Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Simama ktk mambo mazito, utachizika au utapotea hutaonekana! Waulize wazazi wako, ndoto hizi huota mtoto wa dawa! Yani wazazi wako walitembea kwa waganga ili wapate mtoto. Sasa mganga akikupa mtoto huweka bispo fulano. ipo siku vinadai kafara. Au unatakiwa uludi ulikotolewa na njia ni mbili tu. Uchizi upotee! Au upotee tu. Ili upone lazima wazazi wakavunje agano hasa mama, sababu siku alikuzaa damu ya kuzaliwa kwako iliwekewa agano fulani, kwa kutamka maneno au tambiko. Wazazi wakatubu .utapona.
 
Ndoto ya kwanza kuna uliyoyafanya unatakiwa utubu. Unakumbuka kwenye bible walivaa magunia na kulamba chumvi na Mungu amekupeleka mpaka kanisani unapotakiwa kufanya toba na baada ya toba utakuwa sawa na wenzako.


Ndoto ya pili ni destiny yako. Wewe ndiye unamfahamu unataka kupelekea wapi. Usikubali mtu akuendeshe. Safari yako itakuwa na milima na manonde na utapitia sehemu hatari sana.

Ya tatu sijuielewa kwa kweli.
 
Naomba kujua kati ya haya:-

Taaluma yako.
Umri wako.
Je, una wazazi wote wawili..?
 
Kunyaa unyee wewe then mwingine aje kukutawaza? si umeota wewe au, we ndio utuambie tafsiri yake
dah, sikutegemea kupokea matusi ya aina hiyo, hata sijui nimekukosea nini? kwanini maneno makali kama hayo yamekutoka mkuu? unajiona upo normal kweli? hii ni threat ya uhuru wa kupost au kuipotezea hata hatujabishana wewe umerusha tusi kama tunafahamiana vile! maisha magumu ndo yanafanya watz kuwa na hasira hivi bila hata sababu?hahahaha Pole, lakini nimekusamehe bure!
 
Simama ktk mambo mazito, utachizika au utapotea hutaonekana! Waulize wazazi wako, ndoto hizi huota mtoto wa dawa! Yani wazazi wako walitembea kwa waganga ili wapate mtoto. Sasa mganga akikupa mtoto huweka bispo fulano. ipo siku vinadai kafara. Au unatakiwa uludi ulikotolewa na njia ni mbili tu. Uchizi upotee! Au upotee tu. Ili upone lazima wazazi wakavunje agano hasa mama, sababu siku alikuzaa damu ya kuzaliwa kwako iliwekewa agano fulani, kwa kutamka maneno au tambiko. Wazazi wakatubu .utapona.
hahaha, tafsiri yako naikataa Kwa Jina la Yesu Kristo: sio mara yangu ya kwanza kuota ndoto, na huwa zinatokea baadaye either ushindi au kushindwa. sema tu leo sijafunuliwa na Roho wa Mungu na hapa nilipo nipo kwenye maombi ya kufunga siku tatu hadi Mungu aingilie kati, ndio huwa ni desturi yangu, na siku zote huwa nashinda.

mwaka jana ilikuwa nipate dili moja kubwa sana la hela nyingi sana, kuna ndoto ambayo niliiota kuwa kuna mtu amekuja kuichukua hiyo kazi yangu na mazingira yote nilionyeshwa, nilionyeshwa na Mungu, na ilitokea hivyohivyo. Kwa utukufu wa Jina lake sikujua mabaya gani yangenipata ningepata ile kazi na Mungu aliamua kuniepusha bora nisipate zile hela ili nipote. nilimshukuru Mungu kwasababu niliyokuja kuyapata baadaye ni bora kuliko yale niliyokuwa napigania. vilevile, kwa kifupi mimi ni Mkristo, hata kama nilizaliwa vijijini kwenye mambo ya kienyeji sana lakini nimeokoka, maagano yooote ya wachawi waganga na washirikina etc niliyavunja nikaingia agano la Damu ya Yesu, Damu ya Yesu Kristo iliyo kuu kuliko damu ya wanyama na Habili. Hii ni Damu inayonena mema juu ya maisha yetu, ni Damu inayofuta maagano yoote ya mashetani, na ndio agano jipya ambalo Mungu badala ya kutumia makafara ya wanyama aliamua kutumia kafara la Yesu Kristo once and for all litakalokuwa ukombozi wa roho mwili na nafsi zetu. hivyo kwenye hayo maagano unayoongelea kwa upande wangu simu....sikatai tu ni kwamba ninaishi na Mungu moyoni na upo udhihirisho huo. ninaenenda kiroho ndio maana hata hizi ndoto nimeziona kiroho na kuna msukumo wa kiroho kufanya kitu....na kwa kifupi ni kwamba nimeirusha tu hapa ili kushare kitu na siku matokeo yakitoka nitaleta thread hapa kuwaambia yaliyojiri ili iwe fundisho na kwa wengine. hivyo hata tafsiri nyingi mtakazotoa hapa sio zote naziamini, zile nitakazofunuliwa na Roho kuwa ndizo ndizo nitakazoziamini...maana najua hapa tumechanganyikana sana kuna wengine wasoma nyota, mashetani na hata majini yapo humuhumu kwenye internet.
 
