Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Samahanini wakuu wa umu ndani naombeni mnisaidie kujua maana ya hii ndoto,
Nimeota nipo nyuma ya bibi ambaye alikuwa ni mzee na tulikuwa tunapanda kama ngazi ivi (sikumbuki vizuri) lkn yule bibi alikuwa anatembea kidoge sana mpaka nikaamua kuchukua njia nyingine ili niendelee na safaril yangu lkn nilipompita yule bibi akatabasamu mara akanipatia pilipili hoho nyekundu nami nikaichukua alafu pembeni yangu kulikuwa na miti miwili ya matunda, mti mmoja ulikuwa ni wa matnda wa mapesheni na mwingine (nimesahau) basi nikachuma tunda moja moja kutoka kwenye kila mti lknpindi nilipokuwa nachuma tunda la pesheni nikawa natafta lililoiva lkn sikulipata nikachuma lile ambalo lilikuwa linaklibia kuiva mara ghafla mbele yangu nikamuona mwanamke ambaye nazani ulikuwa ni mti wake akawa anakuja kwa kasi nami nikaanza kukimbia naye nyuma yangu akasema weeewe lkn me nikawa nakimbia
Nisaidieni mana yake jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeota nimezaa mtoto wa kike mzuri na mweupe lakin tatizo Ana mkia na nikazaa tena wa pili wakati nataka kumnyonyesha nikagundia huyo mtoto Ana meno marefu kama ya mtu mzima nikamtupa nikastuka hii ndoto ina maana gani


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuota warudi darasani maana kuna mambo wapaswa kujifunza upya ktk maisha yako, tafakari upya ni kitu umepungukiwa nini?

Je, unafanya mitihani? Kufanya mitihani maana yake kuna majaribu utapitia au unapitia ktk maisha, mtihani ulivyokuwa ndivyo hali halisi utakayopitia ama unapitia ktk hilo jaribu.

Kuhusu simba labda nikuulize imani yako, Biblia 1Petro 5:8-9 inasema Ibilisi ni kama simba aungurumaye akitafuta mtu ammeze. Maandiko yanasema namna pekee ya kumshinda ni kuwa thabiti ktk Imani.

Tafakar maisha yako ya kiroho, kumbuka Imani ni neno pana sana ktk maandiko matakatifu.

Mfano Imani kuna mahali inatambulika kama wokovu, Yesu, haki n.k

Mungu akufanyie wepesi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari mkuu,.

Leo nmeota nipo darasani na wanawafunzi niliomaliza nao O level tuko tunafanya mtihani,ambayo io mtihani uneandikwa kwenye madaftali lakini mimi peke yangu daftali langu lilikua halipo.

Nikamwambia mwalimu na akanipa ela ya kununua daftali ili nifanye uo mtihani lakini nikaenda kuchukua ela uku nalia,
mwalimu akaniuliza kwanini nalia nikamjibu"hapana silii ila naogopa huu mtihani maana una maswali mengi sana, na ni kweli maana ulikua na maswali kama 360 ivi..

Msaada wa hii ndoto wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam!!

Habari zenu bandugu,Niende moja kwa moja kwenye mada wakati fulani nikiwa na umri kati ya miaka 11 ama 12 mara nyingi nilikuwa naota ndoto kama hivi "Naona watu wakitembea kwa misafara ukutani na hata niliposhtuliwa wakati mwingine na kakangu niliyekuwa nalala nae hiyo incident inaendelea kwa muda fulani hadi nitapozonduka hata kama naamshwa


Pia kipindi cha umri kati ya miaka 17-18 kuna ndoto ambazo kusema kweli ninewahi kuziota zaidi ya mara 1
I. Kuangukia katika shimo refu ambalo siwezi kuona mwisho wake
II. Nakimbia ama kuendesha baiskeli na kujikuta nashtuka ghafla
III. Ndoto mbaya zinazoambatana na vitisho vikali vya madude ambayo sijawahi kuyaona zikiambatana na hisia kana kwamba napiga kelele lakini sauti haitoki ama hakuna anayezisikia kuja kunisaidia
IV.Kuota naokota maburungutu ya fedha lakini naambulia hasira za matongotongo pindi napoamka

Kwa mwenye uelewa juu ya ndoto msaada tafadhali maana nahisi kupitia mojawapo ya ndoto hizo kuna message fulani ambayo inahitaji kuwa decoded nipate maarifa

Karibuni
 
Japokua nishawahi ota ndoto kama mbili na nikakutana na matukio yenye kufanana nazo but huwa Sizichukulii serious
 
Japokua nishawahi ota ndoto kama mbili na nikakutana na matukio yenye kufanana nazo but huwa Sizichukulii serious
Huwa nikizimbuka nawaza kana kwamba ni kama nimeziota tena so nahisi hapa kuna jambo

Najaribu tu kuwaza kwamba mbona toka kuzaliwa kwangu nimeota ndoto nyingi sana tu ila mbona hizi sizisahau??
 
Back
Top Bottom