Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

MWANAMKE UKIOTA UNA NDEVU
Mwanamke ukiota una ndevu ni dalili ya kuwa hutazaa milele,na baadhi ya wafasiri wamesema ni dalili ya maradhi ambayo yatampata siku za usoni,au ziada ya mali ya mumewe na utukufu wa mwanawe wa kiume.
KAMA AKIWA AMEOLEWA
Ni ishara ya mumewe kuondoka
AKIWA NI MJAMZITO
Atazaa mtoto wa kiume na litatimia jambo lake
AKIOTA NDEVU ZIMEREFUKA NA KUWA NYINGI
Umri wake utakuwa mrefu na mali yake itazidi kuongezeka
UKIOTA UNA MASKIO MATATU
Ni ishara ya kuwa na mke mmoja na mabinti wawili
UKIOTA UNA SIKIO NUSU
Inajulisha kifo cha mkeo na kuwa utaoa mwingine badala yake
UKIOTA UNA MASKIO MANNE
Inajulisha moja kati ya mambo mawili
1.utakuwa na wake wanne
2.mabinti wanne wasiokuwa na mama
UKIOTA MASKIO YAKO YAMEJAZWA VITU NDANI YAKE
Ni dalili ya kuwa utakufuru
KUOTA MENO YANAVUNJIKA
Ni dalili ya kuwa utalipa deni lako kidogokidogo
UKIOTA MENO YANADONDOKA NA UNAHISI MAUMIVU
Ni dalili ya kuondokewa na kitu katika vitu vilivyomo ndani mwako
UKIOTA MENO YAKO YA MBELE TUU YANADONDOKA
Ni dalili ya kuwa unazuiwa kufanya jambo lako ulilokuwa ukilifanya ima kwa vitendo au maneno
UKIOTA KITU KINATOKA MDOMONI MWAKO
Ni dalili ya rizki utakayoipata iwe ni halali au haramu
UKIOTA UNA ULIMI MREFU
Ni dalili ya kushinda katika ufasaha wa kuongea na adabu yako,upole na utukufu
UKIOTA ULIMI WAKO UMEFUNGWA
Ni dalili ya ufukara na maradhi
UKIOTA UNA MENO MEUPE NA MAZURI
Ni dalili ya ziada katika nguvu na mali ya daraja ya juu kwa watu wa nyumbani mwake
UKIOTA UNA MENO YA DHAHABU
ukiwa ni mwenye elimu basi ndoto yako ina sifa nzuri,na ikiwa sio mwenye elimu basi basi ni dalili ya shari na watu wako watapatwa na maradhi au kuangamia
UKIOTA UNA MENO YA FEDHA
Ni dalili ya kupata hasara katika mali yako,na yakiwa ni meno ya kioo ni dalili ya umauti
KUOTA UNALISHA MASKINI
Utatoka kwenye majonzi na utapata amani kama ulikuwa na hofu
UKIOTA UNASWALI KATIKA ALKAABA
Utapata baadhi ya watukufu na viongozi na utapata amani na kheri
UKIOTA UMEKUFA NA KUFUFUKA
Utafanya madhambi na utamuomba mungu msamaha
KUOTA UNAKUFA BILA KUUMWA
Umri wako utakuwa mrefuu
UKIOTA UMEKUFA,WATU WANAOMBELEZA NA KUKUFANYIA SHUGHLI ZA MAZISHI
Dunia yako itakuwa nzuri lakini akhera yako imeharibika
KUOTA MAITI INAJIOSHA YENYEWE
Watu wako watatoka kwenye majonzi na mali yao itazidi
KUOTA UNAONA SANDA
NI DALILI YA ZINAA
UKIOTA SANDA IMEVESHWA LAKINI HAIJAKAMILIKA UVAAJI WAKE
Utatiwa kwenye zinaa lakini hutokubali
UKIOTA UMEFUNGWA KWENYE SANDA VILEVILE KAMA MAITI
Ni ishara ya kifo chako
KUOTA UPO KWENYE JENEZA
Utajenga udugu na mtu kwa ajili ya mungu
UKIOTA UPO KWENYE JENEZA NA WATU WAMELIBEBA
Utatawala na kupanda daraja na watu watakufuata kama ulivyowaona ndotoni
UKIOTA UMEBEBA MAITI
Utapata mali ya haramu
UKIOTA UNAMPELEKA MAITI SOKONI
Utapata mahitaji yako na faida kwenye biashara zako
UKIOTA JENEZA LINAPITA HEWANI
Atakufa mtu mkubwa kama rais,mwanachuoni au yeyote mwenye daraja ya juu
UKIOTA UMEKUFA NA UNAZIKWA
Utasafiri safari ya mbali na utapata mali
KUOTA UMEMFUFUA MAITI
Utamsilimisha mtu wa dini nyingine kuwa muislam au mtu muovu atatubia dhambi zake kwako
UKIMUOTA DADA YAKO ALIYEKUFA ANAISHI
Utajiwa na mgeni kutoka safarini na utafurahi
UNGANA NAMI KATIKA SEHEMU YA PILI
 
