Ndoa hazivunjiki kwasababu ya kuoa mke bikira ila kwa kuchunguzana au kupelelezana period

Ngoja nikusaidie boss wangu Natafuta Ajira hilo swali nililo kuuliza kuhusu ili uinjoy sex unahitaji tango kubwa au dogo?

KIfupi tango kubwa au dogo havina uhusiano wowote na kuinjoy sex,bali sex ili uinjoy inahitaji mambo kadhaa,kwanza hisia juu ya mwenza wako iwepo,maandalizi ya kutosha kabla ya game,hizo ndio nyenzo kuu za kuwa na good sex

Ukifuzu hapo hata ukiwa na nchi mbili pisi itainjoy sex

Asante
 
Shusheni hivyohivyo tu standards za wanawake wa kuwaoa

Kaeni mkijua wanawake wamewazidi akili pakubwa mno

Ndoa zitaendelea kuwatesa sana
Vijana wamezidiwa akili na wanawake wamebaki kuja na blah blah kibao za kutetea usimp wao.

Wanawake wanajua standard wanayoitaka kwa mwanaume ambayo ni uwezo wa kifedha. Uwaambie wanaume masikini wana haki ya kupendwa, wana nyege pia, maisha ya sasa ajira ngumu wanawake hawaelewi sababu wala kisingizo chochote all they want is money.

They are determined and ruthless, they don't settle for less, they don't give a fvck

Ila mivijana ya kiume imekua kama mitahira, kuweka msimamo wa standards zao hawawezi. Standard ya mwanamke ni bikira ila kizazi cha vijana masimp kimekubali kuwekewa standard za hovyo hovyo na wanawake.
 
Mimi nakuelewa. siyo kila mwanamke anastahili kuchunguzwa. inategemea uko na mwanamke wa aina gani.

Huwezi kuwa unadate na mshangazi alafu uanze kuuchunguza wakati umekuoa wewe.

Huwezi kuwa mke/mchumba ambaye unajua mtaa mzima washapita alafu uanze kumchunguza, ili iweje sasa.

Kuamua kumchunguza au kutomchunguza mke/mchumba huwa inakuja automatically. Utamchunguza mke/mchumba unayemthamini au utampotezea kama hana thamani kwako.

Ila kama umeoa mtoto wa watu ambaye amejitunza na una malengo mapana ya kuwa na familia bora, lazima utamchunguza kwa sababu una mthamini na unamlinda.

Mimi nimedate na wanawake wengi, ila ni mmoja tu ambaye nina mzuka wa kumchunguza. kwa sababu nina malengo naye. Wengine huo mzuka wa kuwachunguza sina kabisa.

Kumchunguza mke/mchumba ni sawa sawa na kumthamini na kumlinda, believe it or not.
 
Kama ambavyo upo tayar kumchunguza basi uwe tayar kupambana na matokeo yake na uwe tayar kufanya maamuzi magumu.

Kuna mwamba alimchunguza mkewe yupo humu jf bahati nzuri katika chat akakuta mkewe anawaambia mashosti zake kuwa "mume wake anapiga show kila mara" ni habar nzur

Jiandae kisaikolojia ukikuta mkeo anachati na mashosti kuwa "yaan mume wangu hanili vizur hlf kimoja tu chali" najua hapo utawaza mengi sana,inabidi ujikaze kwasababu umeyatafuta yenye kukuhuzunisha

Asante
 
Dogo unajua hata maana ya redpill kwanza???
 
Unabishana na Cuckold watu kama huyo jamaa hata akimfumania mke wake anatoumbwa na jamaa mwingine kwenye kitanda Chake ndani ya nyumba yake aliyojenga mwenyewe Bado atamsamehe mwanamke huyo akiamini kwamba yeye ndio chanzo Cha mke wake. kuchepuka.
 
Baba yake Hakimi angefanya kazi nzuri, asingefika huko na mkewe. Na pia, ukishakuwa na status ni muhimu kujua na kuangalia nani wakuwa mama wa watoto wako, maana kuzaa tu sio shida. Malezi ni muhimu.
Dear Chujio kwa kukujuza tu, baba yake Achraf Hakimi alishafariki miaka Mingi sana wakati Hakimi Bado mdogo kabla hajaanza hata kucheza mpira, yeye alilelewa na mama yake tu Bi.Saida Houb The queen of all mothers in this gynocentric modern era na mama yake ndio alipambana mpaka kufika hapo alipofika.

