenye namba PW 467 ikitokea Kahama, ikielekea Dar es Salaam kupitia Mwanza, ilizima injini baada ya dakika 51 kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza.

Hofu ilianza kutokea baada ya abiria mmoja, kijana wa kizungu, kuanza kupiga kelele, akiwaeleza wenzake waliokuwa wameketi jirani, kwamba injini imezima.

Baadaye abiria wengine waliingiwa hofu, huku baadhi wakisali, wakilia na wengine kuonekana wamejiinamia, huku wamefunika nyuso zao.

Baada ya abiria kuonekana 'wakipaniki' ndipo rubani wa ndege hiyo alitangaza kuwepo kwa hitilafu hiyo huku akieleza kwamba hali siyo ya kutisha sana.

"Abiria wetu wapenzi, ndege yetu imepata tatizo la kiufundi, injini moja imezima, lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani, tunapanga kutua katika kiwanja jirani na hapa tulipo," alisema rubani huyo.

Hata hivyo, tulizo la mwana anga huyo halikuleta afueni ya wasiwasi kwa abiria wengi, waliendelea na hofu yao, huku wengine waliokuwa hawajatambua kinachoendelea wakiungana na wengine kusononeka.

Rubani alirejea tena kwa tangazo; "Abiria wetu wapendwa, tunasikitika kwa kilichotokea, nawaomba kuwa watulivu wakati sasa tunajiandaa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Tutatua ndani ya dakika 20."

Baada ya muda huo, ndege hiyo ilitua salama katika uwanja huo na abiria walishangilia. Wengine walipiga kofi, wengine wakipiga kelele za shangwe na wengine wakimshukuru Mungu.

Mmoja wa abiria aliyekuwamo ndani ya ndege hiyo, Simon Mkina, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter na taarifa hiyo kusambaa dunia nzima, huku akipongezwa kwa kutoa taarifa hiyo mapema.
Ngozi nyeusi wala hazikuwa zinajua bout engine shut off .hakuna kitu wanajua
 
Back
Top Bottom