ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
Familia
Hivi nini hupelekea watu waliokaa kwenye ndoa miaka 20+ au 30+ kuachana?
Huwa ni tabia za zamani ambazo mmoja wao alikuwa akijipa moyo na muda na kuvumilia akidhani tabia itarekebika?
Nina mfano hai wa mama wa familia fulani
Mume amempa talaka mke wake ambaye wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 30
Huyo mzee alikuwa akipelekewa kesi za ndoa za wanafamilia, na alikuwa anakemea sana suala la kuachana
Kuna binti yake aliomba talaka kwa mume wake, huyo mzee akawa mkali kama pilipili
Hakutaka kusikia habari za binti yake kuomba talaka
Binti akalazimishwa kuvumilia, mzee hakutaka kusikia binti anadai talaka
Kwa kulazimisha binti akaondoka kwa mume wake
Mzee akawa mbogo mpaka baadae sana akakubaliana na hali
Sasa leo yeye ndiye ametoa talaka🙌🏼
Nilivyosikia nilishtuka kidogo kwa kuangalia muda ambao ndoa yao imedumu, ila sikuona ajabu sana kwa sababu mimi ni muumini wa amani
Kama hakuna utulivu, amani mchana kweupe naunga mkono anayeamua kukusanya virago
Kilichonifanya niandike ni kwamba nimejiuliza hivi watu wazima wanapokuja kuachana uzeeni, huwa ni makosa mapya au ni makosa ya zamani ambayo mtu alijipa moyo kuvumilia akidhani mwenza atabadilika?
Sioni mantiki ya kuachana uzeeni wakati tayari mmeshaanza kuzeeka na mna wajukuu
Au ndiyo kumaliza uzee salama?
Mie naona watu wakishindwana mapema tu waachane, kila mtu akatafute changamoto mpya
Weekend ya familia na ShesRise_1 ✋️ Upo wapi leo nyumbani na familia au ume chill sehemu 😊