namshukuru Mungu nimepata tafsiri ya ndoto zangu zote. kwa kifupi, ndoto iliyonitisha kuliko zote ilikuwa ile nimevaa na nimeelekea mbele za watu wenzangu wamevaa nguo na viatu mimi nimevaa nguo lakini sina viatu natembea hivyohivyo....maana ya ile ndoto ni kwamba nilikuwa nimepungua nguvu za kiroho, protection ilipungua kwangu sikuwa na ulinzi wa kutosha hivyo ninahitaji kumtafuta Mungu zaidi kutokana na mazingira niliyomo sasa kuna negative forces zinazohitaji uwepo wa Mungu zaidi kwaajili ya kunipigania na kupigania mambo yangu. ilipoungana na ule mlima nilipokuwa napanda na kuona nguvu zimepungua kumalizia robo ya mlima kufika kileleni, ndio hivyohivyo, nahitaji nguvu za ulinzi zaidi. matumaini yangu kushikilia lile taruma la reli na kua nitafanikiwa ni kwamba katika mambo yangu ninayotafuta nitafanikiwa lakini nahitaji kumtafuta Mungu kwa bidii sana ili uwepo wa Mungu uwe kwa wingi maishani mwangu na ndio utakuwa ulinzi wangu negative forces hazitaweza kunifikia kwasababu nitakuwa nimezungukwa na nguvu za Mungu. kwasasa nguvu za Mungu au uwepo wa Mungu umepungua hivyo nahitaji kutafuta zaidi uso wa Mungu.

kama ilivyo principle, the more you read the word of God, the more you spend more time in prayer and fasting, the more seek the face of God in various manners....ndivyo nguvu za Mungu nyingi zinakuja juu yako na ndivyo Mungu anapokuw akaribu sana na wewe.

the more unavyotegea katika maombi, the more unavyotegea kusoma Neno la Mungu, the more unavyokkuwa haumtafuti Mungu,....the more utakua mbali na Mungu na nguvu zake zitapungua kwako.

Neno la Mungu linasema "nani mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa mioyo yenu yote", na ukimtafuta Mungu kwa bidii atakua karibu nawe, unapopunguza kumtafuta ndivyo unavyopiga hatua moja baada ya nyingine nyumba away from him...

Namshukuru Mungu kwa hilo, yanipasa kukazana sasa nimtafute Mungu, pale palipopungua pajazwe na ulinzi wa Mungu uwe intact na mambo yangu yaende vizuri. ni matumaini/imani yangu kwamba muda si mrefu nitakuja hapa siku moja kutoa ushuhuda wa jinsi matokeo ya ndoto hii yalivyo kama yamebadilika au la, na yote yatakuwa kwa utukufu wa Mungu. Katika Jina la Yesu Kristo!
 
Mi nahisi kuna mapito magumu utayapitia ktk shughuli zako lakini mwisho utashinda. Kutembea bila viatu ni ishara ya kuhangaika ktk kuelekea ushindi ukichanganya na kupanda miinuko mikali na kufika kileleni
 
Kiroho kutembea peku ni kunyang'anywa kibali kuvaa viatu visivyo vyako kubadilishiwa kibali maisha etc siyo ndoto nzuri kabisa kaa kwenye maombi funga rudisha kibali chako Tafuta mistari simamia (iko mingii)
Ndoto ya kwanza Ndio chanzo cha ndoto zote za chini Omba rehema na kibali kwanza mkuu ukianza na Zaburi 51 ,hesabu 14:18
 
Binafsi naota sana nasafiri yaani haizidi siku mbili nitaota nasafiri...wajuzi inaweza kuwa inaashiria nini..?
 
