1: Ndoto Unazozipata kwa Sababu ya Kushiba, Maneno mengi uliyoongea au kumbukumbu ya mambo yaliyopita.
Ndoto hizi ni asili, Kila mwanadamu anaziota. Mtu akikwambia huwa haoti ujue ni Muongo.
Mwenye Hekima Suleiman Anaandika
" Kadiri mtu anavyohangaika zaidi,
ndivyo atakavyoota ndoto;
sauti ya mpumbavu ni maneno mengi." Muhubiri 5:3
Hapa hakuna uhusiano na mapepo, majini wala mashetani.
2:Ndoto Zinazoletwa na Mashetani.
Hii inaushahidi wa kiuzoefu tu. Leo utakuwa umesikia mtu kalala, kaota anafanywa mapenzi na anapoamka asubuhi anakuta amemwagiwa hadi mbegu za kiume huku alikuwa peke yake kitandani.
Wapo wanaooteshwa na kuamka usiku kwenda kulima,kufanya kazi na wanaamka wamechoka, ikifika asubuhi anaweza kukumbuka kama alikuwa anaota anafanya kazi kumbe kazi ilikuwa halisi.
Wapo wanaoamshwa kichawi, wanafanyishwa matukio ya ajabu akiwa katika hali ya ndoto.
(Hapa wenye ukina zaid wanaweza kufafanua ila ni vitu halisi havihitaji kuamini Mungu/Shetani Yupo au hayupo)
cc
Bilionea Asigwa Mshana Jr
Kwa watu wanaomuamini Yesu, Hutokaa ukutwe na mambo haya labda kama unaamini katika viwango vya unafiki au unachanganya dini na uchawi/ulozi.
3:Ndoto Zinazoletwa na Mungu.
Hizi Mungu mwenyewe anasema "Akiwepo nabii kati yenu, Nitasema naye kwa njia ya NDOTO" Hesabu 12:6
Lakini Sio tu nabii, hata watu wa kawaida, hata wasio watu wa Kitabu, hata viongozi.
Alisema kwa njia ya ndoto na Farao, Nebuchadneza, Yule mfungwa gerezani pamoja na Yesufu.
SIFA ZA NDOTO HIZI
1: Ziko wazi, hazina kona kona au kubahatishabahatisha.
2:Lazima zitimie.
3:Hazikutegemei wewe kuifanya itimiie.
4:Huwa haziji mara kwa mara.
MWIISHO
Nimeandika haya ili kusaidia watu ambao wanaota nndoto za kawaida tu, ambazo ukikaa mwenyewe ukafikiri kwa nini umeota hilo utagundua tukio lililopita au mazungumzo yaliyopita ndio chanzo cha ndoto lakini wameibuka watu ambao wao wanaamini kila ndoto ni matokeo ya majini. Kila ndoto lazima iwe na tafsiri, Kila ndoto ni ya Mungu au Ya shetani.
Wajuvi zaidi wa mambo haya wanaweza kuja kushuka nondo zaidi.