Ndoa na Mirathi: Nafasi ya Mahakama ya Kadhi kwa Wanawake

Status
Not open for further replies.

tuko pamoja
 

We intelekcho kama unaona sheria za mirathi za kihaya si zakulinganisha na za kiislamu inakuwaje wewe unalinganisha MoU na mahaka ya kadhi?
 

Hapa hakuna robot. Wote tuna mawazo na huwezi kutupeleka wewe kwa maswali ambayo yapo invalid, rejea juu huko.

Mahakama ya kadhi si ya kumsaidia mwanamke wa Kiislaam pekee, ni kwa jamii nzima, iwe mwanamke, mwanamme, mtoto, kijana, mzee na hata wasio Waislaam watafaidika nayo kwa namna nyingi sana.

Tunataka Kadhi atambulike rasmi, tulikuwa nae lakini Nyerere ndiye alimuondoa.
 
Aaaghrrrr tumechoka jamani, wapeni hiyo mahakama lakini nasisi wabarabaigi tuna mahakama zetu za kijadi tunaomba tupewe na sisi ni muhimu kwetu maana hii ndio dini yetu hatuna uislam wala ukristo

Nadhani unashindwa kuelewa kuwa Uislaam ni "Universal" na haijalishi kama ni Mbarbaig au Mturkana.
 

Kiislaam, hata gharama za maziko ya Marehemu yanatakiwa yafanywe na mali zake alizoacha (kama kaacha), kumbuka gharama za maziko ya Kiislaam ni ndogo sana na hakuna kuchapisha ma t shirt wala kuvaa sare. Ni sanda yake, na gharama ndogo ndogo za kuchimba kaburi, kufikisha mwili na kuuzika. Zingine zote ni ziada na hazina mpango Kiislaam.

Baada ya gharama za maziko, mali yake (Marehemu) ilipe madeni yake kwanza, itayobaki ndio wagawane warithi kwa mujibu wa sharia, ipo wazi kabisa kwenye Qur'an na kama huielewi unauliza wanayoielewa.

Warithi wanarithi alichoacha marehemu kama ni mali au madeni "accordingly".

Isitoshe, si ruhusa Muislaam kusema "sitaki urithi gawaneni nyie" hiyo hakuna, inachotakiwa mgawane urithi na ukishapewa fungu lako kama ni mali au madeni ndio ama uyagawe ama uyapokee baada ya kukabidhiwa, unachogawa hapo kinakuwa ni chako na si cha marehemu.
 

Wakuu mbona mnaongea kama "mmetumwa?" Unaposema kwamba "alichoongea" kama mwakilishi wa Makanisa bila kukitaja alichosema unataka tukuelewe au unataka kujifurahisha mwenyewe? Khaaaaa! Halafu wewe ulitegemea Jambo la "Kidini" liongelewe "Kisheria?" Mambo ya "Ibada ya Waislamu" unategemea yangeongelewa vipi? Wewe endelea kumheshimu Mwakyembe anapozungumzia mambo ya kisheria, then ukimpeleka kuongelea mambo ya kidini usimlazimishe azungumzie Sheria!
 

Huu utaratibu mbona ndio unafuatwa hata na makabila?

Serikali nayo inasimamia utaratibu huu wa mirathi.Ndio maana utaratibu unaitwa "administration of deceased estate" - MADENI kulipa, na kugawana kilichobaki kufuatana na mila, sheria na dini.
Mnachogombea cha ajabu hasa ni nini?
 
Britain has 85 Islamic Courts: Soma hapa Itatupa mwanga zimeanzishwa na nani na zinafanyaje kazi na zinawasaidia vipi wanawake wa Kiislamu na watu wengine ambao si Waislamu ambao wanatakiwa kunufaika nazo.
 

wewe utajitia aibu kabisa kutetea utumbo
Mwakyembe 'amezungumza bungeni'
je bunge ni mahali pa ibada?au sheria?
yeye akiwa kama mwanasheria alikuwa na wajibu wa kuwasaidia wenzie wasiojua sheria
suala la mahakama ya kadhi kisheria lipelekwe vipi....
mbona Kenya ambako mostly ni wakristo waliweza kujadili kisheria na kufikia muafaka?
 
Mbona ueleweki unataka kusema nn!!!mara zitto mara mudhiri...!!tulia utupe habari
 
- Anasema ilikuwa ni Mh. Zitto bila kujali Dini yake, aliyeokoa jahazi, kwa kweli kwa hilo Mungu akuzidishie sana Mheshimiwa na you have my respect.
Le Baharia William @..New York City, USA

What's the point behind....

Enhe Zitto aliokoaje jahazi...dont leave your post hanging, fill it.
 

Mimi binafsi sikuelewi una maana gani au umetumwa kufanya kampeni,kama sivyo basi weka minofu tutafune wenye meno alaaaaaaaa.
 

Bunge ni mahali pa kutunga Sheria, lakini linataka kugeuzwa mahali pa Ibada! Hili suala lingeweza kuzungumzwa Msikitini lingeeleweka zaidi, kwa kuwa ni Ibada ya Waislamu! Kwani Muhammad aliagiza kwamba Mahakama zenu ziendeshwe na kugharamiwa na Serikali? Mbona mambo ya Hija hayaletwi Bungeni yakajadiliw? Sijajua masuala ya Kenya yanaingiaje hapa Tanzania, kila watu na mambo yao, kama ilivyo kwa Uingereza na Marekani walivyoamua kukumbatia "ukameruni!"
 
Thanks Mwakaboko kwa ufafanuzi zaidi, mimi sikuiona Bungeni lakini kwa haya niliyoyasikia pamoja na kukusoma hapo kwa kweli Mheshimiwa Zitto anastahili heshima ya taifa.
Unaikuza mno, heshima ya taifa for what? acheni hizi za dezo jamani,tuwe serious kuliko kutoa awards tu bila mpangilio, unataka kusema haya mawazo ni mara ya kwanza kutolewa?
 
Sielewi hata moja, naona mwabishana tuuuu! Kwani hii mahakama ina umuhimu gani kwa taifa hili mpk kila kukicha tuijadili weee kuliko wenyewe wanavyoijadili msikitini?

Tena cha kushangaza waislamu wa hapa mtaani kwetu hawana hata habari ya uwepo wa ishu yenyewe na wanaiongelea kama ni jambo la watu fulani lisilowahusu. Haya, kesho ndio kesho. Kama kuna mwanaume na aandamane wkt Alhaji Kova kasema NO
 

unashangaza sana wakati qurani imebainisha kwamba Adui wa waislamu ni Wayahudi..,, Na walio karibu kwa urafiki ni wale wasemao sisi ni Wakristo. Au, Allah kadanganya tukuamini wewe topical? kwamba Wakristo ni maadui wa waislamu! Haya qurani inasema Wakristo ni wapole na wenye huruma. Hadith inasema mtawafuata hao Wakristo Shibrin shibrin dhirin dhirin hata shimoni na shimo hilo lina ng'e! kwa sababu ni wabora. Sasa rafiki yako anakushauri wewe unamuona ni adui! Ukaafir huo!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…