Na pia kwanini umekimbilia kumtupia lawama mzazi(baba) wa HAKIMI kwa utapeli aliokuwa anataka kukufanya yule mtalaka wake(Hiba Abouk)????

Kwamba kwenye mgogoro wowote wa kindoa unaopelekea mpaka taraka mwanamke yeye anakuwaga Hana kosa, Bali kosa linakuwa kiumeni tu si ndio?????
 
Hakuna haki zozote kwenye hiyo sheria ya ndoa kugawana Mali, Bali ni ukandamizaji tu na uonevu kwa Mwanaume.

Yaani wewe umeolewa na Mwanaume umemkuta ana networth ya 200m, haya umekaa naye miaka minne kwenye ndoa networth yake imefika 300m....

Halafu leo hii mahakama inaamua eti mgawane 50-50 yaani kwenye hiyo networth ya 300m wewe uchukue 150m na wakati kwa kipindi chote mlichoishi nae kiasi kilichoongezeka ni 100m, Sasa hata kama ni kugawana kwanini msigawane ile 100m ambayo ndio imepatikana kipindi ambacho na wewe upo?? Huoni kwamba kugawana 300m yoye itakuwa mnagawana mpaka na hela alizozitafuta kabla hajakutana na wewe na itakuwa ni wizi ulio wazi kabisa??

Na kama hiyo haitoshi Bado pia Mwanaume ataendelea kutoa child support Kila mwezi, imagine yaani tayari umeshakuchua hela za kutosha lakini Bado pia Kila mwezi Mwanaume akupe hela, na wakati unaweza ukazitumia hizo hela mlizogawana kuwalea hao watoto wenu mliozaa...

lakini usijali muda si mrefu hizi kelele zitaisha maana hakuna Mwanaume mwenye akili timamu na mafanikio yake atakayekuwa na uthubutu wa kuoa... Wanawake mtabaki mnaoana nyie nyie tu
 
Aisee jombaa umeoa tayari?

Kama hujaoa Kuna binamu yangu anahitaji mume nikupe umuoe mwanangu.

Maana naona akiwa na wewe ata enjoy sana, ila chonde chonde sitopenda watoto wake wa kiume waje wawe kama wewe.
 
Mkuu umeongea kiuanaume Sana asipoelewe basi.
 
Umempa mfano mzuri ila ameshindwa kuulewa hata kidogo...

Serikali inatulinda sisi raia wake, lakini hiyo hiyo serikali Ina vyombo kama TISS ambayo kazi yake ni kutuchunguza sisi, kwanini Inakuwa hivyo?

Hivyo hivyo pia kwa mwanaume yapaswa Aishi na mwanamke lakini asiache kumchunguza hili kuhakikisha kwamba yeye mwenyewe na huyo mwanamke wako salama ziku zote za ndoa yao.... Ila yeye amechagua kuwa mbivu wa kufikiri na kuongozwa na Imani.

Lakini tusimlaumu sana Kuna wanaume wengine wamelelewa kwenye mazingira ambayo wamezungukwa na wanawake tupu kwa hiyo mtu kama huyu anakuwa na Ina Imani sana na Kila mwanamke anayekutana nae ukubwani... !!
 
Sawa, ndio maana wanawake wengi siku hizi wanakimbia ndoa pia sababu kizazi cha wanaume wa sasa hawajui wajibu wa baba kwenye familia 😃 Hawana mifano mizuri ya wanaume wenye kuuvaa ubaba inavyopaswa. Na wale wenye ndoa nzuri wametulia zao wanakula mema ya nchi huku akina nyie mnalia mitandaoni.

Ewe kijana, chaguzi sahihi ni muhimu. Unaoa mtu anayeona kuwa na trako ndio kila kitu halafu unakuja kulia akisepa na pesa zako. Huyo ndio unayetarajia awe mama wa watoto wako. Mnapanda mbegu sehemu sehemu za ovyo zisizo na rutuba mkitegemea kuvuna mema. Ndoa yenu ni batili toka mwanzo halafu mnategemea mle mema ya ndoa hiyo wakati msingi wa ndoa yako umejenga juu ya mchanga wa bahari
 
Nashukuru kwa ufafanuzi huu. Nadhani kinamna unaona ninapoelekea. Uwepo wa baba ni muhimu kwa ustawi wa familia. Au kwa kesi ambazo ametangulia mbele za haki, ni muhimu kukawa na mtu wa kiume (yaweza kuwa babu, baba mkubwa, mjomba) ambaye mtoto anamtazamia kuwa mfano wa namna mwanamme au baba anavyopaswa kuwa
 
