Ndoa ya Aziz Ki ni maisha yake binafsi, lakini Wacha nitie neno kidogo

Ndoa ya Aziz Ki ni maisha yake binafsi, lakini Wacha nitie neno kidogo

Kazi kweli kweli! Sema mfikishie salamu vunja maprice.Mwambie habari za kuwaita watoto wazuri dada dada zitamgharimu siku moja, pale alikuwa anapata copy.Yule kidoti aliamua kumbless tu alikuwa na stress za ukiwa baada ya yule mzee wa Chato kutembea
Wakinga tunazalisha sisi wengine ndo wanafata, pale tulitaka kuosha rungu na kupita..!!
 
Naona walitaka waolewe wao😅😅
Wanaume kwani mlitaka Aziz awaoe nyinyi? nikisoma post za wanaume wazima mnatokwa maneno kama maporomoko ya maji khaa!
MMEUMIA KWA KUWA AMEVUNJA KWA KISHINDO kebehi zenu! Kawategua nyonga maamae!
 
Huyu karubuniwa, na nahisi uongozi wa Yanga unahusika kwa asilimia kubwa katika kulitengeneza hili jambo na kulifanikisha. Sijawahi kuona shughuli ya taasisi inahusishwa na faragha za watu ila nilipoona Haji anaanika vitu visivyopaswa kuanikwa kwenye kilele cha siku ya mwananchi nikagundua kuna nguvu kubwa ya watu wanao push hili swala.

Kuhusu kufunga ndoa kwa kipindi hiki nadhani sababu kubwa ni ya kidini, Azizi Ki ni muislam na mwezi wa tatu mwanzoni watu wanaingia kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhani
Mi kinachonopa maswali ni kuhusu mama yake mzazi kutopewa taarifa mapema, na kushiriki

Na amemind ameongea SS hii si sawa!
 
Ila watu wana moyo sana, a 28yr old marries a single mother of two! At such a young age, kweli???? I hope jamaa nae ana watoto kadhaa, otherwise mmmh!
🤣🤣
Ndo nimeelewa Kwann mama mzazi WA ki amemind
 
Hapa angekuwaepo warumi rip,tungejua mengi

🤣🤣

Jmn jux nae jafunga ndoa, Vanessa pia ....
Huu ni mwaka wa "I do"
 
Amemuoa Kwa sababu ya mimba aliyo mpa. Ili mtoto awe halal, ila acha wivu kaka maisha hayana formula
 
Binafsi nampongeza Aziz ki Kwa kupata jiko, ila Nina haya

1. Wazee wanasema kuwa anayeona laZima aulize,
Sina uhakika kama kijana wetu Aziz ki aliuliza na kuchakata kuhusu mkewe.
Au alikutana na machawa wakamjaza akajikuta ameingia cha kike.
Nadhani Kwa maisha ya football ingekuwa njema akapata mke wa kumpa utulivu tofauti na Mobeto

2. Wazazi au ndugu wa Aziz ki kutoonekana siku ya kutoa mahali.
Eng Hersi ndo alisimama kama mzazi,
Hili halikuwa jema
Mama yake Aziz ki yupo Burkina Faso sio mbali ni kufika na kumpa heshima hiyo

Kumbuka hii ndoa ni ya mataifa mawili,
Eng Hersi ni Mtanzania na Mobeto ni Mtanzania, Kwa maana hiyo Eng Hersi anatokea umamani hawezi kusimama upande wa Aziz ki

3. Maisha yatakuwaje baada ya ustaa wa Aziz ki kufika Kikomo
Football ni Kazi ya muda mfupi mno
Labda Mobeto kampenda Aziz ki kisa ni staa lakini nina uhakika Aziz hana misimu 3 mbele akiwa katika form hii

4. Kwanini asingefunga ndoa mwisho wa msimu
Ligi inaendelea key players wanafunga ndoa na wachezaji waandamizi wote wako kwenye harusi na tarehe 17 Kuna mchezo dhidi ya Mashujaa, hapa nawaza

Mapenzi mapya yanahitaji muda, huwezi kuwa na mke mpya uwaze vyema kazi ya physical kama football na ufanye katika form nzuri

Washauri wa Aziz ki hawakukaa nae vyema kumpa madini ya msingi nadhani alikutana na machawa wakampoteza

Mchezaji wa Simba Valentine Nouma alifungwa ndoa ligi ikiwa inaendelea na Sasa sijamuona hata bench Nina Imani Simba itamwacha tu
Wanawahi ndoa kabla ya ramadhan
 
Wazazi wenyewe hawapendi, unadhani rahisi eti...unakuta mama mwenyewe ni single mom lakini hakubali kijana wake kuoa single mom..
🤣🤣na hakuna mzazi anataka hii asikwambie mtu!

Yule mama alichomind hakupewa nafasi km mama,hakupewa taarifa mapema Ili ashiriki km mzazi na Yuko sàhihi
Unaolewaje ,kupikea mahari mama mzazi WA mume hayupo?
Ht hamisa mjinga hakutumia akili hapo,au alidangaywa na huyo mumewe.
 
Ni sahihi, ila ndoa za hawa jamaa huwa zinavunjika fasta kama glass ya mchina.... I mean ma staa, tena wale wa asili ya Madina. Kwa hiyo Aziz anaweza kuepa huu msala, cha msingi asizae naye. Na anaweza kuepa na kuhamia ligi nyingine mbali kabisa ambako Mobeto hawezi fika
 
Back
Top Bottom