Ndoa hapana! Sitaki

Ndoa hapana! Sitaki

Mtu anataka kwenda kutoa mahali,
Alafu yeye mwenyewe hajipendi, anataka aanze kujipenda,
Ni mvuta sigara na mnywa pombe alafu hajui sababu zinazomfanya awe hivo. Ndio anataka kuacha,
Hana akiba, ndio anataka kuanza kuweka akiba,
Kataka kutoa mahali, anaambiwa milioni mbili, kashtuka eti hatoi tena.

Jamani tunamshauri nini huyu, si kijana wa hovyo huyu.

Mbona mahali ni jambo la hisia sana.
Si hajitambui huyu.
Kwanza tumfanye ajitambue. Aimbe ushauri huo.
 
Mkuu kila la kheri naamini lazima utoboe

Huyo mwanamke angekuletea mapicha picha ya ajabu na matumizi makubwa yasiyokuwa na msingi

Ubahili ni mzuri,ila usijibane kwenye kula,kuvaa na kulala pazuri
 
Kamna cha blabla nyingi, sema wewe ni shoga tu. Mwanaume kamili anayajua majukumu yake haogopi kuoa. Milioni 2 ni hela ya kawaida tu ila wewe inakutoa ushuzi.
Shoga? Ulijuaje uliwahi kuwa na uhusiano naye na alikulala?
 
We mjinga Sana eti! Sasa hiyo milioni mbili kwani unatoa yote??

Endelea kuweka akiba uje utoe mahari million ishirini ukifika 40yrs,

Muulize baba yako alitoa ngapi?

Zama zimabadilika

Halafu mnawasikiliza hawa wa jf?? Asilimia 85 wenzio wameoa humu,wasiooa ni wewe na wenzio 14.
 
5.nakuwa mtu wa kujipenda na kupendeza kuvaa vizuri

Ukizingatia hii utapata wake wengi zaidi bila hata mahari mkuu
 
Nilikwenda kuchumbia mahali fulani...majibu yakatoka nikaambiwa nipeleke milioni mbili..,nimejitafakari aisee ni hapana sijajua wazazi wa Binti watanifikiria vipi ...ila watanisamehe tu.

Kwanza naenda kumnunua mtu...pesa inatoka hapo,pili natakiwa niwe namhudumia kwa kila kitu nikiwa naye nayo ni pesa hio,tatu Mwanamke atakuja kunibana aisee nishazoea kulala pekeangu,nne nahofia tukiachana nitapoteza hata hivi vichache nilivonavyo...mwisho kabisa Mwanamke nimemuona mtu wa lawamalawama sana...kwanza ni ngenye ndio zilisababisha harakaharaka nichumbie

Binafsi nikifikisha miaka 40 labda ndio nifikirie kuoa kwa saivi najitafuta kwanza nahitaji niimarike kiuchumi

Mikakati ninayokuja nayo

1.naacha pombe,sigara
2.nakuwa mtu wa ibada na kusoma vitabu.
3.nakuwa mchumi na mbahili lakini nataka nifanye kazi kwa bidii sana
4.naweka akiba
5.nakuwa mtu wa kujipenda na kupendeza kuvaa vizuri
6.mbinafsi.

Note:ndoa ni muhimu lakini sio lazima
2m unakimbia ehhhh.
Siungeongea nao wakakupunguzia au ukawa unalipa kidg kidg maan mahali hua haiishi.
 
Back
Top Bottom