MKANDAHARI
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 5,727
- 6,615
Hongera mkuu..usha unganishwa kwenye international transport ila bado upo kwenye training [emoji23][emoji23][emoji23]Wadau naomba kujua hii ndoto ina maana gani
Mara ya Kwanza niliota napaa angani nikawa najisikia vizuri sana maana nilikuwa naona watu kwa chini wakinishangaa navyopaa angani!
Nikazurura zangu weee wakati wa kutua chini nikatua fresh bila tabu
Haikupita mwezi nikaota tena ndoto ile ile tena mara mbili kwa usiku mmoja. Mara hii nlikuwa nakwepa nyaya za umeme vibaya mno. Nakutana na nyaya za high voltage lakini kwa njia ya ajabu nikawa nazikwepa bila tabu. Na mwisho wa siku nikatua Kama kawaida.
Naombeni tafsiri wadau
Mkuu acha hizo basiHongera mkuu..usha unganishwa kwenye international transport [emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi kuna ndoto naota nikipita katika maji machafu au nikivuka mto wenye maji machafu na huwa sijawahi kufanikiwa kupanda kingo za mto nikaenda ngambo ya pili au naota nikitembea pembezoni mwa mto mkubwa wenye maji mengi yanayoenda kasi sasa nikishaota hiyo ndoto huwa hazipiti siku zaidi ya tatu bila kupata habari za msiba wa mtu yeyote ninayemfahamu. Nikishaota huwa nadikilizia kabisa. Nina kama miaka zaidi ya ishirini ya uzoefu wa ndoto hii. NAICHUKIA SANA. SIJUI NITAIEPUKA VIPIAmen
Ukiota ndoto mbaya unafuta kwa damu ya Yesu. Unaona mapema ili uzuie yasitokee hayo mabaya. Isaya 7:7Mimi kuna ndoto naota nikipita katika maji machafu au nikivuka mto wenye maji machafu na huwa sijawahi kufanikiwa kupanda kingo za mto nikaenda ngambo ya pili au naota nikitembea pembezoni mwa mto mkubwa wenye maji mengi yanayoenda kasi sasa nikishaota hiyo ndoto huwa hazipiti siku zaidi ya tatu bila kupata habari za msiba wa mtu yeyote ninayemfahamu. Nikishaota huwa nadikilizia kabisa. Nina kama miaka zaidi ya ishirini ya uzoefu wa ndoto hii. NAICHUKIA SANA. SIJUI NITAIEPUKA VIPI
Kuna mahali nilisoma wakasema kwamba ukiota unakula au unalishwa sio dalili nzuri, sio mtaalam wa ndoto ila ngoja akina Mshana Jr Divine Waje hapa watoe neno.Naomba msaada wa ndoto hii ambayo nimeota usiku wa kuamkia leo,nimeota nakula chakula,kuna,mwanamke simjui amekaa pembeni yangu ananipa chakula kiko kwenye sahani,nikawa na wasiwasi na hicho chakula lakini cha ajabu ninaendelea kula mpaka ninamaliza akanipa tena sahani nyigine,ila nilionyesha dalili yakutokukikubali hicho chakula laikini alikuwa akinisisitizia kuwa kiko salama niendelee kukila,then baada ya muda nilishtuka na nikaingia kwenye maombi makali ya kukemea,kama ni roho chafu au nimeunganishwa na maagano yaniepuke...
Habari za Asubuhi mpendwa.mimi kuna jamaa yangu tulikuwa Marafiki sana yaani maisha yetu ni kama mtu na kaka .lkn kuna ilikuja kutokea tukawa maadui wakubwa sana na yeye ndie aliyejitenga Nami. siku za hivi karibuni nimeota nimekutana nae maeneo fulani akiwa na mchepuko wake akanipa pesa tena dola kiasi fulani lkn ikawa nilipokuwa nazihesabu zikawa zinazidi idadi ya pesa alizonipa .pia alinipa koti lake na kofia flani kama ina hedfon nikawa naogopa kuivaa Ile kofia na yote ni Kwa sbb ya mambo ambayo nilishaisi juu yake Kwa hiyo ni mtu nisiyemuamini kabisa .je? ndoto hii inamaanisha nini.niyashukuru kama nitajibiwa na Mungu awabarikiSoma mwanzo 28:10-21
Halafu uonishe na hicho ulicho kiandika
duuh pole sanamwanzoni mwa wiki hii nilimuota mwanangu wa nguvu ambae amestangulia miaka minne iliyopita, ktk hiyo ndoto ilikuwa ni kama sherehe flani ambayo mimi nilialikwa tuu, nilipofika pale nilikuta watu wengi nisiowafahamu, ila nilimfahamu jamaa yangu ambae tayari ni marehemu, dah nilistuka, nikamwita kwa jina, jamaa akanipita kama hanifahamu, ila alienda pembeni hivi akaniita kwa ishara, nilipomfikia nikamuuliza G...ni wewe kweli? akanijibu yap ni mimi, jamaa alikuwa smart kavaa suti moja nyeusi iliyomkaa vyema..ikabidi nimuulize kaka we si umekufa? akanijibu mwanangu we acha tu, yah mimi nimekufa ila tuyaache hayo, vipi bi bimkubwa anaendeleaje? akimaanisha mama yangu, nikamwambia hajambo ila man kwanini upo hapa? akasema hapa waliopo karibia wote wameshakufa ila wapo watu watatu ambao mpo hai na hata hawa waliokufa si unawaona wapo hai? ilinibidi nikurupuke tuu, ndoto gani tena za namna hii? sasa kilichokuja nikumbusha hii ndoto ni hiyo siku iliyofuata ikaingia notification ya kuwatakia kheri za kuzaliwa bandugu kule facebook, jina la mwanangu ambaye ndio huyo Marehemu lilikuwa la kwanza....nilijisikia vibaya kwa kwali....siamini ktk ndoto ila...ndo hivyo