Ndoto ni matokeo ya ubongo kupumzika, hazina maana yeyote zipuuzeni

Sasa wewe uliyeandika ndoto ZIPUUZWE tu hukujua kama kuna watu wanaota na ndoto zao huwa kweli!? Acha KUKURUPUKA.
Mnaoota na kuamini ktk ndoto mnacheza na probability of events hamna utofauti na mtu anaye bet
 
Tuondolee upumbavu wako hapa. Sijui unaishi dunia gani ambayo hujawahi kusikia kuna watu wanaota na walichokiota kinatokea. Acha ubishi wa kipumbavu.
Mnaoota na kuamini ktk ndoto mnacheza na probability of events hamna utofauti na mtu anaye bet
 
Tuondolee upumbavu wako hapa. Sijui unaishi dunia gani ambayo hujawahi kusikia kuna watu wanaota na walichokiota kinatokea. Acha ubishi wa kipumbavu.
Sawa mkuuπŸ™
 
Labda nikuulize swali jepesi nikihusishanisha na maelezo yako ya usasa na teknolojia. Hivi jua au mwezi vimeshawahi kubadirika ukilinganisha na usasa na teknolojia zenu unazoziongelea? Je mbona husemi jua limepita na wakati au nguvu yake imepungu ukilinganisha na nyakati.

Mwaka 2017 niliandika ndoto niliyoiona mwaka huo kuhusu Nchi na Rais wa nchi hii. Watu walinikebehi na kusema maneno Kama yako lakini mwaka 2021 Ile ndoto ilithibitishwa. Kwa hiyo Kama hujui kubali kujifunza ukiachana na kukaza shingo yako ukavunjika. Mungu yupo hai na Wala hajafa. Amefanya mengi ya kutisha Sana. Je wewe unayeandika haya mpaka Leo na umri ulionao umefanya nini hata kwenye mtaa wako? Ukashindwa hata kutafakari vitu vidogo tu utaweza kutafakari mambo makubwa?
 
Unatumia hoja za kidini kujibu hoja ya kisayansi, ahsante kwa maoni yako mkuu
 
hadi sasa bjnadamu anatumia asilimia ambazo hazifiki 10 ya uwezo wa ubongo wake. na ndoto ni tafsiri sahihi ya hili.
 
Umezungumzia ndoto kuwa Ni kutokana na sababu ulizozieleza vipi kuhusu kuoneshwa vitu vinavyokuja au vilivyopita ukiwa macho tu. Sizungumzii kitu ambacho nasimuliwa Bali huwa naona mwenyewe na ninpewa maagizo ya kufanya. Na muda mwingine Kuna vitu naambiwa nikavifanyie utafiti wa kibinadamu na majibu nayapata kulingana na kile Mungu ameniambia. Na si kuona tu ninasema naye Kila Mara. Na si peke yangu mfano kwenye familia yangu Ni Mimi, mke wangu na watoto. Humu Jf naamini pia wapo wengi tu. Mungu yupo Wala si utani.
 
Unatumia hoja za kidini kujibu hoja ya kisayansi, ahsante kwa maoni yako mkuu
Sayansi inahitaji facts, na facts unazipataje?

Pitia kwenye akaunti yangu utaona post ya mwaka 2017 na ulinganishe na tukio la kifo Cha Magufuli

Kwa Mungu Kuna facts na siyo maigizo. Mtu akiwa anaumwa akapime hospitali na baada ya hapo Mungu amponye unaruhusiwa kwenda kumpima. Na siyo maigizo ya baadhi ya watumishi.
 
Tatizo linaanzia hapo kwenye Imani
 
Mkuu nina maswali mawili naomba ufafanuzi,
1. Unaweza kunielezea mtu asiyeona/kipofu ndoto zao huwa katika mfumo gani tuseme alizaliwa hivyo
2. Je kwa watoto wachanga mara nyingi wakiwa kwenye ndoto hutabasamu as if wameona kitu cha kufarahisha kwenye ndoto, Unaweza kuelezea hii inakuaje? Ukizingatia hawajafikia umri wa kuona na kuweza ku interpret jambo zuri au baya.
 
Ahsante kwa maswali mazuri
Mkuu nina maswali mawili naomba ufafanuzi,
1. Unaweza kunielezea mtu asiyeona/kipofu ndoto zao huwa katika mfumo gani tuseme alizaliwa hivyo
Kwanza kabisa ili uote kitu lazima kuwepo na kumbu kumbu za taarifa mbali mbali kwenye ubongo wako ( short term and long term memmory).
Hizi kumbu kumbu huhifadhiwa kwenye ubongo wa kati na ubongo wa mbele,

Taarifa zinazopakiwa kwenye ubongo hukusanywa kwa njia kuu 5
  • kuona
  • kusikia
  • Kunusa
  • Kuonja
  • Na kuhisi kwa ngozi au mitetemo
HIvyo basi mtu aliyezaliwa akiwa kipofu atapakia taarifa kwenye ubongo kwa njia nne tu, ambazo ni kusikia, kunusa, kuonja na kuhisi (mfano kumtambua mtu kwa kumshika, kutambua sehemu au njia inayoelekea chumbani kwa kugusa na fimbo n.k)

Ndoto zake zitakuwa ni za kuota anaambiwa jambo flani, kuota anatembea kwa fimbo kakutana na kitu flani, kuota amekunywa kinywaji flani kizuri, kuota amewasikia watu flani wakiongea jambo flani au kuota jambo lolote la hatari kama vile kudondoma, kuungua, ajari n.k isipokuwa taarifa zinazohusisha kuona tu ndio hataota
2. Je kwa watoto wachanga mara nyingi wakiwa kwenye ndoto hutabasamu as if wameona kitu cha kufarahisha kwenye ndoto, Unaweza kuelezea hii inakuaje? Ukizingatia hawajafikia umri wa kuona na kuweza ku interpret jambo zuri au baya.
Kwenye ubongo kuna sehemu inayohusika na kuiga kwa mtindo wa kioo, yaani ukimuoma mtu flani anafanya jambo flani na wewe unajikuta umeiga au kufanya kama lilivyo mfano mtu akipiga miayo na wewe unaweza ukajikuta tu unapiga miayo automatic,

Hivyo hivyo kwa mzazi akitabasamu mbele ya mtoto basi na mtoto anatabasamu automatic kwa hiyo anakuwa amejifunza kwa mtindo huo wa kioo.

Sijui unanielewa mkuu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…