Ndugai ashukiwa "kama Mwewe" na Mwenezi wa Njombe

Ndugai ashukiwa "kama Mwewe" na Mwenezi wa Njombe

Kama huna bando ni hivi, Ndugai aliupata Uspika kwa fitna dhidi ya Mama Anne Makinda, Ndugai alitibiwa kwa mamilioni ya fedha ughaibuni na hajapona Bado, Ndugai ana tabia ya kuwachapa bakora wapinzani wake...
Na Kali kuliko zote, Ndugai anawashikilia Wabunge 19 wasio na vyama kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano....

Video Iko chini
View attachment 2064271
Nimecheka sana kicheko cha kufungia Mwaka... Mpiga fimbo mwenzie
 
CCM haikauki kusifiwa

RaisCCM SpikaCCM MweneziCCM mashabiki cuf, chadema,act

Maendeleo hayana vyama 🙏
 
Naona amaleki wanatoka shimoni kumshambulia ndugaye....
Kwa mimi nilivyo muelewa ndugai katika speech yake halafu na haya yanayo endelea naona ni vitu viwili tofauti naona kuna watu wameamua kuipotisha speech ya ndugai makusudi kabisa

Wewe ngole nikuonye tuu hadhi yako sio ya kumsema spika kwa maneno makali kama hayo na hiyo sio hulka ya CCM niijuayo mimi nadhan umeamua mwenyewe kujiondoa rasmi uenezi njombe vijijini kila la kheri Mwa NGOLE urudi sasa wikichi kulima viazi.
 
Mimi yote aliyozungumza huyu jamaa kuna baadhi ya mambo simuungi mkono kabisa kwani suala la Ndugai japo kazungumza hadharani lakini vitendo vya kila mtu kuibuka hadharani na kuanza kumzodoa Ndugai havijengi chama chao sana sana ni kutengeneza migogoro ya hovyo hovyo tu.

Katika mazungumzo yake kuna mambo matatu huyu mwenezi wa Njombe kayazungumza kwa kweli yamenifikirisha sana:-
1. Ukabila. Ndugai alizungumzia Ugogo wake na jamaa kamzodoa kwa kutumia huo huo ugogo wake. Hili suala la ukabila sio dogo na watanzania tusilichukulie poa hasa kipindi hiki ambapo linazungumzwa wazi wazi. Na hili kuna mtu fulani alipanda mbegu ya ukabila na ukanda miaka michache iliyopita na hakukuwa na mtu wa kukemea hata viongozi wa dini walikaa kimya sasa mbegu imeanza kuota na kumea kwa kasi. Chonde chonde viongozi wastaafu na viongozi wa dini likemeeni hili suala la ukabila mapema tena kwa ukali kabisa kama alivyokuwa anafanya baba wa taifa kwani likiachwa likakomaa hili hakuna atakayebaki salama.

2.Wabunge wasio na chama. Kila siku najiuliza ni nani aliyewapa nguvu na anayewakingia kifua wabunge hao ambao kwanza waliapishiwa gereji pili barua za chama wanachosema kiliwapa hiyo nafasi ya kwenda huko bungeni zilikuwa na utata mkubwa. Je hao wabunge sasa hivi ubunge wao upo salama kiasi gani baada ya hata wana CCM kuanza kuhoji uhalali wao na kutaja kabisa kuwa Spika ndio anawalinda. Na je kama kweli Spika anawalinda anawalinda kwa maslahi ya nani? Na je wapo bungeni kwa gharama za nani kama sio mtanzania huyu huyu maskini anayetozwa tozo? Je huyu mwenezi amefanya nini kupitia chama chake kuhakikisha kuwa wabunge wasio na chama wanafurushwa bungeni ili kuokoa fedha za watanzania au alikuwa anasubiri tu spika akosee tu halafu aje hadharani kumnanga kupitia hao wabunge?

3. Matibabu ya spika. Kwa kweli ni haki huyu mwenezi kuhoji gharama kubwa ya matibabu ya spika kwa hili namuuunga mkono asilimia 100. Lakini napingana naye kwa kuhoji kwa kudhihaki ugonjwa wa spika kwa kweli hata kama binadamu ana kosa gani lakini isifike mahali tukaanza kukejeli/kubeza ugonjwa wa mtu. Kila mmoja wetu hapa natumaini ameshawahi kuumwa muda mrefu au kuuguza muda mrefu kwa hiyo anajua madhila ya kuuguza muda mrefu. Basi ifike mahali tuhoji tu kwa busara gharama za matibabu ya spika lakini tuache kubeza ugonjwa wake kwani spika yeye ni binadamu kama binadamu wengine na hakuomba kuumwa bali maradhi yalimpata kama yanavyowapata binadamu wengine.

Kwa kweli kama ni spana jamaa kampiga spika spana hasa na huko Ndugai alipo nahisi atakuwa amejifungia ndani anaaiangalia hiyo "video" anairudia mara mbili mbili halafu haamini nini kimetokea.
 
Back
Top Bottom