Ndugai: Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL inapata hasara, je tuendelee kununua nyingine?

Ndugai: Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL inapata hasara, je tuendelee kununua nyingine?

Wananchi wajifunze 2025,
CCM haitaweza kamwe kuikomboa hii nchi kimaendeleo ya uchumi.

Siyo kila mwaka mnakuja na kauli za kijinga na uongo km vile;

Hapa kazi tu,
Mitano tena,
Kazi iendelee,
N.k.
 
1. Natamani taarifa ile ungeichambua ukaweka hayo madudu moja baada ya lingine tukayajadili hapa.

2. Masuala mengine ni wahusika kuwa wazembe kushindwa kurejesha majibu kwa wakati kwa CAG (kujibu hoja)

3. Nina imani kubwa Bunge litakapojadili mengi yatatolewa ufafanuzi na yataondoka!

4. Tunamshukuru sana CAG ametekeleza maagizo ya mzee marehemu Hayati JPM na Rais wa sasa Mhe. Samia Sukuhu Hassan kama alivyomwambia ukaandike report ya kina ili tuisaidie serikali na kukomesha ufisadi na wizi. Hivyo CAG amefanya kazi yake kwa weledi kama mwalimu wetu Prof. Assad

Tuwe na akiba ya maneno ndg zangu. Tusubiri Bunge lipitie taarifa hiyo kwa kina tujue mbivu na mbichi.

Namshauri Rais wetu mama yetu Mhe. Samia. Kama kuna mtendaji yoyote yupo madarakani na itathibitika kuiletea Serikali hasara na pia uzembe wa kutokujibu hoja za CAG, basi amtoe haraka sana kabla hajamuharibia kazi
Nyie mtakuwa wanufaika wa wizi uliokuwa ukifanywa na JIWE!
 
Ndugai naona mitazamo yake ya kiuchumi ni kama ya Samia Suluhu. Yule jamaa aliyekuwa anaua sekta binafsi alikuwa anaturudisha miaka 40 nyuma na wala hashauriki. Mashirika binafsi ya ndege alifanya juhudi yafe wakati ATCL ni hasara, PPP ilikuwa imeshakufa.

Watu mnalumu tu kwa nini hawakuongea Magufuli akiwa madarakani, pengine mlikuwa hamumjui Magufuli. Pengine waliona anaharibu sana na haambiliki wakaamua wamtangulize tu kama baadhi ya watu wanavyodai.
Haya mambo leo Ndugai anaongea akina Mbowe waliongea sn wakaambiwa ni vibaraka wa mabeberu, Ndugai ni mtu hatari sn na wa hovyo, mbona kipindi cha marehemu alikuwa mtu wa kusifia tu na madudu yote anayajua?
 
Hapana uzeni zote mtafute njia nyingine za kusafiri.
 
Mzee Mwanakijiji na Pascal Mayalla wanazungumziaje ripoti ya CAG na mwendazake?
Bado wanasaka NDIMI mpya za KUTAFUTA kukubalika na kuendana na 'nyakati' kama Mzee wa fito.
P alitoswa na WANYUMBANI, sasa aendelee kubaki nae wa nini.
Kinacho wachelewesha kupata mwondoko wa kuingilia.
 
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.
So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.
Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu aliyetupa Mali alitunyima akili.
 
Viongozi wote hawa walinyamazishwa, leo wameamua kufunguka.
 
Daah Job Ndugai kafunga kazi leo.

Meaning kila jambo alilokua anafanya na Magufuli hakuliafiki??

As a Christian lazima akatubu kanisani, hii ni dhambi ya wazi na itamtafuna.

Ndugai ajiuzulu tu , hii ni zaidi ya aibu.
 
Back
Top Bottom