Ndio nimefika Musoma Mjini ila nimehuzunika sana

Kwanini mkoa wa Mara hauendelei bado upo nyuma kwenye swala la viwanda?

  • Kwa walio fika MSM ulivutiwa na nini?

  • Mpangilio wa mji

  • Style ya maisha na ukarimu wao

Results are only viewable after voting.
Ngoja uzi wenu uwasili kutoka sehemu. Usitoroke.
 
Umenikumbusha kitambo kidogo enz nimeishi Musoma na kusoma pia form five nusu muhula,kulikua na kund moja la kibabe walikua wakijiita "JAMAICA MOKAZ" walikua wababe balaa,tulikua tunawaogopa mno,nashukuru Mungu nilihama mapema,ila Musoma ni pazuri,especially bei za electronics na nguo ni nzur hazijachangamka sana.
 
Katika mji ambao sijawahi kuuelewa ni Musoma, mji umekata tamaa miaka yote kama uliwahi kwenda mwaka 2004 na ukatembea tembea ukirudi tena baada ya miaka 20 mwaka huu 2024 utakuta pako vile vile hakuna maendeleo ya maana mji haubadiliki
Kama Lindi vile?
 
Watani zao Bukoba. Wako wanaijenga barabara ya njia nne km 5, stendi mbili mpya, bandari ya Bukoba inapanuliwa, uwanja wa Bukoba unawekewa control tower, shopping complex mpya nk.
Kimsingi Bukoba inabadilika sana siku hiz.
Unaongelewa Mkoa wa Mara ( Musoma ) Wewe unaleta taarifa za Mkoa wa Kagera ( Bukoba ) sijui ni lini Watu wengine mtaachana na Ungandamba ( Ushamba ) mlionao.
 
Katika mji ambao sijawahi kuuelewa ni Musoma, mji umekata tamaa miaka yote kama uliwahi kwenda mwaka 2004 na ukatembea tembea ukirudi tena baada ya miaka 20 mwaka huu 2024 utakuta pako vile vile hakuna maendeleo ya maana mji haubadiliki
Ila ndiyo Mkoa wanaotoka Werevu ( Intelligents ) tupu Tanzania nzima ukibisha hili huna Akili na ni Mwehu tukuka.
 
Kuwa na Adabu Kijana sawa? Kwahiyo unataka nikupe Sifa Tukuka za Dada zangu wa Kizanaki ili Unikazie kwa Usununu / Hasira?
Hapana mkuu nataka nijue sifa ili nijue hapa nilipo niishie hapa hapa au nifike Musoma kuhalalisha jambo. Hutaki shemeji mkuu?
 
Ndio wapi huko?
 
Unaongelewa Mkoa wa Mara ( Musoma ) Wewe unaleta taarifa za Mkoa wa Kagera ( Bukoba ) sijui ni lini Watu wengine mtaachana na Ungandamba ( Ushamba ) mlionao.
Lazima tuwatese nyinyi watani. Washamba sana nyinyi. Naam naona unatesekašŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…