Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Nyingine niliota napandisha mlima upo km ukuta japo nilipanda kwa shida ila nilipofika juu nilikuwa ghorofani kuna wazungu na mataifa mengine wanakula maisha na mm nikaungana nao japo ckula vyakula vyao ht vinywaji

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
Kupandisha mlima kama ukuta

Hapa maana yake kuna jambo unatamani kulifanya au kufanikisha lakini hilo jambo ni gumu si rahisi. Muhimu panga mipango yako sahihi kwa kila jambo then go after it

Unajumuika na wazungu lakini huli wala kunywa

Hapa maana yake ni kwamba jambo unalotamani kulifikia hauna uhakika nalo kama litakufanya uwe na furaha au amani kama unavyotegemea.

Fikiria vizuri kuhusu mambo unayodhani unayapenda na kuyahangaikia je utayafurahia ukiyapata?

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Mara nyingi naota nafanya mitian ya form six au nimerudia form six, wakati nina miaka zaid ya kumi toka nime maliza form six, na nilifanya vizuri sana,
Pia mara nyingi huwa naota watu walio kufa, au watu ninao wajuwa wanakula nyama za watu walio kufa....
Nifanyaje nisiote hizi ndoto tena? Kama ya kurudia form six haipiti mwezi lazima niote hiyo ndoto, tena utakuta mitian inakuwa migumu alafu unakuta sijasoma.....huwa inanitesa sana hii ndoto.
Kuota unafanya mtihani wa form six

Maana yake ni kwamba kuna tabia au mazoea fulani unayo katika maisha ya kawaida na ungependa uachane nayo lakini hujafanikiwa. Jichunguze vizuri halafu tia bidii ubadilike

Kuota kula nyama za watu

Maana yake ni hivi...yapo mazoea au tabia fulani ambayo haipendezi moyo wako lakini kwasababu fulani unaendelea tu kuikumbatia hiyo tabia. Nakushauri jaribu kuanzisha aina mpya ya maisha. Free yourself from all hatred, jealousy and mischief

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
ok vipi kuhusu ndoto moja kuwa na maana 2? Unaweza kujuaje ndoto ya aina hiyo?
Ndiyo ndoto inaweza kuwa na maana mbili.

Lakini hii haiondoi maana kuwa haikuhusu. Kumbuka ndoto yoyote unayoota inajaribu kueleza kukuhusu wewe labda na watu wanaokuzunguka inaweza ikawahusu kwa kiwango fulani. Lakini muhusika mkuu ni wewe.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wangu naomba msaada wa kutafsiri hii ndoto,

Nilikua nipo na mdogo wangu tunatembea Tu kawaida sehem ambayo ilikua ni kijijini au mashambani, maana hapakuwa na majengo mengi ila ni miti na miti niliyoiona ilikua mikuyu, tukafika eneo ambapo maji yamejikusanya mengii, ya mto na yalizuiliwa na miamba ya mawe ili yasipite ili kutengeneza ilo bwawa, maji yake hayakuwa meupe sana na yalikua yametulia tuli, ndani ya maji hayo kulikua na baadhi ya watu niliosoma nao sekondari wakiwa wanaogelea, mi nikawa ninahofu kubwa ya kuogelea kwa kuhofia kuzama, japo bwawa lenyewe halikuwa na kina kirefu, kilikua ni mita mbili na Mimi nilikua na mita moja point 9 ivyo nilikasoro point moja Tu, wakati huo wote mdogo wangu alikua yuko pembeni anajihusisha na shughuli za mikono,. Mkuu naomba unisaidie tafsir yake maana hii ndoto imenikaa kichwani sana.
Unaota unaona bwawa lenye maji na unaogopa kuingia

Maana yake ni kwamba unatamani kufanya jambo labda katika kukuingizia kipato au lolote lile lakini unadhani huna maarifa yakufanikisha hivyo.

Bwawa uliloona ni kipimo cha changamoto utakazokutanana nazo ukiamua kutekeleza jambo unalolitamani.

Marafiki uliowaona katika bwawa ni ishara kukuonyesha inawezekana kabisa wewe kuzishinda changamoto ndiyo maana umewaona wao hawazami kweye hill bwawa

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mimi ninaota sana ndoto za nyoka (na ninamuogopa sana huyu mdudu).
Jana nimeota niko sehemu nimejikinga mvua kibarazani kwa watu. Akaja mtoto wa kike miaka kama nane hivi kashika boksi lina nyoka watatu wa ukubwa wa wastani tu. Yule mtoto akaanda kuwachuna ngozi (wakiwa hai na akaanzia vichwani) yaani kashika vichwa vya wote watatu kwa mpigo anawachuna) nikaogopa kuwa watamuuma so nikawa namkataza nikalifunika lile boksi kwa mikono yangu lakini nyoka wakawa kama wanataka kunishinda nguvu watoke nje. Nikashtuka usingizini.
 
