Ndege ya watalii yapokelewa Uwanja wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)

Ndege ya watalii yapokelewa Uwanja wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)

Du ukisikia kufilisika ndiyo huku. Awamu zote watalii wanakuja lakini awamu hii kuja kwa watalii imekuwa ni habari kubwa kabisa. Ukweli ni kwamba itachukuwa muda mrefu ili hali irudie kama zamani. Nchi kama Thailand zinazoongoza kwa utalii mpaka sasa hali siyo nzuri halafu waje huku ambako takwimu zinafichwa? Watalii 200 ni wachache sana na itachukuwa muda hali ya zamani kurudi.
Nchi iliyokua inategemea watalii milioni 2 leo inashangilia watalii mia 2, aisee.
Huu ni mwanzo lazima furaha iwepo,mlitaka wasije kabisa,bora hao 200 kuliko kukosa kabisa,uchawi sio mpaka mtu abebe tunguli,jitazameni kauli zetu

Endeleeni kusubiri taifa hili lifeli,mtasubiri sana.
 
Halafu unakuta mtu anaanzisha thread sijui tujitoe WB or mabeberu wasitupangie embu cheki hiyo desperation ya kupata watalii ndio ujue hazina hali sio nzuri.

Ni jambo jema uchumi urudi kwenye hali ya kawaida as soon as possible serikali ipate mapato yake na biashara zifaidike, but this is just a show of desperation to the world.

Unapoona nchi kama Venezuela inaagiza mafuta yaliyosafishwa na mtu pekee mwenye jeuri kumpelekea duniani has got nothing more to loose ndio ujue kumvaa beberu uwe umedhamiria kweli kupigika ki uchumi.

Kama atuwezi vumilia hata miezi mitatu ya mtikisiko wa kiuchumi tutaweza sanctions kweli watanzania wanao zililia kila siku.
Tuwekewe sanctions tumefanya nini?
 
Kweli TBC ni tv ya propaganda mbona ndege yenyewe imeshusha watu 6 ?
Hao wengine watakuwa maeshukia vituo vya nyuma huko. Ilikuwa inashusha kama Daladala...KIA wapooo...Shushaaa..Andaa nauli kabisa...Ngorongoro unashusha.....Poa bi mkubwa andaa mzigo kama ni chenji niandae kabisa. Nasikia mmoja kachenjiana na konda katoa buku 10 konda hana chenji wakati ndo biashara inaanza. Alikuwa anashukia BURIGI Chato!


MATAGA mtakufa kwa kihoro. Narudia tena kama mnategemea utalii na hii ficha ficha yenu ukweli basi mmeshafeli mapema kabisaaa. Msije kusema sijawaambia. Usanii wenu utabaki huko huko bongo.

Nyambaf!
 
Kwa mustakabali na maslai mapana ya Taifa letu John Pombe Joseph Magufuli, haifai kupewa hata dakika moja, au nafasi nyingine ya kuongoza taifa letu, ametutia aibu Sana , ameturudisha nyuma Kama taifa kwa miaka zaida ya 10, hasara aliyotupa wajukuu zetu hawataweza kulipa
Lakini vitu vingine kama Miundombinu imeboreka sana hadi Ubungo junction tumepata Flyover kuchelewa kazini ndo basi tutawahi kwenda mjini
 
Tuwekewe sanctions tumefanya nini?
Siwezi kubishana utoto kama timamu ungeona mantiki ya post ni umuhimu wa kuonyesha resilience ata wakati unapitia kipindi kigumu.

Haya ebu nielezee ulivyo tafsiri wewe hiyo aya mwisho inasemaje?
 
Siwezi kubishana utoto kama timamu ungeona mantiki ya post ni umuhimu wa kuonyesha resilience ata wakati unapitia kipindi kigumu.

Haya ebu nielezee ulivyo tafsiri wewe hiyo aya mwisho inasemaje?
Unathrow back swali nililokuuliza
 
Kwa waliokaribu na TV tune in TBC 1

======



Ndege ya kwanza ya watalii imewasili nchini ikiwa ni baada ya Rais John Magufuli kuruhusu kuendelea kwa shughuli za utalii nchini baada ya kupungua kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona Tanzania.

Tarehe 20, Mei 2020, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi aliahidi ya kuwa mwishoni mwa Mei ndege ya kwanza ingetua nchini.

Waziri Kigwangala

“Tuna matarajio makubwa kuwa sekta ya utalii na usafiri wa anga itafunguka vizuri kadiri tunavyoelekea”

“Hii ni ndege ya kwanza ya abiria ni ya Ethiopian Airlines, marafiki zetu.”

“Kwa kuanzia Ethiopian Airlines watatua Jumatatu, Alhamis na Jumamosi kwa ndege za abiria. Watatua hapa lakini pia Zanzibar. Kwa sasa wameshusha abiria na mizigo Zanzibar wanashusha na hapa Kilimanjaro, wanaenda Addis na nchi nyingine”

“Kwa siku tano za wiki tutakuwa na ndege zinazotua nchini, lakini zinazotuhusu zaidi watu wa utalii zitatua kwa siku tatu -- Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi -- ambazo purely ni ndege za abiria wote lakini kwa kiasi kikubwa tunatarajia itakuwa ni watalii”

“Dunia inajifunza namna ya kupambana na janga zito kama hili la mlipuko wa Covid 19 bila kufunga shughuli za kiuchumi na maisha ya watu”

Tumejipanga vizuri na tuna uhakika kutakuwa na usalama wa wageni na wahudumu. Tumefanya ziara ya kukagua mifumo na tumejiridhisha kwamba

Naibu Waziri wa Afya, Dr Godwin Mollel

“Ndani ya nchi maambukizi ya Corona kila siku yanapungu, hii ni kumaanisha kuwa kuna mabo yanafanyika”

“Tumehakikisha kuwa miongozo ya Shirika la Afya Duniani na Wizara ya Afya imefuatwa katika kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19”

Meneja Uwanja wa KIA

“Tupo tayari kuipokea kuutangazia dunia kuwa tupo tayari kupokea wageni.”

“Leo tumefurahi kuona tumepokea ndege ya kwanza”

“Kabla ya corona tulikuwa tunapokea abiria wengi sana. Mwaka jana tulikuwa na abiria 28,000 kwa mwezi na hadi kufikia kipindi cha Corona tulikuwa na wastani wa abiria 19,000”

“Tumejipanga vizuri kuwalinda wageni na wageni dhidi ya Covid 19”

Ujio wa watalii uonekane kwenye mapato ya nchi. Hizo mbwembwe za kupotezeana muda waziache.
 
Watalii watakuja tu maana Corona lazima tujifunze kuishi nayo kama yalivyo magonjwa mengine.
Ni mawazo yako na huyo kilaza wako wa Chato. Dunia nzima watu wanaongelea ''maisha kubadilika'' mpaka hapo chanjo itakapopatika na wewe unaleta ufahamu wa nyumbu hapa. Watu kama wewe hata hawajui wastaafu ndiyo wanafanya kundi kubwa la watalii na hawawezi ku-risk maisha yao kuja nchi yenye viongozi wajinga kama yetu!
 
Kwa kipindi hiki watalii 200 Ni wengi Sana..😂
 
Back
Top Bottom