Ndio nimefika Musoma Mjini ila nimehuzunika sana

Ndio nimefika Musoma Mjini ila nimehuzunika sana

Kwanini mkoa wa Mara hauendelei bado upo nyuma kwenye swala la viwanda?

  • Kwa walio fika MSM ulivutiwa na nini?

  • Mpangilio wa mji

  • Style ya maisha na ukarimu wao

Results are only viewable after voting.
Da umenikumbusha mbali sana.wapi majita road,mkinyerero,mgalanjabho,bweri,mtakuja,buhare,nyasho mitumbani hapo.nyabange,nyakato,nimemkumbuka demu wangu salome.Iposiku nitarudi msoma.
 
Watani zao Bukoba. Wako wanaijenga barabara ya njia nne km 5, stendi mbili mpya, bandari ya Bukoba inapanuliwa, uwanja wa Bukoba unawekewa control tower, shopping complex mpya nk.
Kimsingi Bukoba inabadilika sana siku hiz.
Nikipata wasaa nitafika huko tuombe uzima tu.
 
Katika mji ambao sijawahi kuuelewa ni Musoma, mji umekata tamaa miaka yote kama uliwahi kwenda mwaka 2004 na ukatembea tembea ukirudi tena baada ya miaka 20 mwaka huu 2024 utakuta pako vile vile hakuna maendeleo ya maana mji haubadiliki
Ulisemalo ni sahihi kabisa, japo mabadiliko ni kidogo sana kwenye hili nimeshuhudia.
 
Ndugu zangu mnaoishi Musoma kwanza niwape pongezi kwa jinsi mnavyo pambana kupata mkate wenu wa kila siku.

Mkoa huu wa MARA japo una wakazi wengi wenye elimu ya sekondari na kuendelea ila nahuzunika kusema kundi kubwa la vijana wanahangaika mitaani kwa kukoswa ajira za kueleweka na kujikuta wanaishi kwenye mazingira magumu na hii inapelekea wengine kujihusisha na matukio ya kiuhalifu, kama kupora mali za watu na unyang'anyi.

Kwa hali kama hii ninapenda kuiomba serikali kulitizama kwa umakini sana ili kuiokoa jamii na matukio yasiofaa kama ubakaji na unyang'anyi. Maana tutaanza kusikia kuna makundi ya kihalifu kama miaka ya nyuma vijana walipokua na magenge ya uhalifu.

Ifikapo mida ya saa mbili za usiku, bado ni mapema sana ila huu muda usishangae kukutana na uporaji wa kutumia nguvu katika baadhi ya maeneo kama, Nyabange, Bweri, Majengo(songe), Baruti, Nyakato, Nyasho, nk. Inatakiwa jeshi la polisi liweke juhudi kutokomeza tabia za namna hii kwa Nguvu zote ili kuilinda heshima ya mkoa wa Mara. Naamini samaki hukujwa angali mbichi.

Nimefurahia ziara ya mkoani, japo maisha ya walio wengi ni changamoto.
Mkoa gani ambako watu awaangaiki kupata ajira?
 
...
Huoni Malinzi tu mkuu wa TFF alihakikisha Bukoba inapata uwanja wa kisasa wa mpira kaitaba siku hiz unasaport hadi mechi za usiku
Acha uzandiki kijana, so Mkwakwani, Dodoma napo ni malinzi sababu mechi zinachezwa usiku?.

Na unajua sababu ya mechi kuchezwa usiku?

Kuna kitu unataka kudanganya ila unasahau siyo wote wanaweza kudanganywa!.
 
Watani zao Bukoba. Wako wanaijenga barabara ya njia nne km 5, stendi mbili mpya, bandari ya Bukoba inapanuliwa, uwanja wa Bukoba unawekewa control tower, shopping complex mpya nk.
Kimsingi Bukoba inabadilika sana siku hiz.
Bk hawezi badirika sababu inajengwa na serikali kinacho badirisha watu kuwafanya wawe na maendeleo ni aridhi yenye rutuba mkoa wa kagera hakuna aridhi ya kilimo mji utabadilika lakini shida za vijana azitoisha
 
Niliwahi kwenda home mida ya saa 3 usiku hivi nimetoka safari sijui kama mji una vibaka kila kona nikatoka Musoma bus hadi nyakato kwa mguu. Kufika nagonga hodi wakafungua ila wakanishangaa sana nimefikaje home tena kwa mguu?
Nikawaambia nilivyofika na hiyo ilikuwa mara ya pili

Wakasema simama tusali tulivyomaliza kusali, nikaambiwa Mungu wako mkubwa Musoma kwa sasa sio mji wenye usalama kuna makundi ya vijana wadogo wadogo wakorofi kila kikundi kina kiongozi na aina ya ubabe wake nikatajiwa baadhi ya makundi hayo mdomo wa furu, mbio za vijiti, mokasi aaah bana nikawaambia mi sijaonana na kikundi zaidi ya kupishana na mtu 1 mmoja au watu wawili wawili. Naambiwa kila kijana ilikuwa lazima ajiunge kwenye kikundi la sivyo utajuta.

