Ndio nimefika Musoma Mjini ila nimehuzunika sana

Ndio nimefika Musoma Mjini ila nimehuzunika sana

Kwanini mkoa wa Mara hauendelei bado upo nyuma kwenye swala la viwanda?

  • Kwa walio fika MSM ulivutiwa na nini?

  • Mpangilio wa mji

  • Style ya maisha na ukarimu wao


Results are only viewable after voting.
Bukoba haikuwa na stendi lakini una Airport Bora kabisa, stadium nzr kabisa, mji mzima una Barabara za lami, shule kibao, hospital kibao, bandari kubwa.

Nyinyi mnajenga stendi halafu Barabara za mitaa ni ovyo kabisa mfano ni Morogoro, kigoma, singida😂 miji ina stendi nzr lakin Barabara za mitaa sasa.
Bukoba Barabara za mitaa kwanza stendi baadae. Watu hawaishi stendi
Ngoja uzi wenu uwasili kutoka sehemu. Usitoroke.
 
Umenikumbusha kitambo kidogo enz nimeishi Musoma na kusoma pia form five nusu muhula,kulikua na kund moja la kibabe walikua wakijiita "JAMAICA MOKAZ" walikua wababe balaa,tulikua tunawaogopa mno,nashukuru Mungu nilihama mapema,ila Musoma ni pazuri,especially bei za electronics na nguo ni nzur hazijachangamka sana.
 
Katika mji ambao sijawahi kuuelewa ni Musoma, mji umekata tamaa miaka yote kama uliwahi kwenda mwaka 2004 na ukatembea tembea ukirudi tena baada ya miaka 20 mwaka huu 2024 utakuta pako vile vile hakuna maendeleo ya maana mji haubadiliki
Kama Lindi vile?
 
Watani zao Bukoba. Wako wanaijenga barabara ya njia nne km 5, stendi mbili mpya, bandari ya Bukoba inapanuliwa, uwanja wa Bukoba unawekewa control tower, shopping complex mpya nk.
Kimsingi Bukoba inabadilika sana siku hiz.
Unaongelewa Mkoa wa Mara ( Musoma ) Wewe unaleta taarifa za Mkoa wa Kagera ( Bukoba ) sijui ni lini Watu wengine mtaachana na Ungandamba ( Ushamba ) mlionao.
 
Katika mji ambao sijawahi kuuelewa ni Musoma, mji umekata tamaa miaka yote kama uliwahi kwenda mwaka 2004 na ukatembea tembea ukirudi tena baada ya miaka 20 mwaka huu 2024 utakuta pako vile vile hakuna maendeleo ya maana mji haubadiliki
Ila ndiyo Mkoa wanaotoka Werevu ( Intelligents ) tupu Tanzania nzima ukibisha hili huna Akili na ni Mwehu tukuka.
 
Kuwa na Adabu Kijana sawa? Kwahiyo unataka nikupe Sifa Tukuka za Dada zangu wa Kizanaki ili Unikazie kwa Usununu / Hasira?
Hapana mkuu nataka nijue sifa ili nijue hapa nilipo niishie hapa hapa au nifike Musoma kuhalalisha jambo. Hutaki shemeji mkuu?
 
Ndugu zangu mnaoishi Musoma kwanza niwape pongezi kwa jinsi mnavyo pambana kupata mkate wenu wa kila siku.

Mkoa huu wa MARA japo una wakazi wengi wenye elimu ya sekondari na kuendelea ila nahuzunika kusema kundi kubwa la vijana wanahangaika mitaani kwa kukoswa ajira za kueleweka na kujikuta wanaishi kwenye mazingira magumu na hii inapelekea wengine kujihusisha na matukio ya kiuhalifu, kama kupora mali za watu na unyang'anyi.

Kwa hali kama hii ninapenda kuiomba serikali kulitizama kwa umakini sana ili kuiokoa jamii na matukio yasiofaa kama ubakaji na unyang'anyi. Maana tutaanza kusikia kuna makundi ya kihalifu kama miaka ya nyuma vijana walipokua na magenge ya uhalifu.

Ifikapo mida ya saa mbili za usiku, bado ni mapema sana ila huu muda usishangae kukutana na uporaji wa kutumia nguvu katika baadhi ya maeneo kama, Nyabange, Bweri, Majengo(songe), Baruti, Nyakato, Nyasho, nk. Inatakiwa jeshi la polisi liweke juhudi kutokomeza tabia za namna hii kwa Nguvu zote ili kuilinda heshima ya mkoa wa Mara. Naamini samaki hukujwa angali mbichi.

Nimefurahia ziara ya mkoani, japo maisha ya walio wengi ni changamoto.
Ndio wapi huko?
 
Unaongelewa Mkoa wa Mara ( Musoma ) Wewe unaleta taarifa za Mkoa wa Kagera ( Bukoba ) sijui ni lini Watu wengine mtaachana na Ungandamba ( Ushamba ) mlionao.
Lazima tuwatese nyinyi watani. Washamba sana nyinyi. Naam naona unateseka😂
 
Back
Top Bottom