Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Wadau naomba kujua hii ndoto ina maana gani

Mara ya Kwanza niliota napaa angani nikawa najisikia vizuri sana maana nilikuwa naona watu kwa chini wakinishangaa navyopaa angani!

Nikazurura zangu weee wakati wa kutua chini nikatua fresh bila tabu

Haikupita mwezi nikaota tena ndoto ile ile tena mara mbili kwa usiku mmoja. Mara hii nlikuwa nakwepa nyaya za umeme vibaya mno. Nakutana na nyaya za high voltage lakini kwa njia ya ajabu nikawa nazikwepa bila tabu. Na mwisho wa siku nikatua Kama kawaida.

Naombeni tafsiri wadau
 
Hongera mkuu..usha unganishwa kwenye international transport ila bado upo kwenye training [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi kuna ndoto naota nikipita katika maji machafu au nikivuka mto wenye maji machafu na huwa sijawahi kufanikiwa kupanda kingo za mto nikaenda ngambo ya pili au naota nikitembea pembezoni mwa mto mkubwa wenye maji mengi yanayoenda kasi sasa nikishaota hiyo ndoto huwa hazipiti siku zaidi ya tatu bila kupata habari za msiba wa mtu yeyote ninayemfahamu. Nikishaota huwa nadikilizia kabisa. Nina kama miaka zaidi ya ishirini ya uzoefu wa ndoto hii. NAICHUKIA SANA. SIJUI NITAIEPUKA VIPI
 
Ukiota ndoto mbaya unafuta kwa damu ya Yesu. Unaona mapema ili uzuie yasitokee hayo mabaya. Isaya 7:7

Usisahau kuanza na toba
 
Naomba msaada wa ndoto hii ambayo nimeota usiku wa kuamkia leo,nimeota nakula chakula,kuna,mwanamke simjui amekaa pembeni yangu ananipa chakula kiko kwenye sahani,nikawa na wasiwasi na hicho chakula lakini cha ajabu ninaendelea kula mpaka ninamaliza akanipa tena sahani nyigine,ila nilionyesha dalili yakutokukikubali hicho chakula laikini alikuwa akinisisitizia kuwa kiko salama niendelee kukila,then baada ya muda nilishtuka na nikaingia kwenye maombi makali ya kukemea,kama ni roho chafu au nimeunganishwa na maagano yaniepuke...
Kuna mahali nilisoma wakasema kwamba ukiota unakula au unalishwa sio dalili nzuri, sio mtaalam wa ndoto ila ngoja akina Mshana Jr Divine Waje hapa watoe neno.
 
Hakikisha ukiota ndoto yeyote kabla hujaituma humu hakikisha unombea hiyo ndoto kama ni mbaya futa kama huelewi pia mwambie Roho Mtakatifu nisaidie kuombea hii ndoto. Utaomba na usikatishe ndan yako hadi aman imekurejea hata ukii ikumbuka ile ndoto haikupi tabu tena.
Nyunyiza damu ya Yesu ktk hiyo ndoto ikanene mema, hivyo itapangua kika kitu omba tu kuwa na uhakika kuwa Mungu yupo hapo anakusikia

Mwambie Mungu naileta hii ndoto nisaidie kama kuna kibaya nakifuta kwa damu ya Yesu isaya 7:7
Kama kizuri ebrania 12:24 damu ya Yesu ikanene mema.

Na mengine utayaongezea ktk kuomba lakin hakikisha unaanza na toba usijihesabia haki kwa Mungu.

Kama kuna kitu kimekuingia utang'oa pando ndan yako
Kila pando asilo lipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa

Nyunyiza damu ya Yesu ndani yako ikapite inene mema, na kama kuna sumu ifute
Kama kuna madhara iponye palipo haribika

Na mahali mlango uliofunguka uzibwe kwa damu ya Yesu. Ili ulinzi ukae hapo
Kwa uchache kuna mengi Mungu , Roho Mtakatifu atawaongezea
 
Nimeota nimeomba kubadirishiwa kituo cha kazi, nikaulizwa utaweza? Nikasema nitaweza.

Basi nikabadirishiwa kituo na kupelekwa katika msitu flani wa asili ( kiuhalisia mimi ni afisa misitu). Kazi yangu iwe kufanya doria ndani ya huo msitu.

Basi nikaanza kuingia na kuzunguka katika hiyo hifadhi, ndani kuna sehemu nikakuta kuku ana vifaranga viwili kutembea mbele kidogo nikakuta tena kuku mwingine kalalia mayai na vifaranga viwili vimeanguliwa tayari. Mayai yaliyobaki yanalaliwa yalikuwa kama matano hivi.

Tena kuna sehemu nikakuta kama kishimo kidogo ndani kuna nyoka sina uhakika kama niliona nyoka au nilihisi huna nyoka hivyo nikaanza kukiharibu hicho kishimo.

