Kitu Wanawake hawajui ni kadri mwanaume anapokupigia simu afu haupokei ndivyo inavyozidi kupandisha hasira mwanaume .
Najua wanawake wengi huona bora asipokee simu kwa kuepuka kufokewa kwenye simu na kujipa moyo kuwa akifika nyumbani watayajenga . Lakin wasichojua sisi wanaume hufafanua hiyo ni kama dharau na kuamini kile tunachokiamini kwenye akili yetu kwa wakati huo kama vile ananisariti muda huu ndyo maana hapokei simu yangu .
Tisa kumi . Unaweza kujiuliza ni nini kimepelekea huyu mwanaume kuhisi kusalitiwa ?? Kwanini hajawaza labda mkewe alikuwa mbali na simu au alikuwa simu kaiweka silent mode ??.
Hapa kwa uzoefu wangu . Jibu ni kuwa huyu jamaa huende huko nyuma alishawahi fumania mesegi au maongezi fulani ya mkewe ambayo yaliashiria usaliti na kuamua kumsamehe mkewe lakini toka hapo amekuwa hamuamini tenaaa mkewe na ndiyo maana hata simu iliposhindwa kupokelewa moja kwa moja yeye kawaza mkewe alikuwa kaenda kumsaliti tu na si vinginevyo.