Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Umepoteaaaa mi najua kutafsiri ndoto mkuu ila kuna malipo kidogo tu!!
 
Kwakua hamna kipya chini ya jua ..basi hata matukio mengi yanalazimika kujirudia iwe ni really au ndoton...

Sema nn ,,km kuna kaujumbe hapo !!.
 
Itakuwa kuna demu unataka kumuoa ila hakufai! Angalia hilo kwanza
 
Mkuu;
Japo hukuniweka kwa hao wataalam wako ila nakusaidia ki hivi:
Gari ni chombo cha huduma. Hivyo ulivyoota kuwa uliingia kwenye hayo magari ni kuwa; Upo kwenye huduma flani kubwa (Bus) lakini katika hiyo safari ukajikuta mmeingia landcruiser (huduma ikapunguzwa). Mkaendelea mbele kumbe daraja sio imara na sio la kutegemea. Mkatumbukia kwenye maji.
Kutokana na huduma unayoifanya, mbele na muda sio mrefu, mtapunguzwa wengi japo utabaki lakini mda sio mrefu hata wewe utakosa kazi. Tena bila malipo
Kwa utabiri huu anajuta hata kwa nini kauliza
 
fanya ibada kwa dini yako ndio sulusheni ya ndoto zako.
 
Habari zenu wanajamii, naimani mko salama,
Mwenzenu ninaota aina moja ya ndoto tokea 2009, haipiti siku tatu sijaota nasafiri au nagombania usafiri au nahangaika stand ya mabasi. Tafadhali mwenye uelewa anifafanulie ndoto hii tafadhali,. Naamini kuna watu humu wanauelewa na wanaweza saidia kutafakari.
Natanguliza shukrani.
Ni ishara ya kupambana na maisha ya mwili na roho (kuona unagombania kupanda basi).
Ikiwa unafanikiwa kupanda ni heri, ikiwa hufanikiwi kupanda ni ishara kuwa bado muunganiko wako na Mungu ni wa mashaka.
Ktk maisha yako jitahidi kuwa mwaminifu na ujiweke karibu na Mungu kwa sala. Unaonekana ktk mambo yako mengi unayoanzisha kama miradi hufikii malengo yako.
Kwa ufupi badilika kimienendo na umsogelee Mungu wako. Ndoto hii umeacha vitu vingi hujaeleza na ulivyoviacha ni mhimu pia mfano unafanikiwa kupanda, unapata siti, mnaishia wapi na safari,mwendo wa basi ukoje, mnasafiri kwa raha na mengineyo but all in all si ndoto nzuri sana zingatia ushauri.
 
Rafiki yangu ameota tumelala chumba kimoja kiko rafu nguo zimezagaa chini mara katokea nyoka akamng'ata kidole kapambana naye nyoka haachii kidole anasema mimi nikaja na panga nikamkata vipande nisaidieni kutafsiri ndugu zangu mnaejua ndoto
 
Mume wangu amekuwa akiota ndoto ya aina moja muda mrefu sasa haipiti wiki ndoto hiyo haijajirudia huwa anaota yupo shule katika stage mbalimbali anafanya mtihani lakini hajawahi kumaliza mtihani either hajui majibu ya maswali au anajua majibu ila anaogopa kuandika au karatasi za kujibia zinamuishia kabla hajamaliza mtihani aukaratasi zinakuwa zimerowa amashindwa kuandika akiota ni mtihani wa shule ya msingi wanafunzi anaowaona ni walewale aliosoma nao shule ya msingi sekondari na hata chuo wanafunzi ni wale wale na kila akiota anashituka kutoka usingizini msaada kwa anayejua tafsir ya ndoto hii
 