habarini, kuna ndoto naiota hii ni mara ya pili. naota nimepita sehemu nimefika sehemu chini nikaona hela noti ya elfu 5 afu zimekunjwa. kila nikiokota naona nyingine mpaka najaza mifuko yangu ya suruali. cha ajabu hizo noti hazionekani vizuri mpaka uwe na kipaji hasa.

mara ya kwanza kuota hii ndoto niliota niko na rafiki yangu, ila wakati naziokota hizi noti yeye alikuwa anapata tabu sana kuziona ila mimi nikawa nafanya kazi ya kumuonyesha

mara ya pili nikiwa napita tena, nikakutana nazo tena, nikaanza kuziokota kama kawaida yangu. hii inamaanisha nini hii ndoto ya kuota unaokota hela?
 
Nimeota.

Nimetobolewa masikio. Mtoboaji alianza sikio la kushoto kisha la kulia.

Nikawa kama wale wamang'ati au wamasai.

Du kuamka ni saa kumi na nusu alfajiri.


Tafsiri tafadhali.
 
Kutobolewa? Jemsi Delishiaz unamjua hebu mcheki kwanza
 
Yaonyesha unakiburi na siku si nyingi kiburi chako kitakomeshwa!😂
 
wakuu

nimeota kuna mzee nafahamiana nae hapa kijijini kwetu na ni mzee anaheshimika kweli Kwa busara zake,hekima na utulivu wa akili yake.
Leo nimeota nilikua barabarani taratibu natembea basi taratibu akawa anapita na gari lake ,alipofika karibu yangu akalisogeza karibu kabisa na nilipo ile kama anataka kupack, akanitazama tu na hakuongea kitu na hakupaki akairudisha gari barabarani na kuondoka kwake nyumbani alikua anarudi nyumbani. Huwa si kawaida yake Kwa tulivyozoeana na anavyonifaham mimi na wazazi wangu.

Nimeamka asubuhi Leo nimepokewa na habari kwamba mzee fulani amefariki dunia. Hii imekaaje sijaelewa au kule kunitazama ndo majibu yake haya asubuhi ya leo....
 
Jana nilikuwa nasoma kitabu cha The Big Tree of Nebuchadnezzar kilichoandikwa na Kabongo wa Kabongo mwana Lubumbashi akiwa hapo Upanga Dar es Salaam anasema usiidharau ndoto yoyote ile ... kwa kuwa kila ndoto ina maana yake na hutimia....



Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 
Mimi kuna ndoto moja huwa inajirudiarudia yani naweza kuota hiyo ndoto hata mara tatu kwa mwezi sasa ni kama miaka nane tangu nianze kuiota.

