Ndoa ya Miaka 30 Kuishia Talaka: Makosa Mapya au Uvumilivu Uliofika Mwisho?

Familia

Hivi nini hupelekea watu waliokaa kwenye ndoa miaka 20+ au 30+ kuachana?

Huwa ni tabia za zamani ambazo mmoja wao alikuwa akijipa moyo na muda na kuvumilia akidhani tabia itarekebika?

Nina mfano hai wa mama wa familia fulani

Mume amempa talaka mke wake ambaye wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 30

Huyo mzee alikuwa akipelekewa kesi za ndoa za wanafamilia, na alikuwa anakemea sana suala la kuachana

Kuna binti yake aliomba talaka kwa mume wake, huyo mzee akawa mkali kama pilipili

Hakutaka kusikia habari za binti yake kuomba talaka

Binti akalazimishwa kuvumilia, mzee hakutaka kusikia binti anadai talaka
Kwa kulazimisha binti akaondoka kwa mume wake

Mzee akawa mbogo mpaka baadae sana akakubaliana na hali

Sasa leo yeye ndiye ametoa talaka🙌🏼

Nilivyosikia nilishtuka kidogo kwa kuangalia muda ambao ndoa yao imedumu, ila sikuona ajabu sana kwa sababu mimi ni muumini wa amani

Kama hakuna utulivu, amani mchana kweupe naunga mkono anayeamua kukusanya virago

Kilichonifanya niandike ni kwamba nimejiuliza hivi watu wazima wanapokuja kuachana uzeeni, huwa ni makosa mapya au ni makosa ya zamani ambayo mtu alijipa moyo kuvumilia akidhani mwenza atabadilika?

Sioni mantiki ya kuachana uzeeni wakati tayari mmeshaanza kuzeeka na mna wajukuu
Au ndiyo kumaliza uzee salama?

Mie naona watu wakishindwana mapema tu waachane, kila mtu akatafute changamoto mpya

Weekend ya familia na ShesRise_1 ✋️ Upo wapi leo nyumbani na familia au ume chill sehemu 😊
Mkuu nakusalimu,

Kuhusu maada ya Leo, ngoja nianze na maoni yangu binafsi then nitatoa comment kutokana na maoni hayo.

Binafsi naona tunazungumzia ndoa kama kitu Cha lazima au ni jambo la kijamii ambalo Kila mtu linamuhusu. Lakini mimi binafsi naiona ndoa kama kitu private sana, yaani ndoa ni masuala ya watu wawili tuu labda kwa mbali na watoto ndio wanahusika japo kwa udogo sana.

Kwanini nasema ndoa ni mambo ya watu wawili?

Ndoa ni mambo ya watu wawili kwasababu hakuna mtu alishawahi kuwakutanisha hawa watu, hakuna mtu wa zaidi ambaye alishawahi kuwachugulia kwamba huyu apende hiki kwa huyu na huyu apende kile kwa mwenzake, hivyo ndoa ni mambo yanayohusu watu wawili tuu.

Je! Nini chanzo Cha migogoro ya ndoa?

Asilimia kubwa ya chanzo Cha migogoro ya ndoa ni wivu, kusikiliza maneno maneno na mwisho ni tamaa za mali.

Turudi kwenye maada.

Umeuliza chanzo Cha talaka ni makosa mapya au ni uvumilivu uliofika mwisho.

Binafsi naona hapa hakuna majibu sahihi, majibu sahihi wanayo hao wawili walioachana. Kwasababu wao ndio wanajua kitu gani kiliwafanya wakae pamoja miaka 20+, Sasa hiyo sababu ya kuachana kwao haiwezi kuwa na mashiko kuzidi hiyo miaka 20+ walioishi pamoja.

Mwisho niwashauri vijana, usioe kama hujakata tamaa ya maisha. Hakikisha umeshakata tamaa na maisha ndio uoe. Najua nimeongea lugha ngumu hapa lakini ndio ukweli wenyewe "Hakikisha umejikatia tamaa ya maisha ndio uoe au kuolewa"
 
Asante kwa maoni

Sawa mkuu

Kwaninj una shauri hivi ?
 
Eeeh vipi kuhusu wana saikolojia wanaotoa ushauri kwa watu wenye changamoto mbali mbali nao mambo huwarudia?
Wanaambukizwa?

Hiyo dhana yako ipo ki taalamu au ni ile trust me
Masuala ya ndoa pia ushauri wa mahusiano ni hatari sana. Haya mambo huwa wakati mwingine ni ya kiroho zaidi.
 
Wale wasio na watoto ndoa yao itasimama kwa sababu zipi?

Kabla ya ndoa mliishije
Mkuu ndoa inayosimama kwa ajili ya watoto muda wowote kitatokea kitu
Unajua mtoto ni kiunganishi kati ya mama na baba yake. Unless siyo biological father. Nakueleza kuna siku itabidi tu Angalau muongee kuhusu huyo mtoto. Unless Mzazi ha Kali kuhusu mwanae. Nilijitahidi nisiongee na mama wa mwanangu, lakini siku aliposikiwa visu na majambazi, Mbona nilipiga mwenyewe. Achana na mtoto ndugu yangu. Mkizaa kwa kupenda au bahati mbaya, huo ni muunganiko utakaovunjika aidha mtoto afe au Mzazi afe
 
Naelewa ila maana yangu ilikua ndoa inayosimama kwa kigezo cha mtoto ni hatari sana

Kwa sababu hakuna mapenzi
Hakuna kuhurumiana
 
Asante kwa maoni
🤝
Sawa mkuu
🤝
Kwaninj una shauri hivi ?
Unapochagua mtu wa kuishi nae, hakikisha hutatamani vitu vingine nje ya yule ulieweka nae nadhiri.

Binafsi naamini kwamba kila mtu hufikia peak ya kufanya jambo/mambo hivyo unapotaka kuingia kwenye ndoa hakikisha umeshafikia peak ya vitu vingine. Huku ndiko nazungumzia kukata tamaa.

Naipenda biblia kwangu ni kitabu Bora sana. Kwenye biblia Kuna mstari unasema "Nyinyi msipokuwa kama watoto wadogo bhasi hamtauona ufalme wa Mungu". Nikaanza kujifunza kuhusu watoto wadogo.

Kikubwa nilichojifunza kuhusu watoto wadogo ni hiki "Kid's are very flexible"

Been flexible is like dead but alive.
 
Bado sijakuelewa vizuri nataka mantiki ya wewe kusema aoe au kuolewa kijana aliekata tamaa

Sasa aliekata tamaa na nini ?
 
Duuuh! Jamaa🤨🤨🤨

Katia tamaa vishawishi na mambo mengine mengine.

Jichagulie kijana wako barobaro/ Binti mrembo alafu fanyeni maamuzi ya kwamba sisi tukigombana bhasi wa kutusuluhisha ni sisi wenyewe.

Mmoja akimchoka mwenzake bhasi aende kabatini kulamba glucose ili apate nguvu ya kumpenda mwenzake.

Mkikwazana hakikisheni mnabembelezana mpaka mnapelekeana moto, hakuna mambo ya kukomoana na kunyimana unyumba.

Mwisho achani kuvumiliana bali kama Kuna tabia mwenzako haipendi hakikisha imemtoka au nawewe umekua na hiyo tabia.

Mpaka hapa nafikiri nimeeleweka mrembo.
 
Hizi akili zako hizi 😅😅
Haya ushauri wako nauchukua
 
Back
Top Bottom