Musoma bana vijana wengi hawana ajira na ni kama hawataki kujiajiri mbaya zaidi malezi ndo chanzo mama anazaa kisha anaenda vizingani anamuacha mtoto alelewe na bibi malezi ya hovyo bibi hajui kukanya wala kuchapa mtoto udokozi kama wote.

Mtoto ukimgusa tu bibi yake kafika kumtetea hata shuleni wana viburi bibi anaweza lalamika mjukuu hamsikilizi ila mguse mjukuu ndo utamjua bibi. Wajita hamna lile kabila hapana.

Kwa baadae niliambiwa alipelekwa RPC 1 akayatokomeza hayo makundi kwa kuwaweka ndani hadi wazazi alikuwa akikamata mtoto ukitia timu umuwekee dhamana unawekwa ndani na kulikuwa na malalamiko mengi ya wananchi kuhusu hayo makundi ila kwa baadae yaliisha kabisa

Musoma hata kibiashara hapafai kabisa bora uende Tarime mzunguko wa hela upo mkubwa.
Umegusa penyewe kabsa🫡
 
Kwa fedha ipi utaenda kujenga kwenu.
Mishahara hii hii ya tanzania
Labda ule rushwa ili ukafie gerezani.
Ishi kulingana na kipato chako acha kuiga na kujifananisha na watu wengine
 
Ndugu zangu mnaoishi Musoma kwanza niwape pongezi kwa jinsi mnavyo pambana kupata mkate wenu wa kila siku.

Mkoa huu wa MARA japo una wakazi wengi wenye elimu ya sekondari na kuendelea ila nahuzunika kusema kundi kubwa la vijana wanahangaika mitaani kwa kukoswa ajira za kueleweka na kujikuta wanaishi kwenye mazingira magumu na hii inapelekea wengine kujihusisha na matukio ya kiuhalifu, kama kupora mali za watu na unyang'anyi.

Kwa hali kama hii ninapenda kuiomba serikali kulitizama kwa umakini sana ili kuiokoa jamii na matukio yasiofaa kama ubakaji na unyang'anyi. Maana tutaanza kusikia kuna makundi ya kihalifu kama miaka ya nyuma vijana walipokua na magenge ya uhalifu.

Ifikapo mida ya saa mbili za usiku, bado ni mapema sana ila huu muda usishangae kukutana na uporaji wa kutumia nguvu katika baadhi ya maeneo kama, Nyabange, Bweri, Majengo(songe), Baruti, Nyakato, Nyasho, nk. Inatakiwa jeshi la polisi liweke juhudi kutokomeza tabia za namna hii kwa Nguvu zote ili kuilinda heshima ya mkoa wa Mara. Naamini samaki hukujwa angali mbichi.

Nimefurahia ziara ya mkoani, japo maisha ya walio wengi ni changamoto.
Maisha ya sehemu uliyotoka yana afadhali?
 
Musoma wakurya ni wachache mno, musoma imejaa wenyeji wake wajita sehemu kubwa, wazanaki,....tarime kwa wakurya mji uko busy vizuri sana
Mkuu samahani swali nje ya mada, wazanaki wana sifa gani?
 
Mkuu samahani swali nje ya mada, wazanaki wana sifa gani?
Majisifu mengi kubeza vya wale walioweza, unakuta mtu kanunua gari ama kajenga nyumba kwa uwezo wake wenzie zao kubeza aaghh kanyumba gani kale, au kagari gani kale mi mwenyewe hata nikitaka kesho nanunua afu ukimwangalia mtu mwenyewe anatembea suruali imechanika matakoni hajui kesho anaamkaje ila anabeza aliye na uwezo wa kujenga na kuwa na usafiri wake tena sio usafiri tu yaani gari! Maana kuna usafiri, kuna chombo cha moto na kuna gari afu kuna ndinga 😄😄😄😄😄
 
😂 mbona kama tabia za kihaya

Tabia za Wanawake?
 
Acha uongo ,Bukoba ipo nyuma ,unaongelea stendi ambayo hata stendi ipo tangu 2020.

Viwanja vya ndege kila mkoa vinajengwa kaangalie hapo Musoma uone ..
Screenshot 2024-02-15 194551.png

Ujenzi wa stendi ya Bukoba. Hapa ilikuwa January 2024. Sasa sijui wamefikia wap.
Kabla ya kubisha Fanya research kwanza
 
Ndio mnaonja hayo kwa mara ya kwanza Ishomire?
Kwani hii Tanzania imeendelea sana mpaka unashangaa haya?
Tazama jiji la Dar ile terminal ya watu kwenda Zanzibar kama kibanda cha kuku, Tazama Barabara za masaki zilivyo.
Hii nchi Bado sana kiasi cha kuchangaa yanayoendelea Bukoba
 
Back
Top Bottom