Ghafla nikajikuta nipo na bosi wangu msaidizi ( kiuhalisia amehamishwa muda sio mrefu). Huyo bosi msaidizi amenipakia katika pikipiki na tupo tunafukuzia basi kubwa la abiria ( kama ya mkoani) ambalo limepakia mkaa wa magendo mbele kabisa ya basi.

Pikipiki ilikimbizwa tukaliovateki lile basi ili tukalizuie mbele. Tukafika kituo flani tukalitegea hapo ambapo lilifika tukalikagua halikuwa na mkaa, Yule bosi msaidizi akaniambia itakuwa wameushusha ule mzigo na kuuficha sehemu na itabidi kesho asubuhi na mapema niwahi maeneo yale ili nilicheki lile basi kama limepakia mkaa au laa.

Ghafla nikaona tumeenda kama bar au grocery tukawakuta wafanyakazi wengine wapo kunywa pale, walikuwa wakinywa bia.

Yule bosi msaidizi niliyekuwa nae akaniambia itabidi umnunulie Lupembe bia, ( huyo Lupembe ni bosi msaidizi mpya aliyehamishiwa hapa kazini baada ya ambaye nimemuelezea awali kuhamishwa).

Basi nikawa nimetoa elfu kumi namuita Lupembe ( bosi msaidizi mpya ) ambaye kwa muda huo alikuwa nje,nikamuita alivyofika namwambia achukue bia , yeye akajimiminia katika glasi yake bia ya mtu mwingine ambayo ilikuwa mezani. Nikamwambia sio hiyo akasema basi nishamimina, akafika mwenye kinywaji ambacho kimemiminwa ( nae ni mfanyakazi mwenzetu) akawa anamwambia itabidi unilipe kinywaji ulichomimina lakini ilikuwa ni utani kumwambia hivyo tukawa wote tunacheka pale.

Naomba tafsiri ya hii ndoto ndugu.
 
Soma mwanzo 28:10-21

Halafu uonishe na hicho ulicho kiandika
Habari za Asubuhi mpendwa.mimi kuna jamaa yangu tulikuwa Marafiki sana yaani maisha yetu ni kama mtu na kaka .lkn kuna ilikuja kutokea tukawa maadui wakubwa sana na yeye ndie aliyejitenga Nami. siku za hivi karibuni nimeota nimekutana nae maeneo fulani akiwa na mchepuko wake akanipa pesa tena dola kiasi fulani lkn ikawa nilipokuwa nazihesabu zikawa zinazidi idadi ya pesa alizonipa .pia alinipa koti lake na kofia flani kama ina hedfon nikawa naogopa kuivaa Ile kofia na yote ni Kwa sbb ya mambo ambayo nilishaisi juu yake Kwa hiyo ni mtu nisiyemuamini kabisa .je? ndoto hii inamaanisha nini.niyashukuru kama nitajibiwa na Mungu awabariki
 
1: Ndoto Unazozipata kwa Sababu ya Kushiba, Maneno mengi uliyoongea au kumbukumbu ya mambo yaliyopita.
Ndoto hizi ni asili, Kila mwanadamu anaziota. Mtu akikwambia huwa haoti ujue ni Muongo.

Mwenye Hekima Suleiman Anaandika
" Kadiri mtu anavyohangaika zaidi, ndivyo atakavyoota ndoto;
sauti ya mpumbavu ni maneno mengi." Muhubiri 5:3
Hapa hakuna uhusiano na mapepo, majini wala mashetani.

2:Ndoto Zinazoletwa na Mashetani.
Hii inaushahidi wa kiuzoefu tu. Leo utakuwa umesikia mtu kalala, kaota anafanywa mapenzi na anapoamka asubuhi anakuta amemwagiwa hadi mbegu za kiume huku alikuwa peke yake kitandani.
Wapo wanaooteshwa na kuamka usiku kwenda kulima,kufanya kazi na wanaamka wamechoka, ikifika asubuhi anaweza kukumbuka kama alikuwa anaota anafanya kazi kumbe kazi ilikuwa halisi.

Wapo wanaoamshwa kichawi, wanafanyishwa matukio ya ajabu akiwa katika hali ya ndoto.
(Hapa wenye ukina zaid wanaweza kufafanua ila ni vitu halisi havihitaji kuamini Mungu/Shetani Yupo au hayupo)
cc Bilionea Asigwa Mshana Jr

Kwa watu wanaomuamini Yesu, Hutokaa ukutwe na mambo haya labda kama unaamini katika viwango vya unafiki au unachanganya dini na uchawi/ulozi.

3:Ndoto Zinazoletwa na Mungu.
Hizi Mungu mwenyewe anasema "Akiwepo nabii kati yenu, Nitasema naye kwa njia ya NDOTO" Hesabu 12:6
Lakini Sio tu nabii, hata watu wa kawaida, hata wasio watu wa Kitabu, hata viongozi.
Alisema kwa njia ya ndoto na Farao, Nebuchadneza, Yule mfungwa gerezani pamoja na Yesufu.