Huko kijijini kwetu kuna mlima mmoja mrefu huu mlima sijawahi kuukaribia huwa nauona tu kwa mbali cha ajabu nauota mara kwa mara kama nilivyoeleza hapo juu. Kuna wakati naota nimeuona eneo tofauti na hapo kijijini kwetu lkn kuna wakati nauona hapohapo ulipo.

Mwanzoni nilichukulia kawaida lkn sasa napata mashaka iweje niote kitu kilekile mara zote hizo! Kwa wale mnaojua kutafsiri ndoto mnisaidie hapa.

N.B Ktk hiyo ndoto huwa nauona huo mlima kwa mbali.
 
Habari ya asubuhi na poleni na majukumu wakubwa zangu na wadogo zangu pia. Mimi mwenzenu leo nimeota ndoto hii"nilikua naendesha baiskeli barabarani sasa kulikua kuna gari nataka ku overtake hivyo basi nikawa nimefanikiwa ku overtake.

Mara ghafla gari nyingine ikawa inakuja kunigonga uso kwa uso daaah hapo nikashtuka usingizini ghaflaa...aisee yeyote mwenyewe uelewa wa ndoto hii anisaidie maana si mara ya 1 naota ndoto ya namna hii.

karibuni wakuu msaada wenu
 
Habar ya asubuhi na poleni na majukumu wakubwa zangu na wadogo zangu pia...,mimi mwenzenu leo nimeota ndoto hii"nilikua naendesha baiskeli barabarani sasa kulikua kuna gari nataka ku overtake hivo bas nikawa nimefanikiwa ku overtake sasa mara ghafla gari nyingine ikawa inakuja kunigonga uso kwa uso daaah hapoo nikashtuka usingizini ghaflaa...aisee yyte mwenyewe uelewa wa ndoto hii anisaidie maana si mara ya 1 naota ndoto ya namna hii.....karibuni wakuu msaada wenu
Umekwishaaa..... Ngoja wake wajuzi na wale wa mi5 tenaa
 
Habari ya asubuhi na poleni na majukumu wakubwa zangu na wadogo zangu pia. Mimi mwenzenu leo nimeota ndoto hii"nilikua naendesha baiskeli barabarani sasa kulikua kuna gari nataka ku overtake hivyo basi nikawa nimefanikiwa ku overtake...
Ukiota ndoto mwombe Mungu akupe tafsiri wanadamu hakuna ajuaye tafsiri sahihi ya ndoto ndugu yangu utadanganywa tu
 
Huenda kuna kitu kibaya kinataka kukutokea lakini unakiepuka bila kujijua.. Ikitokea tu ukaota umegongwa bro jichimbie kaburi kabisa.. Mitano Tenaaa!!
 
Hali yako ya kiuchumi ikoje? Baiskeli inasimama kuonesha mtu mwenye uchumi mdogo na gari katika ndoto yako linasimama kuonesha mtu mwenye uchumi mkubwa.

Ulivyoota unataka kuovertake gari ni kuwa,kwa akiri ya kawaida ni ngumu mtu mwenye baiskeli kuovertake gari,hivyo maana ya ndoto yako ni hii:-

Katika Maisha yako unajaribu kupambana sana ili kujikwamua na hali uliyokuwa nayo katika Maisha yako,na kuna wakati unatumia nguvu nyingi sana katika kujikwamua na juhudu nyingine zinakuwa ni za hatari ambazo zinaweza kupoteza au kuhatarisha Maisha yako.

Hivyo nakusihi sana ndugu Yangu kuwa makini katika harakati zako za kujipatia riziki kwani kuna muda zaweza kukutia katika hatari (kifo)

Kwa kuongeza ni kuwa mtu hapaswi kupuuza ndoto,huwa zina ujumbe mzito sana ukizifuatilia,na kunakipindi inafikia kile ulichoota lazima kitimie
 
Back
Top Bottom