Mume wangu amekuwa akiota ndoto ya aina moja muda mrefu sasa haipiti wiki ndoto hiyo haijajirudia huwa anaota yupo shule katika stage mbalimbali anafanya mtihani lakini hajawahi kumaliza mtihani either hajui majibu ya maswali au anajua majibu ila anaogopa kuandika au karatasi za kujibia zinamuishia kabla hajamaliza mtihani aukaratasi zinakuwa zimerowa amashindwa kuandika akiota ni mtihani wa shule ya msingi wanafunzi anaowaona ni walewale aliosoma nao shule ya msingi sekondari na hata chuo wanafunzi ni wale wale na kila akiota anashituka kutoka usingizini msaada kwa anayejua tafsir ya ndoto hii
Mambo anayofanya yamepitwa na wakati abadili mbinu na njia zake za maisha.
Hata kama angeota anahangaika kuvuka daraja ila anashindwa ni sawa tu.
Kujiona uko stage ambayo in fact ulishapita tafsiri ni hiyo.
 
Wakuu nilikuwa nimelala usiku wa leo kuamkia sasaivi tare 13/01/2018, kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili na madakika...nimeamka saa moja. nimeota ndoto tatu. ndoto hizi haziondoki, they are so demanding moyoni mwangu kama nizijue maana yake, zinachoma na ni kama zinahitaji nifanye kitu haraka sana. kila nikijaribu kuzipotezea bado zinazunguka kichwani mwangu hadi sasaivi hadi nikaamua kuandika. ndoto zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. NDOTO YA KWANZA: Niliota tupo na watu wengine tumeenda Church, wenzangu wamevaa smart lakini mimi nimevaa tu suruari kubwa na jaketi kubwa bila kuvaa nguo zingine za mashati ni jaketu tupu na sijavaa viatu. Nikaingia mle ndani mimi peke yangu sina viatu. ndoto ikaishia pale nikastuka nikaanza kuifikiria ile ndoto na kutafakari, baadaye kidogo usingizi ukanijia tena. ile kutovaa viatu imeniuma sana na inazidi kuzungua moyoni kwamba kuna sehemu sijavaa viatu natembea vila viatu, and most likely spiritually: hivi kiroho mtu ambaye anatembea bila kuvaa viatu huwa inaashiria ana mapungufu gani:


2. NDOTO YA PILI: usingizi uliponijia tena, ndoto nyingine ikaja....Niliota napelekwa sehemu, mtu aliyeteuliwa kuwa dereva aniendeshe ananichelewesha hajui kuendesha vizuri na hajui wapi tunaelekea, mimi nikawa najaribu kumuelekeza nikamwambia asimamishe gari nimuonyeshe njia, tukashuka kwenye gari mimi nimuelekeze njia gani aelekee kwasababu mimi niliufahamu uelekeo viziru kuliko yeye, barabara ilikuwa bondeni sana, nikapanda toka kwenye cliff moja hivi refu kuifikia reli ili nivuke, ile cliff ilikuwa too sharp na ya hatari sana kuipanda ni kama korongo refu unapanda toka korongoni kufika juu, nilifanikiwa kwa shida sana kushikilia miimo ya ile cliff kwa kushika mawe yaliyojuu ni kama yalitunika kujenga msingi wa ile reli sasa mawe mengine yanaparanganyuka na kudondoka nikitaka kuyashika yanaporomoka hadi nikafanikiwa kushika juu kabisa nikashika taruma la reli ambalo haliporomoki ni imara nikawa namalizia kupanda sasa ili nifike juu, ile tu inabaki unaweka mguu kileleni huku umeshikilia chuma chuma la reli iliyotandazwa juu na hapo ndipo kwenye usalama na niliona moyoni lipo tumaini kwamba hapa nimepona kwasababu nimeshakanyaga hatua ya mwisho kufikia juu,(Yule mwingine aliyekuwa ananiendesha nimemwacha kule chini sana ya bonde)….. ila niliona Yule niliyemwacha kule chini sio rahisi kufanikiwa kupanda ile cliff kama nilivyofanya mimi kwasababu mapitio niliyoyapitia mimi hadi kufika pale mawe niliyokuwa nashikilia kupanda yamedondoka hivyo hakuna pa kushikilia tena na yeye atakosa pa kushikilia hadi kufikia nilipofikia mimi. ndoto ikaishia hapo.


