Ndoa ya mke mmoja ni maagizo potofu ya mwanadamu, sio Mungu. Ukweli huu hapa

Ndoa ya mke mmoja ni maagizo potofu ya mwanadamu, sio Mungu. Ukweli huu hapa

Kuoa wanawake wengi sio kudio la Mungu ni matakwa ya wanadamu na tamaa zao hata hao mitume waliokuwa na mitaala waliishia kujuta tu! Ndio maana yesu kwenye agano jipya anasisitiza kuoa mke mmoja na sio vinginevyo! Injili maana yake ni habari njema Kwa watu wote sio wazungu Wala waafrika Wala waislamu Wala wabudha, hata hao waislamu wenye wake wengi wanajuta na mwislamu anaejitambua hawezi kuwa na wanawake wengi!! Suala la kuoa sio la Kila mtu Kuna watu hawapaswi kuoa au kuolewa!
Biblia imechezewa mno tuje kwenye Quran je inaeleza nini juu ya wake wengi?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuchelewa. Kuoa wake wengi ninaamini ni sawa kwa utamaduni wa mababu zangu na kwa dini zote za asili ya Abraham maana hakuna ilipozuiwa. Nitakuwa mwendawazimu sana nimezalizaliwa na mke wa pili kwa baba na kisha nimezeshwe dhana ya uongo tu na mchungaji au pastor kuwa mke wa pili ni kosa na hivyo nami nijione haramu bila hata kutafiti.

Moja, nimefanya utafiti nimegundua dini haizuii na mwanzo wa jambo hilo ni tamaduni ya Urumi (Roman Empire) ambapo wao utamaduni wao ulikuwa mke mmoja tu. Hivyo sioni haja ya kuamini utamaduni wa Kirumi na kuacha utamaduni wa mwafrika.

Pili, kama Mungu anaamini nyumba ndogo ni haramu asingeruhusu Yesu azaliwe katika uanadamu wake atokee nyumba ndogo.

Historia ya dunia hii nimejaribu sana kuisoma kila sehemu. Mwanzilishi wa jambo hili kuliweka kwenye sheria ya kirumi kabisa na kuhakikisha siyo utamaduni pekee bali sasa liko kwenye sheria ya kirumi dhama hizo anaitwa emperor Augustus! Na kwa msaada tu huyu ni mtoto wa emperor Julius Ceasar (mnaita Julius Kaisari).

Wakati mitume wa yesu wanakimbia Rome baada ya yesu kufa walikuta hii sheria ni kali sana, mke mmoja na mume mmoja. Na wakristo wanaanza kuuliza vipi hili mbona linakingana na torati mnasemaje? Soma kitabu cha Tito ambapo wanaorodheshwa ambao wamezuiwa kuoa zaidi ya mke mmoja. Tena kinasema kabisa kwamba "wafuatao wawe waume wa mke mmoja". Sasa wametajwa. Sisis katika hao waliotajwa hatumo, inakuwaje mchungaji atumezeshe hiyo imani tuikubali?

USHAURI WANGU
Nawashauri wanaume wenye uwezo wa kuoa mke zaidi ya mmoja wafanye hivyo mara moja kwani hakuna kifungu cha biblia hata kimoja kinachowazuia kufanya hivyo. Watu waoe mitala wazae na kuijaza dunia. Hili ndilo agizo la Mungu Baba Mwenyezi. Maagizo mengine yoyote yale ni ubatili kwani yametokana na utashi wa wanadamu!
Hata kuoa wanne ni maagizo potofu ya binadamu. Ima usioe uishi kimalaya au uoe hata milioni shauri yako.
 
Kwani dunia hii bado kuna wanaume wenzetu wana mke mmoja tu ?

Wachunguzwe watakuwa na tezi dume
 
Mkuu hujasoma maandiko vizuri, huijui biblia na desturi za wayahudi!

Kwa taarifa yako mke wa kwanza wa Adam alikuwa Lilith, Eva ni mke wa pili baada ya Lilith.

Na pia Adam sio binadamu wa kwanza kuumbwa.

Adam ni mtu wa kwanza kuumbwa kwa udongo shambani Eden.
Chochote amacho hakipo kwenye Kitabu kitakatifu Biblia ni "UONGO".
 
Back
Top Bottom