wakuu naombeni msaada wa tafsiri ya ndoto hii, leo nimeota kuwa nipo maeneo flani nmevaa gwanda za FFU ghafla nkakutana na askari kibao wametanda barabaran njiapanda hivi wakiwa kama wanasaka kitu flani.(kwa walioko dodoma ni pale ilipo airtel shop)
Kutokana na hofu nilishtukiwa na afande mmoja akaniuliza kitu ambacho skumbiki ni nn, nkamuita pembeni nkamwambia broo naomba unisamehe na usiwaambie wenzako please, naomba unitoe eneo hili akakubali, tukiwa njiani kuelekea kusikojulikana tukakutana na askari wengine wengi sana wakiwa kwny paredi, jamaa yaonekana alikuwa mkubwa alipokaribia akawaamulisha wakafungua mguu(mguu pande), nikiwa katika hofu sana nilitembea kwa kutetemeka hadi nikaskia minong'ono miongoni mwa askari waliokuwa pale.
Tulifika sehem inayoonekana kuwa ni nje ya mji kwnye mashanba ya watu, nliwaona jamaa flani wanalima tuliwasemesha ( skumbiki tuliwasemesha nini) tukakatiza katikati ya mashamba kutafta njia, mbele kulikuwa kama na korongo flani lililotuzuia kupita, tukapinda kulia hivi, kulikuwa na nyumba flani ndogo hivi inayoonekana ubavuni, kwa mbele kulionekana barabara ya lami na magari yalionekana kupita.
Yule Askali akanambia sasa tafuta barabara inayoelekea Bahati au Arusha urudi, nlishangaa sana kwanini jamaa kanifikisha mbali hvo na sjui narudi vipi dom maana sikuwa hata na mia mfukoni.
Wakati na tafakari jamaa skuona alipopotelea ghafla wakaja mabinti wawili nnaowafahamu, ambao sikuwa na wazo la kujiuliza wapetokea wapi kwa sababu tulikuwa pembeni ya nyumba ile. Basi wakanisemesha (skumbiki tuliwasemeshana nini ), dada mmoja akanambia kuwa anapenda shati langu huku akilishikashika, ghafla nikagundua sijavaa gwanda za FFU tena bali ni nguo flani kama rangi ya maziwa hivi.
wakati akishika shati langu nikagundua kuna maandishi mengi sana kwny suruali yangu mguu wa kulia wakiyoandikwa kwa kalam ya wino.
Nilishangaa sana na kujiuliza yametoka wapi, baada ya kuchunguza vizur nikagundua sio maandishi bari ni namba nyingi sana zmeandikwa na kutengeneza kama umbo la mraba hvi, niliangakia kwa umakini nikaona kuna namba tatu zimeandikwa kwa wino mwekundu ambazo ni 1, 3, na 7 halafu kuna moja ya mwsho iliandikwa kwa wino wa blue kama zingne ila naikumbuka kwa sababu ilikuwa ni ya mwsho upande wa chini kulia mwa umbo lile la mraba na ilikuwa haijaandikwa kikamilifu na ilikuwa kubwa kuliko zote, nayo ni namba 8 ( iliandikwa as if mwandishi alikuwa na speed kubwa hivyo haikufungwa vizuri upande wa juu kulia).
Baada ya hapo nilishtuka toka usingizini.
Sent using
Jamii Forums mobile app