Sio ndoto mbayaaa za kukufanya ushindwe kufikia kitu ambacho Mungu amepanga ukipate ila
Kupata mahangaiko rohoni Roho Mtakatifu anakuonesha unahitaj kufuatilia hivi vitu

Usipuuzie ndoto, zote zina maana, gari ni maisha, kama gari ni maisha nani anaendesha hayo maisha yako, gari ni safari, yan maisha yako ni safari
Katika maamuzi mwambie Mungu akuongoze na sio mtu mwingine
Hatua za mwenye haki zaongozwa na Bwana

Na kingine, angalia mguu wako usikose kiatu, kiatu ni utayari, kuna kitu utayar wako umepokonywa hivyo omba viatu vyako virudishwe, omba utayari urudi
Na jua popote ulipo wewe ni mtumishi wa Mungu hivyo kusud la Mungu lisimame kupitia wewe,
Kama wenzio wana mavaz na wewe huna umevaw oversize angalia nani kachukua vazi lako sababu vazi ni uwezo na nguvu pia, nani kabeba Viatu vyako omba funga Mungu atakurejeshea,

Na huku kwingine almost ndoto zote zina ushindi
Ila hiyo kutembea kwa miguu na wenzio wana usafiri. Angalia tena, mbio za faras na mwendo wa miguu hazifanani,

Ukiweza kunens kwa lugha nena utavuka hapo all da best.Mungu akuvushe
 
Binafsi naota sana nasafiri yaani haizidi siku mbili nitaota nasafiri...wajuzi inaweza kuwa inaashiria nini..?
Rejea safar ya wana wa Israel walitakiwa kufika kanani, hivyo hiyo ni maisha yako angalia hiyo safar unafika au hufiki , kuna kikwazo gani njian
 
Hakuna MTU mwenye uwezo wa kufasili ndoto zaidi ya mungu mwenyewe.
Hao wanaotafsir wanajaribu kukaribia ila mwenye uwezo wa kufasili Ni mungu!.
Kama unasoma biblia jaribu kupitia vifungu mbali mbali utaona tafsiri
 
Kila kitu kiko kichwani mwako mwenyewe, ukiota ndoto za ajabuajabu ujue kichwa chako kimejaa garbage. siku nyingine kunywa bia mbili tatu kabla ya kulala. You will sleep like a baby
 
Hakika Mungu ni mwema dada Divine nimetafuta sana somo la malango bila mafanikio, ninasumbuliwa na ndoto za kuwa darasani eidha chuoni au shule ya msingi nikiwa eidha nafanya mitihani au ratiba za kawaida chuoni au shuleni ndoto imedumu kwa muda sasa nafsi inaniuma sana kila ninapoota ndoto hiyo
 
Hakika Mungu ni mwema dada Divine nimetafuta sana somo la malango bila mafanikio, ninasumbuliwa na ndoto za kuwa darasani eidha chuoni au shule ya msingi nikiwa eidha nafanya mitihani au ratiba za kawaida chuoni au shuleni ndoto imedumu kwa muda sasa nafsi inaniuma sana kila ninapoota ndoto hiyo
Nitakutag
 
Hakika Mungu ni mwema dada Divine nimetafuta sana somo la malango bila mafanikio, ninasumbuliwa na ndoto za kuwa darasani eidha chuoni au shule ya msingi nikiwa eidha nafanya mitihani au ratiba za kawaida chuoni au shuleni ndoto imedumu kwa muda sasa nafsi inaniuma sana kila ninapoota ndoto hiyo
Ni mlango wa nafsi kwa jicho la kiroho na sio malango nilikosea kukuambia uzi, nimekutag nenda kaangalie
 
Amina nashukuru sana kwa muda wako.
Nimekuelewa kiongozi nityafanya hivyo.
Kwanza miaka ya 2009 -2010 ilikuwa ni magari madogo ila meupe na nilikuwa napanda sigombanii ila ninaokuwa nao maranyingi sikuwa nawatambua na sifiki mwisho wa safari.
Kwenye mabasi Mara nyingi nagombania na ndugu
Mazingira huwa ni ya Miji Mikubwa.
Kwenye bus nimewahi kufanikiwa kuingia na kuanza safari mara moja ila nilikaa na mama mmoja mnene kavaa ushungi ila simfahamu na sikufanikiwa kufika nilipokuwa naenda na sijui nilikuiwa naenda wapi.
Ina maana unavyo safiri kabla hujafika unastuka??
 
Back
Top Bottom