View attachment 2578766
Ndege ya KLM kutoka Amsterdam imeshindwa kutua uwanja wa ndege wa KIA masaa machache yaliyopita na kusababisha watalii na watu wengine karibu 150 kushindwa kuingia nchini.
Ndege hiyo ililazimika kwenda kutua Entebbe ambako taa zilikuwa zinaangaza kwa manjonjo yote. Pamoja na watu wazima wengi ndege hiyo imebeba wamama wajawazito, watoto na wazee ambao sasa wanahangaika kutafuta usafiri wa haraka.
Haieleweki tatizo ni taa au umeme au upepo. Kuna watu wengine wamesikika wakilitaja Jina la yule Marehemu Mpendwa, wakionesha kusikitishwa na Tanzania kuzidiwa na umeme wa Jinja.