Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Mwende kwanza Halmashauri Kuu mkatafute kupata mitazamo yenu upya, baada ya kuachwa na Marehemu.
 
."...razima niseme ukweri..hii nchi ni tajiri..imeriwa sana"....kumbe 🤪🤪🤣🤣
 
kwani mwendazake mikataba alikuwa anaweka wazi ? vipi kuhusu na mikataba ya ununuzi wa ndege je iliwekwa wazi na kupitishwa na bunge?
 
Kwa hiyo kwa madudu haya yanayoanikwa, wewe uko wapi? Mama au Marehemu? Hujui kajinywe uji kwanza.
 
Ninachojifunza hapa ni kuishi maisha yako bila kumtegemea mwanadamu maana kumtoshereza ni vigumu.
Hivi itokee muujiza wamkute ndugu magufuli asubuhi yupo kwenye kiti chake ikulu akipitia taarifa zilizotolewa wakati amevunga kufa ili kuwaona wabaya wake, je atabakiza hata mmoja kwenye serikali yake?!
 
Bandari ya Bagamoyo ijengwe Kwa haraka Sana, na inahitajika Kwa haraka mno Kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu,

Lakini, Kwa kuwa hii ni nchi yetu sote, maana awali tulisikia sifa na uzuri wa uwekezaji huo, Mara ya pili tukasikia, uwekezaji huo, ni mwendawazimu pekee anayeweza kuruhusu uwekezaji wa Aina hiyo

Ili kuondoa utata, Tunaliomba Bunge kupitia Mh Sipika, Mkataba huo usomwe bungeni, nini faida yake na hasara yake

Itatusaidia kuondoa tongotongo usoni,

Kwa maana Kwa sasa hivi, CCM kuwaamini ni Sawa na kupoteza sehemu ya akili yako,

Maana usije kuta huyo anayewashawishi wabunge wenzake, na yeye aliahidiwa mgao wake, maana hata kile kipindi, ni yeye tu aliyekuwa amekomalia na badaye tena yeye mwenyewe Akasema, mradi huo masharti yake ni mabovu na haufai

Inakuwaje tena Leo anabadirika?? Unajua Kweli nyinyi CCM ni watu wa ajabu Sana,
 
Tatizo langu siyo kuurudisha au hapana, Spika atueleze juu ya yale masharti. Ndivyo yalivyokuwa au hapana? Kama ni ndiyo, spika usijifanye nawe ni mkuu wa nchi. Kama sivyo, hapo tujadili aliyemdanganya rais ni nani?

Hata hivyo China inaeleweka kwa rushwa inapokuwa inashughulika na miradi nje ya nchi. Tusifurahie tu kuona mradi unarudishwa tujiulize hawa akina spika na wengine wanapenda tu au wamepewa chochote china na ziara zao.
 
Aliye M misled Magufuli ni nani!??
 
Wnawake walikunja ngumi ... peoplessssss! Wao wanaitikia Power! kumbe pwaaaa!
 
Hawa wakubwa kwa jinsi wanavyoukumbuka mradi huu, sina shaka wana chao mfukoni tayari!
Mkuu, Mimi ninamashaka Sana Mh Sipika, kuna kaugali kake humo,

Si ni yeye aliyesemaga kuwa mradi huu Kweli Kwa masharti yaliyomo haufai??

Halafu leo anabadirika??
 
Siamini nachokisikia kwakweli!!!!!!!!!!!!
 
Hata Magufuli alishauriwa vibaya kumwondoa CAG Assad kisa kuhoji mabilioni aliyotumia Ndugai kwa matibabu.
Pamoja na kutoonyesha mkataba Magufuli alionyesha madhara ya mkataba wa bandari ya Bagamoyo yeye alipoenda China tutaamini vipi hakupewa rushwa
Hii ni sehemu ambayo JPM alikosea sana, now we know. Angemfungulia kesi ya uhujumu uchumi tu kng huyu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…