Ndio nimefika Musoma Mjini ila nimehuzunika sana

Ndio nimefika Musoma Mjini ila nimehuzunika sana

Kwanini mkoa wa Mara hauendelei bado upo nyuma kwenye swala la viwanda?

  • Kwa walio fika MSM ulivutiwa na nini?

  • Mpangilio wa mji

  • Style ya maisha na ukarimu wao


Results are only viewable after voting.
Ushawishi tu wa watu wa Bukoba. Kuanzia na wabunge, mawaziri nk.
Huoni Malinzi tu mkuu wa TFF alihakikisha Bukoba inapata uwanja wa kisasa wa mpira kaitaba siku hiz unasaport hadi mechi za usiku
Watani/ndugu zetu wa Mara hawana ushirikiano na kuendeleza mkoa wao. Wana wasomi wengi sana lakini hawana umoja wala mpango kuendeleza mkoa.
 
Niliwahi kwenda home mida ya saa 3 usiku hivi nimetoka safari sijui kama mji una vibaka kila kona nikatoka Musoma bus hadi nyakato kwa mguu. Kufika nagonga hodi wakafungua ila wakanishangaa sana nimefikaje home tena kwa mguu?
Nikawaambia nilivyofika na hiyo ilikuwa mara ya pili

Wakasema simama tusali tulivyomaliza kusali, nikaambiwa Mungu wako mkubwa Musoma kwa sasa sio mji wenye usalama kuna makundi ya vijana wadogo wadogo wakorofi kila kikundi kina kiongozi na aina ya ubabe wake nikatajiwa baadhi ya makundi hayo mdomo wa furu, mbio za vijiti, mokasi aaah bana nikawaambia mi sijaonana na kikundi zaidi ya kupishana na mtu 1 mmoja au watu wawili wawili. Naambiwa kila kijana ilikuwa lazima ajiunge kwenye kikundi la sivyo utajuta.

Musoma bana vijana wengi hawana ajira na ni kama hawataki kujiajiri mbaya zaidi malezi ndo chanzo mama anazaa kisha anaenda vizingani anamuacha mtoto alelewe na bibi malezi ya hovyo bibi hajui kukanya wala kuchapa mtoto udokozi kama wote.

Mtoto ukimgusa tu bibi yake kafika kumtetea hata shuleni wana viburi bibi anaweza lalamika mjukuu hamsikilizi ila mguse mjukuu ndo utamjua bibi. Wajita hamna lile kabila hapana.

Kwa baadae niliambiwa alipelekwa RPC 1 akayatokomeza hayo makundi kwa kuwaweka ndani hadi wazazi alikuwa akikamata mtoto ukitia timu umuwekee dhamana unawekwa ndani na kulikuwa na malalamiko mengi ya wananchi kuhusu hayo makundi ila kwa baadae yaliisha kabisa

Musoma hata kibiashara hapafai kabisa bora uende Tarime mzunguko wa hela upo mkubwa.
 
Watani zao Bukoba. Wako wanaijenga barabara ya njia nne km 5, stendi mbili mpya, bandari ya Bukoba inapanuliwa, uwanja wa Bukoba unawekewa control tower, shopping complex mpya nk.
Kimsingi Bukoba inabadilika sana siku hiz.
Ndio mnaonja hayo kwa mara ya kwanza Ishomire?
 
Hussein sokoni alishafariki ila vijana wake nazani Bado wapo japo Kuna wengine walihamia mwanza,
Dah kumbe alishafariki basi Hussein sokoni kaacha Legacy siyo mchezo mchezo kabisa huko Musoma , jamaa jina lake lilikua kwenye midomo ya watu wengi sana ni mfanyabiashara aliewapelekea vitu vizuri
 
Katika mji ambao sijawahi kuuelewa ni Musoma, mji umekata tamaa miaka yote kama uliwahi kwenda mwaka 2004 na ukatembea tembea ukirudi tena baada ya miaka 20 mwaka huu 2024 utakuta pako vile vile hakuna maendeleo ya maana mji haubadiliki
Mji ukikosa wachaga na wanyantuzu hauwezi kuendelea.
 
Watani/ndugu zetu wa Mara hawana ushirikiano na kuendeleza mkoa wao. Wana wasomi wengi sana lakini hawana umoja wala mpango kuendeleza mkoa.
Wasomi hawajengi mkoa hata siku moja ,kwa sababu wengi ni waajiriwa .

Akili za watanzania karibia wote kwa sababu ya umaskini ,hawataki kufanya kazi mikoa ya kwao .
Mji yenye wasomi mingi imebakia kuwa na idadi ndogo ya watu .
 
Watani zao Bukoba. Wako wanaijenga barabara ya njia nne km 5, stendi mbili mpya, bandari ya Bukoba inapanuliwa, uwanja wa Bukoba unawekewa control tower, shopping complex mpya nk.
Kimsingi Bukoba inabadilika sana siku hiz.
Watani zako wao bado wapo zama za ujima yaani wanaishi kama binadamu wa kale yaani homo habillis kama sio homo erectus, kila kitu wanatumia nguvu badala ya akili.
 
Tutoe lai Kwa wenyeji wa Mkoa wa Mara kukumbuka na kurudi kujenga kwao.

Musoma haikui miaka na miaka
 
Back
Top Bottom