Lutandagula
JF-Expert Member
- Apr 8, 2018
- 1,762
- 2,154
Hawastahili kuongoza kwa sasa!Kweli nyinyi maccm ni ndumila kuwili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawastahili kuongoza kwa sasa!Kweli nyinyi maccm ni ndumila kuwili
Hapa sio fahamu kurudi bali ni fahamu kuhama. Yaani Bagamoyo iendelezwe kwa sharti bandari Dat, Tanga, Mtwara etc zisiendelezwe na mwekezaji apewe lease 99 years. TZ inafaidika au inaliwa? Au aliyeuidhinisha huo mradi kabla kajipenyeza kwa hiyo kamati na Ndugai wake akijua wanamwogopa bado?Kuna watu fahamu zinaanza kurudi- ile Kinga yako ya kutokushitakiwa ameshauriwa vibaya?
Mkuu haya mambo yalikuwa wazi kabisa. Ndungai ni mchumia tumbo tena kilaza wa kutupwa. Magufuli alikuwa anapenda watu kama hawa. Kichwani hamna kitu tumboni kuna tani mbili. Alidhani kina Lissu ni maadui kumbe walikuwa watu wema sana na wanataka kumsaidia afanye vizuri. Ohooo. mbona kila alichoasisi Magufuli kinasambaratika kwa kasi ya ajabu namna hii! Wale waliokuwa wanamsifia mchana kutwa ndiyo wamegeuka wapondaji. Haki watu wangekuwa wanarudi kutoka kaburini Magufuli asingeamini kinachotokea sasa hivi.Mkuu Yoda,
Naomba nami nipandie kwenye hoja yako hii ya "kutokuwa na Bunge Huru."
Naomba sasa tushirikiane kuwastua hawa wabunge wa CCM waliomo kwenye Bunge hilo.
Mfadhiri wao mkuu, KAONDOKA; hakuna tena anayewashikilia wasiweze kulifanyia haki taifa hili.
Kitu cha kwanza wanachopaswa kukifanya ni kusafisha takataka zilizoko huko Bungeni kwao kwa kuwaondoa katika ngazi za uongozi wapuuzi kama huyu Ndugai.
Ndugai bila ya mbeleko wa mtu mwingine (kama Magufuli), hana nguvu ya kumuyumbisha mtu yeyote. Huyu wamkatae asiwaongoze, wamwondoe haraka.
Wakishafanya hivyo, hapo ndipo itatakiwa wafanye kazi za wananchi ambao kiuhakika hawakuwachagua kwa hiari zao. Hapo watakuwa wamelifanyia taifa lao haki, na wartastahili kupewa heshima.
Unga ulipokuwa mashariki, aliufuata kwa mapambio, ikiwemo kutaka kutekeleza harakati za kumwongezea mungu mtu muda. Leo unga unaelekea magharibi, anaufuata.leo ndio nimeona wanasiasa hawawezi kuiona pepo kwa unafiki wao,huyu huyu ndugai aliwekwa pale na mzee leo anaongea haya kweli
Hawa si ni ''wachapa kazi '' wa Magufuli lakini? Si ndio alikuwa anawaamini na kusema wana uzalendo? Maskini mzee wa watu hakujua alikuwa amezungungukwa na mbwa mwitu. Alidhani kina Lissu ndiyo maadui zake kumbe walikuwa wazalendo na hawa kina Ndungai ndiyo maadui wa Taifa.
Tena aibu kubwa Spika anapigia debe mradi kuwa mzuri kwa ki presentation cha power point cha marketing officer wa kichina .Shame on him.LooKuwa na spika kama huyu ni aibu kwa taifa.
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo.
Ndugai amesema kuwa mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa Watanzania na tukichelewa hatutauta tena.
Magufuli alisema mradi huo ulikuwa ni hasara kwani ulikuwa na masharti magumu ikiwemo ya kuzuia bandari yoyote kuendelezwa, wala TRA kukusanya kodi na kupewa lease kwa miaka 99.
Pia soma: Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha
Ndiyo maana tulikuwa tunalilia uchaguzi huru. Haya ni matokeo ya Magufuli kuokoteza mabaki huku na huko.Mama Samia kaa chonjo kuna kundi la wezi eanataka kurudu hewani kwa spidi ya mwewe hata arobaini haijaisha walifungiwa kwenye banda la mifugo sasa wanatoka kwa kasi kurudi kula mazao shambani
Wanaanza kukunjua mikucha yao mchana kweupe hata bila haya
Mzee Ndugai na uzee ule rushwa hata kweli anafanya decision kuwa mradi mzuri kwa kuangalia presentation ya mchina !!! Nimekubali CCM tunaingiza baadhi ya watu wenye upeo mdogo bungeni Ndugai akiwemo.
Hao ndio watanzania wala usishangae, we jiulize una marafiki wangapi ambao ‘piga, uwa’ lazima wawepo.Du! Tujifunze kuweka akiba ya maneno, "mkono wa chuma" kafa leo Ndugai anamgeuka kweli wanafiki ndani ya CCM wapo wengi
Ajabu walioshauri mradi usijengwe ndiyo hao hao wanashauri mradi ujengwe.HApo kwenye bold....inaanzia kwenye familia, mtaani, makazini hadi TAiFA