Wamenizunguka ila sina hofu,Wako watatu mmoja mweusi mwingine wa kijani na mwingine wa dhahabu,ila uyo wa dhahabu ndo anaonekan kuwaongoza ao wengin
Japo bado umeeleza kwa ufupi tu nitajaribu kukujibu

Unaona nyoka watatu rangi tofauti lakini huna hofu

Maana yake ni kwamba kuna tabia au a in a fulani ya maisha unaendesha na umetawaliwa na mambo matatu unayoyaendekeza. Inaweza kuwa mazuri au mabaya. Lakini kwa namna yoyote ile huoni tofauti yoyote.

Unaona nyoka wa dhahabu anawaongoza wenzake

Maana yake ni kwamba katika aina ya maisha unayoendesha kama nilivyoeleza hapo juu, ipo tabia kuu ambayo unaishikilia zaidi na kuiona inafaa japo inaweza isiwe nzuri mbele ya macho ya wengine.

Jaribu kuangalia je aina ya lifestyle unayoongoza mambo yapo sawa? Je tabia/mazoea yako ni yapi? Je ungependa uache hizo njia zako au unapendezwa nazo tu?

Duh
 
Nimeota ninabeba mait na MTU Fulani na Huyo MTU ninae beba nae ni marehemu,nn maana yake
 
Kilubwa Usiamini ndoto. Ndoto nyingi ni uongo Japo kwa waumini wa kikristo kuna baadhi ya ndoto ni Za MUNGU ila chache sana.
 
Wakuu kwanini ndoto kila ambapo unakaribia kuamka ndipo inaisha ile ndoto?
 
Nimeota ninabeba mait na MTU Fulani na Huyo MTU ninae beba nae ni marehemu,nn maana yake
Mara nyingi vitu unavyoviona kwenye ndoto ni sehemu ya haiba yako (personality)

Kuona maiti inawezekana ni namna ya kukuambia kuna jambo unapoteza.

Inawezekana kipaji fulani ulichonacho. Au namna fulani nzuri ya maisha unaiacha na unaelekea ambapo si pazuri sana. Au inawezekana jambo lako fulani la kazini.

Mtu uliyebeba naye maiti alishakufa.......hapa pia huyu uliyemuona ni sehemu ya personality yako iliyokufa tayari. Ambayo hauko nayo tena.

Ninamna fulani ubongo wako unataka kusema na wewe.

Kuota ni jambo poa tu.

Cheers
 
Nashukuru kwa ufafanuzi!! Kuna cku niliota boss wangu ananikimbiza nikamzidi mbio nikakata vichochoro nikampoteza

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
Hii ndoto yako rahisi kuielezea.

Kuna jambo unajaribu kufanya kwenye maisha yako ya kila siku. Au bado upo kwenye hatua za maandalizi.

Jambo hili linaweza kuwa la kiuhusiano, kifedha au kibinafsi tu.

Deep inside your spirit hauamini sana jambo hilo ni jema ua linamanufaa sana kwako.

You are in a dilemma.

Pia unapojaribu kuwazia madhara ya jambo unalotenda/unalotaka kutenda unaiona hatari isiyomidhilika.

Na hatari hiyo inajidhihirisha kwa taswira ya boss wako mwenye mamlaka.
 
Wakuu kwanini ndoto kila ambapo unakaribia kuamka ndipo inaisha ile ndoto?
Kwa sababu ndoto inatokea wakati ubongo wako unaoitwa conscious mind umelala angali ubongo wako wa pili unaoitwa subconscious mind unaendelea kufanya kazi.

Hapa kinachotokea subconscious mind yako inajaribu kuonyesha/kukumbuka experience fulani ambazo kwa kweli ni trillion of thoughts ulizowahi kuwaza kwa kipindi cha nyuma.

Ndiyo maana mara nyingi ndoto hazi make sense.

Inahitaji umakini kuelewa ndoto.

Asubuhi usingizi ndiyo unakutoka. Unapata akili sasa
 
Mkuu mimi ninaota sana ndoto za nyoka (na ninamuogopa sana huyu mdudu).
Jana nimeota niko sehemu nimejikinga mvua kibarazani kwa watu. Akaja mtoto wa kike miaka kama nane hivi kashika boksi lina nyoka watatu wa ukubwa wa wastani tu. Yule mtoto akaanda kuwachuna ngozi (wakiwa hai na akaanzia vichwani) yaani kashika vichwa vya wote watatu kwa mpigo anawachuna) nikaogopa kuwa watamuuma so nikawa namkataza nikalifunika lile boksi kwa mikono yangu lakini nyoka wakawa kama wanataka kunishinda nguvu watoke nje. Nikashtuka usingizini.
Mkuu nilikuwa sijaona hii

1• Unamwona mtoto na box lenye nyoka

Hapa maana yake ni kwamba mtoto na hao nyoka wanawakilisha changamoto fulani katika maisha yako.

Inawezekana nzuri au mbaya.

Labda masuala fulani ya kazini/kibarua au katika mahusiano unasita kuyachukulia hatua na kwa kweli inabidi uchukue hatua ili uyashinde.

2• Unamzuia mtoto kwa kujaribu kulishika box

Maana yake unaweza kukabili changamoto zako no matter how powerless you may think.

Mkuu you must become more courageous
 
Back
Top Bottom