SIFA ZA NDOTO HIZI
1: Ziko wazi, hazina kona kona au kubahatishabahatisha.
2:Lazima zitimie.
3:Hazikutegemei wewe kuifanya itimiie.
4:Huwa haziji mara kwa mara.

MWIISHO
Nimeandika haya ili kusaidia watu ambao wanaota nndoto za kawaida tu, ambazo ukikaa mwenyewe ukafikiri kwa nini umeota hilo utagundua tukio lililopita au mazungumzo yaliyopita ndio chanzo cha ndoto lakini wameibuka watu ambao wao wanaamini kila ndoto ni matokeo ya majini. Kila ndoto lazima iwe na tafsiri, Kila ndoto ni ya Mungu au Ya shetani.

Wajuvi zaidi wa mambo haya wanaweza kuja kushuka nondo zaidi.
 
mwanzoni mwa wiki hii nilimuota mwanangu wa nguvu ambae amestangulia miaka minne iliyopita, ktk hiyo ndoto ilikuwa ni kama sherehe flani ambayo mimi nilialikwa tuu, nilipofika pale nilikuta watu wengi nisiowafahamu, ila nilimfahamu jamaa yangu ambae tayari ni marehemu, dah nilistuka, nikamwita kwa jina, jamaa akanipita kama hanifahamu, ila alienda pembeni hivi akaniita kwa ishara, nilipomfikia nikamuuliza G...ni wewe kweli? akanijibu yap ni mimi, jamaa alikuwa smart kavaa suti moja nyeusi iliyomkaa vyema..ikabidi nimuulize kaka we si umekufa? akanijibu mwanangu we acha tu, yah mimi nimekufa ila tuyaache hayo, vipi bi bimkubwa anaendeleaje? akimaanisha mama yangu, nikamwambia hajambo ila man kwanini upo hapa? akasema hapa waliopo karibia wote wameshakufa ila wapo watu watatu ambao mpo hai na hata hawa waliokufa si unawaona wapo hai? ilinibidi nikurupuke tuu, ndoto gani tena za namna hii? sasa kilichokuja nikumbusha hii ndoto ni hiyo siku iliyofuata ikaingia notification ya kuwatakia kheri za kuzaliwa bandugu kule facebook, jina la mwanangu ambaye ndio huyo Marehemu lilikuwa la kwanza....nilijisikia vibaya kwa kwali....siamini ktk ndoto ila...ndo hivyo
 
ndoto za misiba mara nyingi hubeba tafsiri za heri,ila ndoto zisizo na maana huitwa ndoto za mang'amung'amu.upo sahihi kwa asilimia zaidi ya themanini.ndoto hizi huotwa mwanaadamu akiwa na mawazo,malaria au mvurugano fulani ubongoni.ila shetani na mungu ndio hutawala ndoto za mja.
 
mwanzoni mwa wiki hii nilimuota mwanangu wa nguvu ambae amestangulia miaka minne iliyopita, ktk hiyo ndoto ilikuwa ni kama sherehe flani ambayo mimi nilialikwa tuu, nilipofika pale nilikuta watu wengi nisiowafahamu, ila nilimfahamu jamaa yangu ambae tayari ni marehemu, dah nilistuka, nikamwita kwa jina, jamaa akanipita kama hanifahamu, ila alienda pembeni hivi akaniita kwa ishara, nilipomfikia nikamuuliza G...ni wewe kweli? akanijibu yap ni mimi, jamaa alikuwa smart kavaa suti moja nyeusi iliyomkaa vyema..ikabidi nimuulize kaka we si umekufa? akanijibu mwanangu we acha tu, yah mimi nimekufa ila tuyaache hayo, vipi bi bimkubwa anaendeleaje? akimaanisha mama yangu, nikamwambia hajambo ila man kwanini upo hapa? akasema hapa waliopo karibia wote wameshakufa ila wapo watu watatu ambao mpo hai na hata hawa waliokufa si unawaona wapo hai? ilinibidi nikurupuke tuu, ndoto gani tena za namna hii? sasa kilichokuja nikumbusha hii ndoto ni hiyo siku iliyofuata ikaingia notification ya kuwatakia kheri za kuzaliwa bandugu kule facebook, jina la mwanangu ambaye ndio huyo Marehemu lilikuwa la kwanza....nilijisikia vibaya kwa kwali....siamini ktk ndoto ila...ndo hivyo
duuh pole sana
 
sio kweli.
kwa mfano hiyo no. 2, mwanaume huwa anaota anafanya mapenzi na kujimwagia shahawa kutokana na kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi/kuzitoa hivyo inafikia kipindi zinatoka zenyewe.
 
Umedanganya Sana Wewe Mpuuzi!
Hiyo Ya Kuota unafanya mapenzi Umedanganya Sana.
Ni Mambo Ya Kisayansi Zaidi, Sio Unakuja Hapa "Unaropoka" Tu "Matapishi" Yako Hapa! Acha Wehu!
 
Back
Top Bottom