3. NDOTO YA TATU: tena baada ya kutafakari ndoti ingine ilikuja ya taru mwishoni kabisa saa kumi na mbili: Tulikuwa safarini mimi nimeongozana na binti yangu wa kwanza, tupo wengi kwenye gari, tukafika mji Fulani maarufu wenye ofisi ya Umoja wa Mataifa….watu wanapanga mstari kuingia kwene jengo la Umoja wa mataifa kwa interview, wote hatujaanza kuitwa kwanza, mimi nimekaa pale nje na binti yangu na sisi tunajiandaa kuingia. Kuna askari wengi wa UN na wa kawaida, mara nikaona nimekaribisha watu wengi nyumbani kwangu wanalala hapohapo wanakula tunaburudika kwangu wengine classmates wa kike na kiume, mara nikaona classmate mmoja, na mzee mmoja na mtu mwingine pamoja na mimi tumeteuliwa kwenda kufanya shughuli Fulani ya Umoja wa Mataifa hivyo tukawa tumeenda chumba chetu spesheli kujadili yatupasayo kufanya.


Kwenye series hiyo hiyo ya hii ndoto kuna kipengele kinachosumbua moyo wangu, ambacho ni: niliona tunatakiwa kuondoka kwenda kwenye huo mji maarufu wenye ofisi ya UN. wale askari na watu wengine wote wakatangulia na basi la binafsi kuelekea huko UN, sisi wanne tuliokuwa tumeteuliwa spesheli na kwenye nafasi bora kuliko wengine wote kwenye ile shughuli maalumu, tukawa tunaenda kwa gari ndogo, mara nikajikuta tena tunatembea kwa mguu wakati wenzetu wameenda na basi, tukafika kwenye mlima mmoja mrefu sana na mkali sana ambao gari ni vigumu kupanda lakini lile basi la wenzetu limepita, ila sisi tukawa tunapanda ule mlima mkali kwa mguu, nikaona mimi na wenzangu tunapanda ule mlima bila shida yeyote, mwenzangu mmoja akawa anamsukuma mgongoni Yule mzee mwenzetu kama kumshikilia mgongo mtu anayeishiwa nguvu kuelekea juu mlimani ili apate nguvu kuendelea kuupanda ule mlima Yule mzee akapata nguvu ghafla na kuendelea kuupanda, tulipofika kama robo tatu ya ule mlima (bado robot u tufike kileleni) nikaona wote bado wana nguvu lakini mimi nimeanza kuishiwa nguvu lakini bado nina pursue kwa shida hivyo nikawa nashindwa kuendelea kwa haraka kama before kuupanda ule mlima ili nimalizie kale karobo kalikobaki nifike juu kileleni.

Mambo haya nimeyaota randomly bila systematic mpangilio wa kipi kinaanza na kipi kinamalizia ila matukio yote hayo yapo na yanazunguka kichwani kwangu muda wote hadi sasaivi ninavyoandika hii meseji. Ndoto zingine huwa naota zinaisha ila hii haiondoki kichwani mwangu, kama kuna mtu anaweza kunitafsiria tafadhali?
 
Kunyaa unyee wewe then mwingine aje kukutawaza? si umeota wewe au, we ndio utuambie tafsiri yake
 
hivi vipengele vyote kwa ufahamu wangu ni kitu kimoja tu, una vita vinapiganwa kati yako na maadui zako ili kukushusha cheo, kukuharibia biashara, kukuharibia mahusiano yako ya kimapenzi hii ipo sana kwa wanawake, kinachokusaidia ni malaika wako au mababu zako wanakusimamia, mwishoni hawa maadui zako watashindwa utafanikiwa ila utapata shida omba sana Mungu, na nenda kwenu ukasalimie baba, mama, mababu na mabibi zako kama wapo, kama walishafariki kasafishe makaburi yao.
 
Back
Top Bottom