Yote kwa yote, ukweli halisi ni huu.
1. Huenda zaidi ya 90% ya watumishi wa umma hawakuwa tayari kuhamishwa kutoka Dar kwenda Dodoma.
2. Uamuzi wa kuhamishia shughuli za kiserikali kutoka Dar kuja Dodoma haukuwa na maslahi yoyote kwa taifa. Ulikuwa ni uamuzi wa kipuuzi na kipumbavu kwa 100%
3. Dodoma haiwezi kuwa mbadala wa Dar katika hali yoyote ile. Ni sawa na kujaribu kulazimisha usiku uwe mchana na mchana uwe usiku.
4. Mtawala wa sasa (Samia) ameonyesha nia ya dhati kabisa kuachana na mpango wa yeye na serikali yake kukaa Dodoma. Huenda hapapendi na hapataki Dodoma.
5. Kiuchumi Dodoma inaenda kugeuka na kuwa sawa sawa na kile kilichoipata Mtwara wakati wa kuchimbwa gesi. Watu na wafanyabiashara wengi waliaminishwa makubwa kutokea Mtwara wakati gesi inachimbwa kinguvu, wakakimbilia kuwekeza, kilichowakuta ni majuto matupu.