Wakuu nilikuwa nimelala usiku wa leo kuamkia sasaivi tare 13/01/2018, kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili na madakika...nimeamka saa moja. nimeota ndoto tatu. ndoto hizi haziondoki, they are so demanding moyoni mwangu kama nizijue maana yake, zinachoma na ni kama zinahitaji nifanye kitu haraka sana. kila nikijaribu kuzipotezea bado zinazunguka kichwani mwangu hadi sasaivi hadi nikaamua kuandika. ndoto zenyewe ni kama ifuatavyo:
1. NDOTO YA KWANZA: Niliota tupo na watu wengine tumeenda Church, wenzangu wamevaa smart lakini mimi nimevaa tu suruari kubwa na jaketi kubwa bila kuvaa nguo zingine za mashati ni jaketu tupu na sijavaa viatu. Nikaingia mle ndani mimi peke yangu sina viatu. ndoto ikaishia pale nikastuka nikaanza kuifikiria ile ndoto na kutafakari, baadaye kidogo usingizi ukanijia tena. ile kutovaa viatu imeniuma sana na inazidi kuzungua moyoni kwamba kuna sehemu sijavaa viatu natembea vila viatu, and most likely spiritually: hivi kiroho mtu ambaye anatembea bila kuvaa viatu huwa inaashiria ana mapungufu gani:
2. NDOTO YA PILI: usingizi uliponijia tena, ndoto nyingine ikaja....Niliota napelekwa sehemu, mtu aliyeteuliwa kuwa dereva aniendeshe ananichelewesha hajui kuendesha vizuri na hajui wapi tunaelekea, mimi nikawa najaribu kumuelekeza nikamwambia asimamishe gari nimuonyeshe njia, tukashuka kwenye gari mimi nimuelekeze njia gani aelekee kwasababu mimi niliufahamu uelekeo viziru kuliko yeye, barabara ilikuwa bondeni sana, nikapanda toka kwenye cliff moja hivi refu kuifikia reli ili nivuke, ile cliff ilikuwa too sharp na ya hatari sana kuipanda ni kama korongo refu unapanda toka korongoni kufika juu, nilifanikiwa kwa shida sana kushikilia miimo ya ile cliff kwa kushika mawe yaliyojuu ni kama yalitunika kujenga msingi wa ile reli sasa mawe mengine yanaparanganyuka na kudondoka nikitaka kuyashika yanaporomoka hadi nikafanikiwa kushika juu kabisa nikashika taruma la reli ambalo haliporomoki ni imara nikawa namalizia kupanda sasa ili nifike juu, ile tu inabaki unaweka mguu kileleni huku umeshikilia chuma chuma la reli iliyotandazwa juu na hapo ndipo kwenye usalama na niliona moyoni lipo tumaini kwamba hapa nimepona kwasababu nimeshakanyaga hatua ya mwisho kufikia juu,(Yule mwingine aliyekuwa ananiendesha nimemwacha kule chini sana ya bonde)….. ila niliona Yule niliyemwacha kule chini sio rahisi kufanikiwa kupanda ile cliff kama nilivyofanya mimi kwasababu mapitio niliyoyapitia mimi hadi kufika pale mawe niliyokuwa nashikilia kupanda yamedondoka hivyo hakuna pa kushikilia tena na yeye atakosa pa kushikilia hadi kufikia nilipofikia mimi. ndoto ikaishia hapo.
3. NDOTO YA TATU: tena baada ya kutafakari ndoti ingine ilikuja ya taru mwishoni kabisa saa kumi na mbili: Tulikuwa safarini mimi nimeongozana na binti yangu wa kwanza, tupo wengi kwenye gari, tukafika mji Fulani maarufu wenye ofisi ya Umoja wa Mataifa….watu wanapanga mstari kuingia kwene jengo la Umoja wa mataifa kwa interview, wote hatujaanza kuitwa kwanza, mimi nimekaa pale nje na binti yangu na sisi tunajiandaa kuingia. Kuna askari wengi wa UN na wa kawaida, mara nikaona nimekaribisha watu wengi nyumbani kwangu wanalala hapohapo wanakula tunaburudika kwangu wengine classmates wa kike na kiume, mara nikaona classmate mmoja, na mzee mmoja na mtu mwingine pamoja na mimi tumeteuliwa kwenda kufanya shughuli Fulani ya Umoja wa Mataifa hivyo tukawa tumeenda chumba chetu spesheli kujadili yatupasayo kufanya.
Kwenye series hiyo hiyo ya hii ndoto kuna kipengele kinachosumbua moyo wangu, ambacho ni: niliona tunatakiwa kuondoka kwenda kwenye huo mji maarufu wenye ofisi ya UN. wale askari na watu wengine wote wakatangulia na basi la binafsi kuelekea huko UN, sisi wanne tuliokuwa tumeteuliwa spesheli na kwenye nafasi bora kuliko wengine wote kwenye ile shughuli maalumu, tukawa tunaenda kwa gari ndogo, mara nikajikuta tena tunatembea kwa mguu wakati wenzetu wameenda na basi, tukafika kwenye mlima mmoja mrefu sana na mkali sana ambao gari ni vigumu kupanda lakini lile basi la wenzetu limepita, ila sisi tukawa tunapanda ule mlima mkali kwa mguu, nikaona mimi na wenzangu tunapanda ule mlima bila shida yeyote, mwenzangu mmoja akawa anamsukuma mgongoni Yule mzee mwenzetu kama kumshikilia mgongo mtu anayeishiwa nguvu kuelekea juu mlimani ili apate nguvu kuendelea kuupanda ule mlima Yule mzee akapata nguvu ghafla na kuendelea kuupanda, tulipofika kama robo tatu ya ule mlima (bado robot u tufike kileleni) nikaona wote bado wana nguvu lakini mimi nimeanza kuishiwa nguvu lakini bado nina pursue kwa shida hivyo nikawa nashindwa kuendelea kwa haraka kama before kuupanda ule mlima ili nimalizie kale karobo kalikobaki nifike juu kileleni.
Mambo haya nimeyaota randomly bila systematic mpangilio wa kipi kinaanza na kipi kinamalizia ila matukio yote hayo yapo na yanazunguka kichwani kwangu muda wote hadi sasaivi ninavyoandika hii meseji. Ndoto zingine huwa naota zinaisha ila hii haiondoki kichwani mwangu, kama kuna mtu anaweza kunitafsiria tafadhali?