Ndoa zimekuwaje? Kuna Video inatrend leo Mume akimkaba mkewe na kutaka kumuua live barabarani

Ndoa zimekuwaje? Kuna Video inatrend leo Mume akimkaba mkewe na kutaka kumuua live barabarani

Hao watu waliokuwa wanarekodi tu na kumbembeleza huyo mwanaume nao ni kama wapumbavu tu. Katika hali ya kawaida huyo mwanaume alipaswa kushambuliwa kwa fimbo na mawe, raia hawakupaswa kucheka na huyo mwanaume, ndoa sio kichaka cha kufichia ukatili.
 
Biashara ikiwa ngumu, binadamu anatafuta ufumbuzi ,anaishinda

Kazini mazingira magumu kweli ya kazi , binadamu anatafuta ufumbuzi ,anaishinda

Maisha hata yawe magumu vipi, binadamu anatafuta ufumbuzi ,anaishinda

Lakini mtego wa kwenye ndoa ,changamoto kidogo, binadamu anawaza kukimbia.Kibaya kishazaa,anaandaa mtoto wa mtaani akawe changudoa au shoga.
Kila mtoto wa mtaani ni shoga na changudoa? Au kila shoga na changudoa ni mtoto wa mtaani??
 
Kitu Wanawake hawajui ni kadri mwanaume anapokupigia simu afu haupokei ndivyo inavyozidi kupandisha hasira mwanaume .

Najua wanawake wengi huona bora asipokee simu kwa kuepuka kufokewa kwenye simu na kujipa moyo kuwa akifika nyumbani watayajenga . Lakin wasichojua sisi wanaume hufafanua hiyo ni kama dharau na kuamini kile tunachokiamini kwenye akili yetu kwa wakati huo kama vile ananisariti muda huu ndyo maana hapokei simu yangu .

Tisa kumi . Unaweza kujiuliza ni nini kimepelekea huyu mwanaume kuhisi kusalitiwa ?? Kwanini hajawaza labda mkewe alikuwa mbali na simu au alikuwa simu kaiweka silent mode ??.

Hapa kwa uzoefu wangu . Jibu ni kuwa huyu jamaa huende huko nyuma alishawahi fumania mesegi au maongezi fulani ya mkewe ambayo yaliashiria usaliti na kuamua kumsamehe mkewe lakini toka hapo amekuwa hamuamini tenaaa mkewe na ndiyo maana hata simu iliposhindwa kupokelewa moja kwa moja yeye kawaza mkewe alikuwa kaenda kumsaliti tu na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom