Nilikwenda kuchumbia mahali fulani...majibu yakatoka nikaambiwa nipeleke milioni mbili..,nimejitafakari aisee ni hapana sijajua wazazi wa Binti watanifikiria vipi ...ila watanisamehe tu.
Kwanza naenda kumnunua mtu...pesa inatoka hapo,pili natakiwa niwe namhudumia kwa kila kitu nikiwa naye nayo ni pesa hio,tatu Mwanamke atakuja kunibana aisee nishazoea kulala pekeangu,nne nahofia tukiachana nitapoteza hata hivi vichache nilivonavyo...mwisho kabisa Mwanamke nimemuona mtu wa lawamalawama sana...kwanza ni ngenye ndio zilisababisha harakaharaka nichumbie
Binafsi nikifikisha miaka 40 labda ndio nifikirie kuoa kwa saivi najitafuta kwanza nahitaji niimarike kiuchumi
Mikakati ninayokuja nayo
1.naacha pombe,sigara
2.nakuwa mtu wa ibada na kusoma vitabu.
3.nakuwa mchumi na mbahili lakini nataka nifanye kazi kwa bidii sana
4.naweka akiba
5.nakuwa mtu wa kujipenda na kupendeza kuvaa vizuri
6.mbinafsi.
Note:ndoa ni muhimu lakini sio lazima