We didn't run away from our responsibilities, we unlock the code that, no woman loves a man unconditionally, women are only attached to what a man can bring on to the table, that's,man's achievements, money, success, resources etc
 
We didn't run away from our responsibilities, we unlock the code that, no woman loves a man unconditionally, women are only attached to what a man can bring on to the table, that's,man's achievements, money, success, resources etc
Sasa unaelekea kwenye ukweli, a man is loved with conditions..that he provides. Women and children are loved unconditionally. Nikipata namna nzuri ya kutetea hii nitarudi kuelezea
 
Huwa mara nyingi sipendi porojo lkn kuna porojo moja naona inahitqji kujibiwa hapa au kuwekwa sawa

Kuna hii ishu kwamba eti wanawake wametuwekea viwango vyao vya kuolewa badala viwango vyao vingekuwa ni bikira,,hii sijui ina uzito gani hasa katika swala zima la kujenga famillia

Kwa mujibu wa mafundisho yangu ya dini na ambayo yana play kiasi kikubwa katika jamii hasa linapokuja swala la kupata mwenza wa kuoa,kuna standards zifuatazo

Mosi, Ukoo aliotoka binti,hili ni jambo muhimu sana kujua kwa undani ukoo au nasabu ya ukoo husika,kuna baadhi ya tabia huwa zinasambaa katika koo hiyo na kurithishana vizazi na vizazi,hivyo ni muhimu sana kuoa kwa kuangalia koo husika

pili, mwanamke mwenye dini,hapa mwenendo mzima wa dini unachukua nafasi kubwa sana kumchunga na kumuongoza binti husika,ucha mungu unapatikana kutokana na kiasi gani binti anamjua Mola wake, binti wa namna hii tegemea ukiwa naye utastarehe kwakuwa ana hofu ya Mungu.

tatu, mali yake,hapa mwanamke anaweza kuolewa kwa kigezo cha kuwa na mali,unaweza kuamua kumoa mke kutokana na ukwasi wake

nne,kutokana na uzuri wake,binti anaweza kuolewa kutokana uzuri wake,ukavutiwa nae na kuamua kumuoa,kumbuka uzuri uko machoni kwa muoaji,na Mtume Muhammad (s.a.w) anasema Oa mwanamke ambaye ukimtazama basi nafsi inafurahi


Hizi ndizo standards za kumuoa mke,na sio hizo za ubikira,ubikira kama anatoka ukoo wa hovyo ina faida gani,ubikira kama binti si mcha mungu unafaida gani,ubikira kama binti hakuvutii unafaida gani,ubikira kama binti ana tabia mbaya unafaida gani

Think big boys!
 
Kuna ishu nyingine nayo sio mbaya nikiigusia tena walau kidogo,ni swala zima la kumchunguza mke,hii vijana wa hovyo ndio imekuwa ajenda yao kubwa siku hizi,na hii yote ni kutokana na kuigaiga ujinga kutoka mitandaoni

Ndoa haijengwi kwa kuchunguzana bali inajengwa kwa kuheshimiana na kuaminiana,ukimuamini mwenza wako unakuwa na amani sana na hata mapenzi yanakuwepo baina yenu

Lakini mkiwa hamuaminiani ndoa hiyo haiwezi kuwa na ile furaha ya kweli,kila mtu anajikuta anaishi na mwenza wake mguu nje mguu ndani,matokeo yake,hata yakitokea mambo madogo madogo tu labda ya mwenza kachelewa kurudi kazini basi wewe huku moyo unawaka moto

Umemtafuta mume au mke kwenye simu hakupatikana basi wewe huku moyo unawaka moto,je utaishi maisha haya mpaka lini? Ebu jionee huruma walau mara moja,you deserve to be happy na ndoa yako

Hivi umemuoa mke kumchunguza au kufurahia maisha yenu ya ndoa pamoja,kile kitendo tu cha wewe kuhaingaika kumfuatilia mke kuwa anawasiliana na nani,ni shida kubwa sana unajipatia,je unatarajia kuvuna nini kama sio maumivu?

Ebu fanyeni uchunguzi kwa wale wote ambao walifanya huu ujinga na ambao wanaendelea kufanya huu ujinga je wameambulia nini kama sio.majonzi tu

Na wewe ulivyo mpuuzi unaendelea kufanya ujinga ule ule,halafu kesho na kesho kutwa unaanza kulialia,je ulitarajia nini kwani?

Think big boys!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…